Kubuniwa kwa Hizb ut Tahrir

Hizb ut-Tahrir imebuniwa kwa kuitikia mwito wa maneno ya Allah (swt):

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu na hao ndio walio fanikiwa”

[Aal-Imran:104]

Dhamira yake ni kuleta mwamko katika Umma wa Kiislamu kutokana na mporomoko mbaya uliofikia, na kuukomboa kutokana na fikra, nidhamu na sheria za kikafiri, pamoja na kutawaliwa na athari ya dola za kikafiri. Pia inalenga kurudisha serikali ya Kiislamu ya Khilafah ili kuhukmu kwa yale yote aliyoteremsha Allah (swt) kurudi tena.