Mwito wa Dhati kutoka Tanzania: Majeshi ya Nchi za Waislamu Yaende Haraka Kuinusuru Ghazza

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Kufuatia kampeni dhidi ya mauaji ya halaiki, mateso na dhulma kwa Waislamu wa Ghazza yanayotekelezwa kwa ukatili na kijidola bandia cha waporaji ardhi cha Mayahudi kwa msaada wa Marekani na madola mengine ya Magharibi, Hizb ut Tahrir Tanzania imeifanya rasmi siku ya Ijumaa (31 Mei 2024) kwa ajili ya dua kwa ajili ya Waislamu wa Ghazza katika misikiti mbali mbali Tanzania.
Dua hizo ziliambatana na Khutba na mihadhara zikipaza sauti dhidi ya mauaji ya halaiki na kuoneshwa suluhisho la Kiislamu na jukumu la kisharia linaloyataka majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu hususan Misri kuingilia kati kijeshi haraka ili kukifutilia mbali kijidola bandia cha Israil na kuwaokoa Waislamu wa Palestina na pia kuukomboa msikiti mtakatifu wa Al -Aqswa.
Aidha, khutba na mihadhara hiyo ziliwakumbusha Waislamu kwamba uwepo wa dhulma, mateso na mauaji ya halaiki kwa Waislamu ndani ya Ghazza na pengine ni matokeo ya kutokuwepo kwa dola ya Kiislaumu ya (Khilafah). Jambo linalowafanya Waislamu dunia nzima kuwa na jukumu na dhima ya kisharia kuirejesha tena dola hiyo kwa kuanzia katika ulimwengu wa Kiislamu. Kwa dola hiyo ndio tawezekana kuepusha mauaji ya kikatili na dhulma visitokee tena.
Dua, Khutba na mihadhara vilifanyika katika baadhi ya misikiti ndani ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga nk., ambapo Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya 𝐇𝐢𝐳𝐛 𝐮𝐭 𝐓𝐚𝐡𝐫𝐢𝐫 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 Sheikh Musa Kileo aliongoza dua katika Masjid Rahma, Buguruni jijini Dar es Salaam.
Tunamuomba Allah Taala Awazidishie ndugu zetu wa Ghazza istiqama (msimamo), Awamiminine zaidi subra, na Awaharakishie ushindi, kwao, na kwa Waislamu wote mashariki na magharibi – Amiin
Kumb: 1445/09
31 /05/2024
Ijumaa 23 Dhul Qi’dah 1445 H

Maoni hayajaruhusiwa.