Kwanini Majeshi Ya Nchi Za Waislamu Yanachelewa Kuinusuru Gaza

بسم الله الرحمن الرحيم

Tangu kuanza kwa uvamizi wa majeshi ya Israel katika eneo la Gaza tarehe 27/10/2023, kuna uharibifu mkubwa sana umetokea hususan kwa upande wa Palestina. Kuna jumla ya vifo takribani 36,000, majeruhi 80,011, hospitali 31, shule 613, nyumba za makaazi 370,00, misikiti zaidi ya 600, waandishi wa habari 148, vyuo vikuu 12 na kadhalika.
Baada ya athari zote hizi, kuna masuluhisho mbalimbali yanayotolewa kukabiliana na mauaji haya ya halaiki ya raia wasiojiweza wa Palestina. Miongoni mwa masuluhisho hayo ni pamoja na kuifungulia mashataka Israel katika Mahakama za Kimataifa ya Uadilifu(ICJ) uliofanywa na Afrika Kusini, au kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa viongozi wa Israel ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu iliyotolewa na Mahakama ya Uhalifu wa Kivita(ICC) chini ya Muendesha Mashtaka wake Mkuu Karim Khan. Suluhisho hili si sahihi kwani mahakama hizi zimeundwa na wakoloni ambao ndiyo walioanzisha kijitaifa haramu cha Israel. Hivyo, hawawezi kutoa haki kwa Palestina kama inavyoshuhudiwa
Suluhisho lingine linalotolewa ni suluhisho la kuwepo kwa nchi mbili katika ardhi ya Palestina, yaani nchi ya Palestina inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, na nchi ya Israel inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Suluhisho hili si sahihi kwa vile linatoa nafasi kwa wavamizi wa Kizayuni kuunda taifa ndani ya nchi ya watu wengine ya Palestina. Hivyo, ni suluhisho butu linaloegemea upande mmoja.
Jambo lingine ambalo linatajwa kama suluhisho la kukomesha mauaji haya kwa raia wa Palestina wasio na silaha ni kuwepo kwa jeshi la kulinda amani, na Hammas kuweka silaha chini. Panasemwa hii itatoa fursa ya majadiliano na hatimae kukomesha kabisa mauaji. Suala hili kama yalivyopita masuluhisho mawili ya mwanzo pia si muafaka kwavile linawalazimisha waliovamiwa yaani Palestina kuacha kupigana na mvamizi wa ardhi yao .
Amma suluhisho linalofaa ni moja tu, nalo ni majeshi miongoni mwa majeshi ya Waislamu kama vile jeshi la Misri, Jordan, Lebanon, Uturuki nk. kuingia Gaza kuwahami ndugu zao. Suluhisho hili ni muafaka kwa vile linatoa haki na uwiano wa mapigano. Kama ambavyo jeshi la Israel lenye vifaa na weledi linapigana likisaidiwa na Marekani, Uingereza, Ujerumani na nchi nyingine nyingi za Ulaya, itakuwa muafaka iwapo upande wa Palestina pia badala ya kupigana na kikundi kidogo cha watu cha Hammas basi wapigane Israel na jeshi la kinchi kama lao lenye silaha na usaidizi kutoka nchi nyingine pia.
Suluhisho hili litakomesha vita na mauaji kwani bila shaka kushindwa kwa Israel katika hali hii ni jambo la kutatajiwa. Ikiwa Israel pamoja na kusaidiwa na nchi nyingi kubwa za Ulaya na Marekani lakini bado ameshindwa kupiga hatua yeyote muhimu ndani ya miezi zaidi ya nane katika uwanja wa vita, ikiwa ni pamoja na kushindwa kujua hata eneo walipo Hammas, na badala yake anahamishia hasira zake kwa raia na kuripua shule, hospitali, masoko na makambi ya wakimbizi nk. Ni wazi endapo Hammas watapata msaada kama wanaopata Israel basi Israel itashindwa vita hivi.
Kama hili ndiyo suluhisho muafaka, swali la msingi linakuja ni kwanini sasa majeshi katika biladi za Kiislamu licha ya kuona namna majeshi ya Wamagharibi wakisaidia Israel na kufanya mauaji ya halaiki ya ndugu zao bado wanachelewa kwenda kuwasaidia ndugu zao wa Gaza?
Sababu zipo nyingi lakini leo tutaangazia baadhi ya sababu hizo.
Miongoni mwa sababu hizo ni suala la uzalendo. Fikra hii chafu ya uzalendo ilipomakinishwa katika vichwa vya Waislamu, na Uislamu haukuwa tena muongozo wao bali wakaongozwa na matakwa ya nchi zao kuzingatia mipaka ya kijografia iliyochorwa na wakoloni makafiri. Kwahiyo, mtu huona suala la Palestina ni la wapalestina na yeye Mmisri kwa mfano halimuhusu. Hali hii ni miongoni mwa vikwazo vikubwa vya kuikomboa Gaza na Palestina kiujumla kutoka katika makucha ya Mazayuni
Amma kwa upande mwingine, ni maslahi ambayo wanayapata wanajeshi ya mishahara mikubwa na marupurupu. Baada ya kipimo cha halali na haramu kutolewa katika maisha ya Waislamu, na badala yake kuwekwa kipimo cha ‘maslahi’ ya kushikika imekuwa ni vigumu kwa wanajeshi kuacha maslahi ya kidunia na kuvunja minyororo ya watawala na kuvuka mipaka kuikomboa Gaza na Palestina
Sababu nyingine kubwa ni msukumo hafifu wa Waislamu katika kuliendea jambo hili. Katika suala hili Waislamu wamegawanyika makundi makuu manne:
Kundi la kwanza ni wanaotaka misaada ya kibinadamu tu iwafikie watu wa Gaza bila kwenda mbali na kupata suluhisho la kudumu, mfano wao ni Waziri wa Saudia Faisal Farhan alipokutana Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken tarehe 14 Oktoba, 2023 alisisitiza kuhusu hili kana kwamba misaada pekee itatoa haki kwa Palestina.
Kundi la pili: ni wanaotaka suluhisho la nchi mbili. Kwa mfano, Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) Riim Ibrahim Al-Haashimiy, katika kikao cha Baraza la Usalama cha Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 24/10/2023 alisisitiza kuhusu suala hili bila kujali kuwa litapora haki ya Palestina
Kundi la tatu ni wanaowapinga Hammas, wanataka Hammas wasalimishe silaha, waache mapigano nk. Hapa mfano mzuri ni Imamu wa Masjid Qubaa mjini Madina Sheikh Sulaiman Alrahiil alisema “Ni haramu kupeleka msaada (Gaza) ila kwa idhini ya mtawala wa nchi yako” . Pia Sheikh Salim Twawiil yeye akaenda mbali zaidi na kusema “kwanza, Aqswa kwetu siyo muhimu hakuna agizo toka kwa Mtume (SAAW) na ndio sababu hata yeye mwenyewe Mtume maisha yake yote hakuwahi kwenda Aqswa (zaidi ya siku ya Israa na Miraaj)”
Kundi la mwisho ni la kiasi fulani cha Waislamu wanaotaka majeshi ya nchi za Waislamu waende kuwanusuru Waislamu wa Gaza. Kundi hili liliopo sawa bado halijatoshia kuwashawishi majeshi kuvunja minyororo waliyofungwa na watawala na kuvuka mipaka na kuwahami ndugu zao wa Gaza na Palestina hali ya kuwa sehemu kubwa ya Umma wa Kiislamu bado umelala ukiota ndoto za masuluhisho ya Kimagharibi ambayo yanawakandamiza ndugu zao wa Gaza, kama vile suluhisho la nchi mbili, kujikita katika dua na misaada pekee na kuwashawishi Hammas waweke silaha chini.
Hivyo, tunatoa mwito kwa Waislamu dunia nzima kupaza sauti na kuungana katika mwito wa kuwataka majeshi katika biladi za Kiislamu hususan Misri kutoka mara moja kwenda kuwahami na kuwanusuru watu wa Gaza na Palestina kiujumla.
Tunayakumbusha majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu yana dhima kubwa mbele ya Muumba wao. Hivyo, yatoke mara moja kwenda kuikomboa Gaza na Palestina bila kukata tamaa, bali wawe na matarajio ya Janna ya Allah Taala.
Aidha, tunayataka majeshi hayo yatoe nusra yao ili isimamishwe dola ya Khilafah ambayo itauhami Uislamu, Waislamu na biladi zao.
“Damu ya Gaza inaendelea Kumwagwa”
Risala ya Wiki No. 182
24 Dhu -al Qidah1445 Hijria | 31 Mei 2024 Miladi
Afisi Ya Habari – Hizb Ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.