Tuhuma za Uwongo dhidi ya Hizb ut Tahrir kutoka Redio/Tv Imani

8

 MKURUGENZI
ISLAMIC FOUNDATION
MOROGORO

Tafadhali husika na kichwa cha habari nilichotanguliza

 Tv/Redio Imani katika muendelezo wa kipindi chake cha “Jihadi na Ugaidi” kinachoendeshwa na Mohammed Issa, kilichokuwa hewani tarehe 03/07/2017 (na kurejewa 06/07/2017) kilitoa tuhuma nzito na za hatari dhidi ya Hizb ut Tahrir kwamba ni kundi la kigaidi. Tuhuma hii licha ya kuwa ni hatari kwa Umma wa Kiislamu pia  ni aibu na fedheha kwa mwendeshaji na kwa vyombo vya habari vya Imani vilivyopeperusha hewani.

Tuhuma hiyo haina hata tembe ya ushahidi, imevunja misingi ya Uislamu na hata hayo maadili yenu ya habari. Katika kipindi hicho cha “Jihadi na Ugaidi” ambacho mwendeshaji wake Mohammed Issa hujiwasilisha kama mwanafikra na mtafiti kashindwa hata kunukuu walau kijipande cha nyaraka ya Hizb ut Tahrir kuthibitisha madai yake. Bali tuna mashaka kamwe hata kama anajua kuwa Hizb ut Tahrir ina vitabu vingi vilivyoandika kufafanua kila nukta ya fikra inayoifuata kwa dalili za wazi.

Zaidi ya hayo tuhuma hiyo inapingwa hata na halihalisi, kwani tangu kuasisiwa kwa Hizb ut Tahrir haijawahi kuripotiwa popote duniani kutumia nguvu wala mabavu kufikia malengo yake bali kwa muda wote imekuwa ikitumia mchuano wa kifikra na kisiasa tu.

Tunapenda kuikumbusha taasisi yako kuwa tuhuma na kauli za uwongo dhidi ya Hizb ut Tahrir kutoka katika vyombo vyenu vya habari sio jambo geni.  Kampeni hiyo chafu ilishika nguvu zaidi mwishoni mwaka 2010. Na tulifafanua hilo kwa kina katika barua yetu ya malalamiko kwenu yenye Kumb : 2010/04  ya tarehe 26 Disemba 2010.

http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/kenyaa/993.html.

Aidha, tuna kila sababu ya kuamini kwa kuashiria (by implication) kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa  tuhuma na kauli hizo hutolewa kwa baraka za taasisi yenu.  Kwa mfano, katika tuhuma za Redio Imani juu yetu mwishoni mwa mwaka 2010 (kwenye link niliyoweka juu) vipindi kadhaa vyenye  ajenda za kupotosha kuhusu Hizb ut Tahrir vilipeperushwa kwa mfululizo wakati huo,  na baada ya ujumbe wetu kukutana na uongozi wa redio hiyo na kuwataka washikamane na masharti ya Kiislamu na ya maadili yenu ya kihabari kwa kuomba radhi, kusahihisha au kutupatia fursa ya kufafanua fikra zetu kufuatia tuhuma hizo, kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa licha ya kuwa Redio yenu kulazimika kufanya hayo chini ya maadili ya habari ya kuupatia upande wa pili fursa ya kusikilizwa (natural justice) kamwe haikutoa fursa hiyo.

Tuhuma hizi kali za sasa dhidi ya Hizb ut Tahrir zinazojiri leo ni muendelezo na matokeo yanayotarajiwa, kwa kuwa lau wakati ule Redio yenu ingeshikamana na masharti ya Kiislamu na maadili yenu ya kihabari tuliyowaeleza wakati ule, haya ya leo yangeweza kuepukika.

Tunapenda pia kutanabahisha taasisi yenu kwamba mwenendo wa vyombo vyenu vya habari kupeperusha tuhuma na kauli za uwongo baina yetu Waislamu ni jambo ovu, hatari na linadhoofisha umoja na udugu wa Umma wetu, udugu ambao sisi Hizb ut Tahrir licha ya tuhuma mbaya za awali tulizowahi kupachikwa na vyombo vyenu vya habari, kutofautiana na taasisi yenu katika baadhi ya fikra na misimamo yenu, bado tumekuwa tukichunga kwa umakini mkubwa mipaka ya umoja na udugu huo ambao kwa masikitiko makubwa taasisi yenu mnaonekana kutoujali.

Katika kuthibitisha hilo :

 1. Baada ya tuhuma za Redio Imani za awali za mwaka 2010, sisi Hizb ut Tahrir tulishikamana na ustaarabu na maadili mema ya Kiislamu kugharamika kwa kutuma ujumbe rasmi mjini Morogoro ili kuonana na uongozi wa Redio hiyo ana kwa ana na kufikisha rasmi waraka wa malalamiko yetu.
 2. Pia baada ya tuhuma zile za awali za Redio yenu, sisi Hizb ut Tahrir tulifikia maamuzi ya kusita kupeleka malalamiko yetu kwa Mamlaka ya Habari na Mawasiliano licha ya uzito wa tuhuma zile, kwa sababu  tu ya kuchelea huenda Mamlaka hiyo ingeweza kuchukuwa hatua za madhara dhidi ya Idhaa hiyo.
 3. Licha ya Redio yenu kutupachika tuhuma kadhaa za uwongo, kukataa kukanusha, kusahihisha, kuomba radhi au kutupa fursa ya kusahihisha na kujieleza kama tulivyowataka katika waraka wetu baada ya tuhuma zile, bado idhaa hiyo ilipopewa adhabu ya kufungiwa na serikali kwa muda wa miezi sita kupitia Mamlaka ya Habari na Mawasilinao, sisi kama Hizb ut Tahrir kwa maslahi ya udugu na umoja wa Kiislamu tulisimama kidete na kwa nguvu zote kupinga uonevu na dhulma mliyotendewa. Angalia hapa:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/kenyaa/1870.html

4.Hizb ut Tahrir inapokuwa na shughuli yoyote kubwa daima hutoa mwaliko kwa vyombo vyenu vya habari. Mfano mzuri wa karibu ni Kongamano letu la Kukaribisha Ramadhani liliokusudiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Shaaban (20 Mei 2017)

Kufuatia tuhuma hizi za sasa Hizb ut Tahrir Tanzania tunaitaka taasisi yenu iisimamie Tv/Redio yake kushikamana na masharti yale yale tuliyowahi kuyaeleza awali. Kwa kuwa hayo ndio masharti ya Kiislamu na pia yapo kwa mujibu wa maadili yenu ya habari, nayo ni :

 1. Mwendesha kipindi aombe radhi na arekebishe kauli yake juu ya uwongo na tuhuma alizotoa, afanye hivyo mara moja ndani ya kipindi kinachofuata katika muendelezo wa kipindi. Kama hawezi kufanya hivyo, Tv/Redio Imani itupe fursa sisi kufanya hilo. Tunasisitiza kuwa masahihisho hayo lazima yafanywe hewani kama zilivyokuwa tuhuma.
 1. Ikiwa mwendesha kipindi (Mohamed Issa) ana yakini juu ya ukweli wa kauli yake na ana ushahidi, basi Kiislamu na kwa mujibu wa maadili yenu ya habari pia hana budi kusita na kipindi, ili kuupa fursa upande wa pili kusikilizwa. Kwa sura hiyo (ya kuwa mwendesha kipindi ana ushahidi) tunalazimika na tunamtaka mwendesha kipindi (Mohammed Issa) ashiriki katika mjadala wa wazi nasi hadharani ndani ya kipindi cha wiki moja (kuanzia tarehe ya barua hii) ili apate fursa ya kuwasilisha ushahidi wake, nasi tupate fursa ya kusimamisha hoja juu ya hilo. Na kwa msingi huo Tv/Redio Imani watalazimika kuutangaza mjadala huo kabla, na kuupeperusha hewani utakapofanyika ili hadhira ipate fursa ya wazi wazi. Na sisi tuko tayari kwa mjadala huo wakati wowote, mahala popote pia tunampa fursa Mohamed Issa kupata msaada kutoka  kwa yeyote.
 1. Taasisi yako ikishindwa na kukataa kwa mara nyengine tena kukubali hatua (1&2) kama mlivyoshindwa awali, sasa itakuwa imedhihirika wazi zaidi juu ya ajenda ya hatari na uadui mliyobeba dhidi ya Uislamu na Waislamu wenzenu. Na litakuwa ni jambo la wajibu kujulishwa Waislamu juu ya uadui huo.

 

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut-Tahrir Tanzania

 

Nakala :

 Redio Imani

Tv Imani

Gazeti Imani

Mohammed Issa

Vyombo vya Habari

Jumuiya za Kiislamu

Waislam wote

 

Tel.: +255778 870609

Email: jukwalakhilafah@gmail.com

Hizb ut Tahrir Official Website

www.hizb-ut-tahrir.org

Hizb ut Tahrir Media Office Website

www.hizb-ut-tahrir.info

8 Comments
 1. So great to find someone with some original thoughts on this topic. Really..

 2. Live TV says

  I very delighted to find this internet site on bing just what I was searching for as well saved to fav .Live TV

 3. canlı fox tv izle says

  There is definately a lot to find out about this subject. like all the points you made .-mediathek vox

 4. hey dudes mens says

  Pretty! This has been a really wonderful post.any thanks for providing these details. – mens hey dudes

 5. air jordan 1 retro low og says

  Great post Thank you. look forward to the continuation.

 6. najlepszy sklep says

  Wow, awesome blog layout! How long have you been blogging for?
  you make running a blog glance easy. The total look of
  your website is great, let alone the content! You can see similar here sklep internetowy

 7. check that says

  Your insights mean a lot to me, thank you for sharing! hop over to this website

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.