Harambee ya Makonda ni Aibu

7

Vyombo vya habari kadhaa vimeangazia kadhia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kuwataka wanawake waliotelekezwa na waume zao kwa kukoseshwa fedha za kuwahudumia watoto kufika ofisini kwake ili kupatiwa msaada wa kisheria. Wito huo umeitikiwa na mamia ya wanawake wakiwa na watoto hao kufurika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo tarehe 09/04/2018. Zoezi hilo likifanikishwa na timu ya madaktari, jeshi la polisi – Dawati la jinsia, wataalamu wa sheria, pamoja na maafisa ustawi wa jamii.

Pamoja na ukweli kuwa tukio hili limebuniwa kufikia malengo fulani ya kisiasa ya kuchafua haiba ya wale wanaoonekana kuwa na ushawishi wa kisiasa hasa katika ngome ya upinzani, pia tukio hili limedhihirisha aibu kubwa kwa Taifa katika nukta kadhaa.

Limetoa taswira ya zama zile zinazoitwa zama za kijahiliya ambapo jamii huwa na fikra duni kiasi ya baba kumtupa mwanawe. Na hili lategemewa kwa Taifa lenye mustawa duni wa kimaadili kama Tanzania, Taifa ambalo limefungua milango kwa hadhara ngeni ya kimagharibi, likafungua milango kwa kila aina ya uchafu kama vile pombe za kila aina, mabaa kila kichochoro, ugawaji wa kondom kila pembe huku wakipewa uhuru wa kutembea uchi kwa anaetaka kwa sababu tu wote hao wamedhaminiwa uhuru wao kutoka kwa Taifa lenye kujinadi kwa kujifunga na misingi ya kidemokrasia.

Limetupa taswira ya uozo wa kimaadili uliopo nchini ikiaminika kuwa, kesho yake lau Tanzania ikipiga mbiyu ya mgambo na kuita watoto wa mitaani katika uwanja wa Taifa basi uwanja huo utafurika.

Tukio hili nimetoa taswira ya uduni wa huduma za kijamii zinazotolewa nchini, kwani kuna akina mama kadhaa wamekuja hapo kwa aibu na lau kama wangalikuwa wanapata huduma bora za kijamii ambazo ni haki kutolewa kwa kila raia kamwe wasingeweza kujitokeza katika fedheha kama hiyo. Lakini pia, vipi wimbi la walemavu, wazee na wasiojiweza ambao wametapakaa kila kichochoro cha Mkoa wa Dar es Salaam wakiomba walau wapate pesa ya kununua kikombe cha chai, hao bado hawajaonekanwa au wametelekezwa na nani?.

La aibu zaidi ni pale mwezi wa July, 2016 Serikali ilipofanya msako ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa – Paul Makonda, msako wa kuwasomba na kuwatia mbaroni mafukara wanaoomba Dar es Salaam. Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa kutoa agizo kwa raia wenye huruma kutowasaidia mafukara hao. Katika msako huo zaidi ya ombaomba 60 walitiwa mbaroni na kwa wale wanaotoka maeneo ya mikowani kuambiwa watarejeshwa kwao, hii ni dharau na kuwacheza shere raia kwa yule anaenadi eti awahurumia watoto waliotelekezwa.

Aidha, twaiona Serikali inashindwa kuwasaidia raia wanyonge wanaosibiwa na mafuriko na wala hawana pakukaa na Serikali kupaza sauti ya kuwafukuza bila kueleza wapi waelekee.

Tukiangalia upande wa pili yaonekana wazi kuwa tukio hili limeletwa kwa lengo la kuwazuga raia tu kwani limeletwa wakati ambao Serikali imeshindwa kuleta majibu ya mambo kadhaa ya msingi hususan suala la usalama, kama kuwepo mauaji holela ya raia na waumini yanayoendelea mpaka katika nyumba za ibada pamoja na utekaji nyara wa ajabu unaofanywa na Serikali kwa kisingizio cha uvunjwaji wa sheria za kimtandao. Utekaji nyara huu unaongeza maradufu wimbi la wajane na mayatima ambao eti Serikali haitaki watelekezwe.

Upazaji sauti wa kulani unyama huu unaoendelea nchini umekua ukifanywa na vyombo vya habari, raia na hata baadhi ya wabunge kusema barazani kuwa wahalifu wanashirikiana na vyombo vya dola, bado Serikali imekua kiziwi, bubu, na wala haioni. Sasa ni kichekesho kwa serikali eti yawatafuta wanaotelekeza wanawake na watoto.

Kwa kweli taswira ya umma mkubwa uliojitokeza imetoa uhalisia wa uozo wa kimaadili na uduni wa fikra walizonazo ummah juu ya kuwaangalia wanawake, watoto na wanaadamu wenziwao, na hapo Serikali imedhihirisha kushindwa kutibu fikra hizo.

Njooni katika uislamu muangalie Mtukufu wa Darja Mtume SAW kupitia hadithi iliotoka kwa Abuu Huraira kwa kusema;

 “Muumini aliekamilika imani yake ni yule alie na tabia nzuri zaidi, na wabora wenu ni walio bora kwa watu wake (familia)” (Imepokewa na Tirmidhy)

Uislam umefungamanisha mahusiano ya mke na mume kupitia mkataba wa ndoa, na kwa mkataba huo pekee ndipo baba huwa na uhalali wa umiliki wa mtoto husika. Hii inamaana kwamba baadhi ya mababa wanaodaiwa kumiliki watoto hao kamwe hawatambuliwi kuwa baba halali wa watoto ikiwa tu kumekosekana mkataba wa ndoa awali, bila kujali vipimo vya vinasaba (DNA) vimeonesha kufanana au la, bila kujali muda gani wameishi pamoja mwanamke na mwanamume kwani vyote hivyo, si vipimo vya DNA wala muda wa kuishi pamoja havina nafasi katika kuthibitisha umiliki wa mototo katika sheria ya Kiislam.

Kinachoweza kusemmwa ni kuwa kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa usimamizi wa watawala wa Serikali ya Kiislam – Khilafah pale Amiril- Muuminiina Omar Bin Abdil-Aziiz akinunua ngano na kuzimwaga Milimani ili ndege wale, seuze wanaadamu. Kuna ya kujifunza pale watawala kama Amiril- Muuminiina Omar Bin Khattab akipita usiku wa manane kuangalia mwenye shida ili atatue yanayowasibu, wewe wapita usiku wa manane na kuwapakia kwenye makarandinga ili uwashtaki na kuwarejesha mikowani ulikoomba kura kwa unyenyekevu.  Ila hilo si la fedheha kwenu kwani ndio asili ya tawala za Kibepari zinazoendeshwa kwa ulaghai na ujanja wenye msingi wa ulafi na maslahi binafsi.

Mwisho lazima tukubali kuwa Uislamu pekee ndio umeweza kuweka utawala uliojaza huruma na mapenzi ya kweli kati ya wanadamu na kujaza mapenzi kati ya raia na watawala wao, na taswira halisi ya utawala kama huo itashuhudiwa karibuni pale itakaporudi tena Khilafah raashida ambayo miale yake imeanza kuchomoza kila pembe ya dunia, nasikuhiyo waumini na ulimwengu mzima utafarajika.

Yaasin Muombwa

7 Comments
  1. So great to find someone with some original thoughts on this topic. Really..

  2. Live TV says

    A big thank you for your blog.Really looking forward to read more.<a href="https://www.google.com.mt/url?sa=t

  3. watch irib 3 live says

    Very nice blog post. definitely love this site.tick with it!-vox lice

  4. hot deals says

    I think the admin of this site is really working hard for his website since here every stuff is quality based data.Acer Nitro 27″ WQHD 2560 x 1440 PC Gaming IPS Monitor | AMD FreeSync Premium Up to 180Hz Refresh 0.5ms DCI-P3 95% 1 Display Port 1.2

  5. kids hey dude shoes says

    Definitely what a great blog and instructive posts I definitely will bookmark your site.All the Best! . – hey dudes mens

  6. mens slip on dress shoes says

    I appreciate you sharing this blog post.hanks Again.

  7. see this here says

    The scenery is breathtaking, thank you! learn this here now

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.