Tangazo la Mwandamo wa Mwezi wa Shawwal wa Mwaka 1440H na Tahnia za Sikukuu yenye Baraka ya Idd ul-Fitr

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lillahi Alhamd

(Imetafsiriwa)

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, Bwana wa Ulimwengu, Mwenye Nguvu Pekee anayewaangamiza madhalimu, Aliyeupa Utukufu Uislamu na Waislamu. Amani na baraka zimwendee Mtume aliyetumwa kama rehema kwa ulimwengu, bwana wetu Muhammad, bwana wa viumbe na Mtume wa mwisho ambaye ndiye kiongozi katika kujifunza njia sahihi na familia yake na maswahaba zake na wale wanaomfuata kiusahihi mpaka Siku ya Hukumu…

Ahmad amevua kutoka Muhammad Bin Ziyad kwamba alisema kuwa, nilimskikia Abu Hurairah (ra) akisema: kwamba Mtume (saw) alisema, au alisema: Abu Al-Qasim (saw) alisema: «صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ»“Funga kwa kuuona mwezi na fungua kwa kuuona mwezi wa. Lakini lau kutakuwa na mawingu (hauku uona mwezi) kamilisha siku thelathini.”

Baada ya kufanya uchunguzi juu ya mwezi mpya wa Shawwal baada ya kuchwa kwa jua siku ya Jumatatu, kuamkia Jumanne, tunadhibitisha kuonekana kwa mwezi mpya kwa mujibu wa vigezo vya Shari’ah. Hivyo basi, kesho, Jumanne ni siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na ni siku ya kwanza ya Idd ul-Fitr yenye baraka.

Katika Sikukuu hii ya Idd ul-Fitr yenye baraka, Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi anawapa tahnia watu wote wa Ummah huu mtukufu wa Kiislamu, na anamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuturuzuku fadhla Zake za kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itatekeleza Shari’ah za Mwenyezi Mungu juu ya ardhi na kuulingania Uislamu duniani kama ujumbe wa muongozo na nuru, Dola ya Uadilifu itakayokomboa ardhi na kuleta uadilifu kwa watu; Dola ya Jihadi ambayo itafungua ardhi kama ilivyofanya hapo zamani na watu watapiga takbira katika Idd zao na kufunguliwa kwa ardhi: Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, la ilaha ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lillahi Alhamd.

Pia ni furaha yangu kutoa tahnia zangu na zile za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wale wote wanaofanya kazi ndani yake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir  na kwa Waislamu wote kwa ajili ya Idd ul-Fitr hii yenye baraka. Eid hii Mwenyezi Mungu ameileta iwe ni furaha kwa wenye kufunga na alama ya umoja wa Waislamu, na ukumbusho kwao kuwa ni Ummah mmoja tofauti na watu wenginewote.

Na kwa Waislamu wote duniani kutoka mashariki hadi magharibi, kwa watu walio na msimamo wa Ash-Sham na watu wa Murabiteen wa Ardhi Tukufu (Palestina), watu wenye subra wa Yemen, watu wa mapinduzi wa Sudan na Algeria, Waislamu wa Uchina walio na matumaini ya malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Waislamu wanaokandamizwa wa Burma na Waislamu Mujahidina wa Kashmir… Enyi ambao mlikuwa mnafunga, mkisimama katika ibada, mkiabudu na kufanya kazi, tahnia za Idd yenu ya Idd ul-Fitr ya baraka ziwafikie.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar

Enyi Waumini, njooni katika Idd yenu huku vifua vyenu vikiwa vimepanuka kwa furaha kwa yale mliyoyatoa katika ibada zenu katika mwezi wenu; na uonyesheni ulimwengu furaha yenu katika nyuso zenu kwamba mumebarikiwa kwa ibada za mwezi wa Ramadhani, ili kufaulu katika maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):  [سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ] “Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu.” [Al-Fath: 29].

Na waonyesheni wakoloni Makafiri Wamagharibi na vibaraka wao makhaini, watawala wa Waislamu, kupitia nyuso zenu nguvu na ari muliyopata kutoka kwa itikadi tukufu ya Uislamu. Waonyesheni kuwa nyinyi ni taifa ambalo mmepewa ahadi na Mwenyezi Mungu, na linaelekea kufikia lengo lake lililowekwa na Mtume (saw) nalo ni lengo la kujifunga kikamilifu na kamba ya Mwenyezi Mungu wote kwa pamoja nyuma ya Imamu mmoja, Khalifah mchamungu na muadilifu ambaye atarudia sera ya Makhalifa waongofu. Atayaunganisha majeshi na nguvu za Ummah, ata wekeza katika manufaa na khair ya nchi. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu atafungua milango ya mema kupitia nyinyi kwa ajili yenu na watu wenu, na kurudisha tena matumaini katika dunia hii kwa kuongozwa na taifa bora ambalo limetumilizwa kwa wanadamu, Ummah ambao ni bora kuliko mataifa yote duniani ili kuujenga ulimwengu na kuwa katika hali inayomridhisha Muumba wake.

Enyi Waumini, uwezo wenu na njia yenu kufikia khair hiyo inayosubiriwa ni kupitia kurudisha tena Dola ya Khilafah, dola ambayo muliwachiwa na Mtume wenu, bwana wa viumbe Muhammad, mbora wa amani na baraka zimwendee yeye.

Hizb ut Tahrir na waasisi wake, Mafuqaha’ wake na Mashabab wake wameichunguza Seerah ya Mtume Muhammad (saw), wamesoma vitendo vyake, wametathmini matamshi yake na kufuata mtizamo wa wanachuoni wakubwa na Mujtahidina walioacha mengi katika dini hii, wafahamu kwamba njia ya Mtume (saw) ya kisiasa na kusimamia mambo ya watu kutokana na muundo wa Maswahaba kutokana na kutangazwa kwa dola ya Kiislamu ndani ya al-Madina al-Munawarah. Hivyo basi, wameifahamu njia yake na kuipata njia iliyopotea inayoelekeza huko, na ramani ya muongozo wa Mtume ili kurudisha tena Dola ya Khilafah, dola ya Abu Bakr, Omar, Othman na Ali, Khilafah Rashidah (Makhalifa waongofu) kwa njia ya Utume.

Enyi Waislamu, Wamagharibi wako makini kuwaweka mbali na Wabebaji Da’wah wa Hizb ut Tahrir. Hivyo basi, ondosheni kizuizi hicho kiovu na songeeni mbele muungane na Mashabab wa Hizb ut Tahrir, na waulizeni kuhusu yale mema wanayolingania juu yenu, kwani wao ni miongoni mwenu na wanatokana nanyi popote pale Waislamu walipoenea, na mukiwauliza mutawapata wamewakunjulia mikono yao na vifua vyao vikiwa tayari kuwafikishia waliyobeba kiufahamu na kimaono… Musipoteze nafasi ya kujua njia ya ukombozi na kisha unganeni mikono ili Mwenyezi Mungu awabariki nyinyi na wao kwa ushindi na nguvu.

Enyi Waislamu popote mulipo, furaha yenu katika Idd hii ni ibada kwa Mola wenu, kunawirisha nishati zenu, kufuta wasiwasi wenu na uovu wa adui wenu. Hivyo basi, pigeni Takbeer na Tahleel, furahini na enezeni furaha na kisha fanyeni kazi na wafanyikazi.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar

Eid Mubarak na Mwenyezi Mungu atakabalie ibada zenu na zetu.

Wasalaamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu

Kuamkia Jumanne ni siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal wa Mwaka wa 1440 H sawa na 4 Juni 2019 M

Mh. Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Na: 1440 H / 033

29 Ramadan 1440

Jumatatu, 03 Juni 2019

Maoni hayajaruhusiwa.