Sheikh. Taqiuddin an-Nabahani

Alizaliwa 1332 Hijria au 1914 Miladia

Taqiuddin bin Ibrahim bin Mustafa bin Ismail bin Yusuf an-Nabahani (mwanzilishi wa Hizb ut Tahrir) anatoka katika kabila la Bani Nabahan na anatoka kijiji cha Ajzam mji wa Haifa eneo la Kaskazini mwa Palestina. Familia yake ilijulikana kwa elimu, kushikamana na dini na uchaMungu.  Babake, sheikh Ibrahim, alikuwa ni mwanachuoni wa fiqh na msomi wa ‘Ulum ash-Sharai,’ ambayo aliipata kutoka kwa babake sheikh Yusuf an-Nabahan.

Riwaya tofauti tofauti zimemtaja babu yake mzalia mamake Sheikh Yusuf Nabahani kwa maneno haya: Yusuf bin Ismail bin Yusuf bin Hassan bin Mohammad Al Nabahani Al Shafii’ – kunya yake (jina la lakabu) ilikuwa Abu al Mahasin na alikuwa mshairi, Sufi na msomi. Alichukuliwa kuwa miongoni mwa makadhi wazuri zaidi wa zama zake. Alihudumu kama kadhi katika eneo la Jenin lililounganishwa na Nablus. Baadaye, alihamia Istanbul ambako alihudumu kama kadhi katika eneo la Kavi Sanjaq mjini Mosul. Hatimaye aliteuliwa kama mkuu wa mahakama ya kifalme eneo la Al-Azqya na Al-Quds. Na kisha alichukua usimamizi wa Mahakama ya Haki ya Beirut. Ameandika vitabu arubaini na nane.

Shakhsiyya ya Kiislamu ya Sheikh Taqiuddin kwa kiwango kikubwa ni matunda ya msingi wa familia yake. Hivyo basi, alihifadhi Qur’an Tukufu akiwa na umri wa miaka 13. Alivutiwa sana na elimu na utambuzi wa babu yake mzalia mama na kupata kutoka katika bahari hii ya elimu, kadri kile alichoweza kuchukua. Tangu mwanzoni, alipata utambuzi wa kisiasa hususan kutoka kwa zile harakati za kisiasa ambazo babu yake alizianzisha kuisaidia Khilafah ya Uthmaniyya. Sheikh huyu alinufaika pakubwa kutokana na majadiliano ya kifiqhi ambayo yaliandaliwa na babu yake Sheikh Yusuf. Ni wakati wa mijumuiko hii ndipo alipovutia umakinifu wa babu yake kwake. Hivyo basi, Sheikh Yusuf alimshawishi babake Sheikh Taqi kumpeleka Chuo Kikuu cha Al Azhar kwenda kupata elimu ya ‘Uloom Ash-Sharaii’.

Kupata Elimu:

Sheikh Taqi alipokewa na kujiunga katika daraja ya nane katika Chuo Kikuu cha Al Azhar mnamo 1928 na kumaliza mtihani wake kwa alama ya juu zaidi ya ‘Distinction’ mwaka huo huo. Alipewa cheti cha ‘Shuhada Al Ghurba’. Baada ya hapa alijiunga na kuliyya ya sayansi ambayo ilikuwa imeunganishwa na Chuo Kikuu cha Al Azhar wakati huo. Alikuwa akihudhuria makongamano ya kielimu ya wale wanavyuoni ambao babu yake alimuongoza kwao mfano ni Sheikh Mohammad Al Khizar Hussain (Rahimahullah). Katika mbinu ya kizamani ya kusomesha iliruhusika kwa wanafunzi kuhudhuria halaqa za aina hiyo.  Sheikh an Nabhani daima alibakia kuwa mwanafunzi hodari; hata ingawa pia alikuwa na majukumu ya kimasomo katika Kuliyya ya Sayansi, wakati huo huo pia alikuwa akihudhuria makongamano ya kielimu. Wanafunzi wenzake na walimu walikuwa wakimuonea wivu kutokana na kina cha ufahamu wake, alielimika kwa rai na mijadala ya kukinaisha, ambayo aliiwasilisha katika midahalo iliyofanywa jijini Cairo na biladi nyenginezo za Kiislamu.      

Sheikh alipata shahada hizi: Shahada ya Wastani kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar, Shahada tal Ghurba kutoka Al Azhar, kufuzu katika lugha ya Kiarabu na fasihi kutoka Cairo, Dar al ‘Uloom, shahada ya ukadhi kutoka Mahad al A’laa – taasisi ya mafunzo ya mahakama iliyo unganishwa na Al Azhar na Shahada tal ‘Alamiyyah katika sharia kutoka Al Azhar (shahada ya uzamili) mnamo 1932 M.

Afisi Alizofanya kazi Sheikh:

Sheikh alihudumu katika kitengo cha elimu za sharia cha Wizara ya Al-Ma’arif hadi mnamo 1938 M. Kisha kupandishwa cheo na kupewa uhamisho katika Mahakama za Sharia na kuteuliwa kuwa mwanasheria katika Mahakama Kuu ya Haifa. Baada ya hapo alipandishwa ngazi katika cheo cha msaidizi wa kadhi. Kisha alihudumu kama kadhi katika Mahakama ya Ramallah hadi mnamo 1948 M. Baada ya uvamizi wa Mayahudi wa Palestina, aligura kwenda Syria lakini kisha kurudi Palestina mwaka huo huo na akateuliwa kuwa kadhi wa Mahakama ya Sharia ya Al-Quds. Kisha alihudumu kama kadhi wa Mahakama Kuu ya Sharia hadi mnamo 1950 M. Baada ya hapo, alijiuzulu wadhifa wa ukadhi na kuwa mwalimu katika Kuliyya ya ‘Uloom Al-Islamia ya Oman. Sheikh (Rahimahullah) alikuwa bahari ya elimu; alikuwa gwiji katika kila fani ya elimu. Alikuwa mujtahid mkubwa na Muhadith.

Vitabu Vyake:

1. Nidhamu ya Uislamu

2. Muundo wa Chama

3. Mafahimu ya Hizb ut Tahrir

4. Nidhamu ya Uchumi katika Uislamu

5. Nidhamu ya Jamii katika Uislamu

6. Nidhamu ya Utawala katika Uislamu

7. Katiba (Dola ya Khilafah)

8. Utangulizi wa Katiba

9. Dola ya Kiislamu

10. Shakhsiyya ya Kiislamu (Mijeledi Mitatu)

11. Fahamu za Kisiasa za Hizb ut Tahrir

12. Fikra za Kisiasa

13. Mwito wa Harara

14. Khilafah

15. Tafakuri

16. Uwepo wa Akili

17. Nukta Kianzilishi

18. Kuingia katika Jamii

19. Lislah al-Misr

20. Al Ittifaqiyat as Saniya al Mastiya al Suriya wal Yamania

21. Hal Qadeeh Falasteen ‘ala Tareeqa tal Amreekya wal Engleezia

22. Nazrya al Faragh al Syasi Hol Mashroo’ Eezan Hawar

Na kuna mamia ya Makala ya kifikra, kisiasa na kiuchumi vile vile. Kabla ya kuasisi Hizb, aliandika vitabu viwili: Anqaz Falasteen (Uokozi wa Palestina) na Risala tal ‘Arab (Risala kwa Waarabu).