Taarifa Kwa Umma Kuhusu Clip ya Hizb ut Tahrir Juu ya Sakata la Bandari

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Clip ya Hizb ut Tahrir Juu ya Sakata la Bandari

Kuhusiana na matumizi mabaya ya clip ya Hizb ut Tahrir Tanzania ya Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir ndugu Said Bitomwa, ambapo baadhi ya wafuasi wa Chadema na Maaskofu wanaitumia kwamba inaunga mkono msimamo wao, tunapenda kusema haya:

Ifahamike kwamba Hizb ut Tahrir haiungani na Chadema, Maaskofu wala DP World juu ya sakata la bandari. Kwani makundi yote hayo yanakubaliana juu ya ubinafsishaji au kuwekeza katika mali za Umma ila wanachotofautiana apewe nani na kwa masharti gani.

Msimamo wa Hizb ut Tahrir ambao ndio msimamo wa Kiislamu ni kwamba mali za Umma ni haramu kuwekwa chini ya mikono ya watu binafsi, shirika nk.

Mali kama mito, maziwa, bahari, fukwe, bandari, milima, vyanzo vikubwa vya maji   au umeme, gesi asilia, migodi mikubwa ya madini nk.  ni mali za Umma. Na kamwe Uislamu hauruhusu yoyote umiliki binafsi katika milki za Umma, hata iwe serikali(hairuhusiwi), bali serikali ina jukumu la usimamamizi tu.

Ni wazi wafuasi wa Chadema na Maaskofu ambao ni wadau na waumini wa ubepari wanafahamu fika kwaamba sera za kiuchumi za kibepari zinaruhusu kubinafsisha mali za Umma, bali mataifa ya kibepari ya kikoloni yanalazimisha nchi changa kamwe.

Sakata la bandari inaonekana linatumika na upinzani hususan Chadema kuwa mtaji mwanana wa kisiasa, likichapuzwa pia na chuki za kidini, kikanda na kijinsia.

Maaskofu, katika suala hili wanasukumwa na chuki zao binafsi za kidini na mazoea yao ya kurambishwarambishwa makombo na mabepari tangu zama za ukoloni, na mpaka zama hizi za uhuru wa bendera, wamezoea kudekadeka pale wanapohisi kupoteza rambaramba. Upingaji wa maaskofu ni maslahi binafsi na sio kwa maslahi ya Umma, kwani ubepari umekua ukilitumia kanisa kubeba ajenda zake kama usekula, ushoga nk. Hivyo, wamezoea maaskofu duniani kuonjeshwaonjeshwa asali kwa kufanyia kazi ajenda za kibepari ikiwemo pia kwenye mikataba ya kinyonyaji.  Hata hivyo, maaskofu wanajitia upofujuu ya ukweli kuwa nyuma ya kampuni ya DP World kuna serikali za Ulaya hususan Uingereza.

Hizb ut Tahrir Tanzania haikubaliani na ubinafsishaji wa mali zote za Umma na sio bandari tu. Sera hiyo haitokoma mpaka pale mfumo wa kibepari utakapokomeshwa duniani.

 

AFISI YA HABARI

HIZB UT TAHRIR TANZANIA

08—09—2023 MILADI / 23 SAFAR 1445 HIJRIA

Maoni hayajaruhusiwa.