Hadithi za Mtume (Saw) Ambazo Zinakataza Bei Mbili Ndani ya Moja na Mikataba Miwili Ndani ya Mmoja

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullah,

Swali kuhusu bei:

Tunataka kukodi ardhi kwa pesa kwa ajili ya kuvuna mawe humo, na ikiwa mawe yatakuwa hayafai tutabadilisha bei (makubaliano ya mwanzo ya pesa) iwe asilimia. Je bei (biashara) hii ni sahihi au batili kwasababu ni mkataba ndani ya mkataba? Nataraji majibu kwa haraka.

Jawabu:

Waalaykum Salaam Warahmatullah Wabarakaatuh,

Ndugu yangu, kuingiza mkataba ndani ya mkataba kwa namna ya kuwa ni sharti lake huo mkataba basi haijuzu. Kwasababu wewe hapa unasema kuwa mkataba wa mwanzo ni kukodi ambao umeekewa sharti kuwa ikiwa mawe hayafai basi mkataba utakuwa ni bei kwa asilimia… Na kwa kuwa hili haliko wazi katika swali lako kwasababu hukubainisha wazi kilichokusudiwa katika neno asilimia… Isipokuwa maana yenye nguvu hapa ni kuwa (umekusudia) utakuwa mkataba mwengine, yaani sio mkataba kukodi wa mwazo bali utabadilika na kuwa mkataba mwengine… Na kwa kutegemea juu ya maana hii yenye nguvu, hakika hadithi za Mtume (SAW) ambazo zinakataza bei mbili ndani ya moja na mikataba miwili ndani ya mmoja zinafanya kazi hapa:

-Ametoa Tirmidhi katika Sunan yake kutoka kwa Abu Salama kutoka kwa Abuu Huraira amesema: “Amekataza Mtume (SAW) bei mbili ndani ya bei moja”. Abuu Issa amesema hadithi ya Abu Huraira ni nzuri ( hasan ) na ni sahihi.

-Ametoa Ahmad katika Musnad wake kutoka kwa Abdurahman bin Abdillah bin Mas-ud (RA) kutoka kwa baba yake amesema: “Amekataza Mtume (SAW) mikataba miwili ndani ya mkataba mmoja

Yameelezwa yafuatayo katika Shakhsiyyah ya pili; Mlango wa bei kwa malipo ya kidogo kidogo:

(…Lililopo hapa, hakika lau muuzaji na mnunuzi mmoja atasema kumwambia mwengine nakuuzia nyumba yangu kwa elfu kwa sharti uniuzie yako kwa elfu na akasema nimekubali, basi hakika mkataba huu mmoja uliofikiwa kwa bei (mikataba) miwili haujuzu. Kwasababu Mtume (SAW) amekataza bei mbili ndani ya bei moja, na amekataza pia mikataba miwili ndani ya mmoja…)

Kwahiyo mkataba huu haufai, na kama nilvyotangulia kusema kwamba jawabu hili ni kwa kutegemea kukipa nguvu kilichokusudiwa katika neno asilimia, kwasababu neno hili lina maanisha mkataba mpya na sio mkataba wa kukodi bali ni mkataba wa bei ya mawe kwa asilimia. Na kwa maneno mengine unauhamisha mkataba wa kukodi kwa fedha maalumu kwenda kwenye mkataba wa bei ya mawe yatakayopatikana kwa asilimia…Ama ikiwa kilichokusudiwa sicho hicho basi lirejee tena swali lako kwa sura ya wazi, Allah Yuko pamoja nawe.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashta

Maoni hayajaruhusiwa.