Mlipuko wa Beirut Unafichua Kina cha Ufisadi ndani ya Vyombo vya Dola

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(Imetafsiriwa)

Mlipuko mkubwa uliutikisa mji mkuu wa Beirut mchana huu, na baadaye ikadhirika kwamba ulikuwa ni mlipuko katika bandari ya Beirut, katika mojawapo ya mabohari yake, na ilisemekana kuwa ni bohari la 12…

Watu waliona katika video zilizo peperushwa ukubwa na uzito wa mlipuko huo, ambao ulijitokeza kwa umbo la wimbi mkubwa sana la mlipuko, ambao uliathiri jiji zima la Beirut kiasi ya kuwa sauti ya mlipuko ilifika kwa uchache kilomita 40 pambizoni mwa mji huu, na athari yake pia ilihisiwa na nchi jirani kama Cyprus… Watu wengi wa Beirut walidhani kuwa tetemeko la ardhi limeukumba mji mkuu huu, iliyopelekea watu wengi kutamka Shahada, wakidhani kuwa wako katika muda wa mwisho wa uhai wao!

Matokeo rasmi mpaka kufikia wakati wa kuandika taarifa hii, kwa mujibu wa Waziri wa Afya, yamefikia vifo vya watu 73 na majeruhi 4,000, yanayo tarajiwa kuongezeka. Baraza Kuu la Ulinzi liliitangaza Beirut kuwa eneo la janga.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon, huku tukimuomba Mwenyezi Mungu usalama na ulinzi kwa watu wa Lebanon, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awarehemu majeruhi, jambo hili ni kubwa sana kiasi ya kuwa matukio haya mabaya katika sehemu kubwa ambayo hayaelezeki, yamewatoa machozi wanahabari na watazamaji wengi…

Jambo la yakini na la kihakika kufikia hapa ni uwepo wa bidhaa zenye uwezo mkubwa wa kulipuka ndani ya mabohari haya! Iwe ni silaha za chama cha Iran zilizo lengwa na ndege za Kiyahudi, au iwe ni idadi kubwa ya vilipuzi hatari vilivyo hifadhiwa ndani ya bandari hii yote ni bure, katika hali zote hizi, swali msingi ni: vipi itaruhusiwa kwa vilipuzi hatari, bila ya kuzingatia zilikuwa ni silaha au bidhaa nyengine, kuwepo ndani ya bandari iliyo mkabala na jiji ambalo linachukuliwa kuwa ndio mshipa muhimu wa nchi, na katikati ya maeneo ya makaazi yaliyo na watu wengi, vipi, enyi wafisadi?!!

Mlipuko huu unafichua kina cha ufisadi ndani ya vyombo vya dola, ufisadi ambao umefikia nukta ya kuuweka mji mkuu katika volcano ya mlipuko bila ya uwajibikaji wala udhibiti, ima iwe ni silaha au bidhaa zenye uwezo mkubwa wa kulipuka.

Kana kwamba haitoshi kwa watu kupoteza usalama wao wa kisiasa nchini, na kisha usalama wao wa afya, hatari hii imekuwa ndio uhalisia wa usalama wa maisha yao na maisha ya watoto wao na familia zao, bila ya serikali hii na serikali zilizo tangulia kufanya lolote kuwafanya watu kuwa salama, au kufanya chochote kivitendo kumhisabu kila mfisadi ndani ya mamlaka hii, waliozifanya huduma za nchi hii, hususan bandari, kuwa shimo la ufisadi; ufisadi ambao umeathiri maisha ya watu katika nyanja zake zote, hata wakiwa wamekaa majumbani mwao… Na watu hawa wafisadi wangali wamekwamia mamlaka na utawala… lakini mpaka lini?!

Ama tabaka fisadi la wanasiasa nchini Lebanon, ambao wamezinyamazisha ndimi za wale wanaowajibika kwa masaa dhidi ya taarifa yoyote!!! Ingawa wao ni wafalme wa matamko na ufagiliaji, kwa tabaka hili, na yeyote anayewaunga mkono, kuwapa nguvu, au kupewa nguvu nao, tunawaabia maneno ya Mtume (saw):

«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ»

“Ewe Mwenyezi Mungu! Yeyote anayetawalishwa jambo lolote la Ummah wangu kisha akawadhikisha basi nawe mdhikishe, na yeyote anayetawalishwa jambo lolote la Ummah wangu akawa mpole kwao basi nawe kuwa mpole kwake.” [Muslim]

Ukweli mchungu ni kuwa Lebanon, kama zilivyo nchi zote za Waislamu, inaishi katika hali ya utovu wa usalama wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, pengine haujawahi kuonekapo katika historia… Hivyo basi, watu leo wanalinganiwa, hususan watu wenye kumiliki nguvu na ushawishi, kukomesha serikali na tawala hizi, kwani nyoyo zimefika kooni, na hakuna suluhisho bora la kashfa kama hizi, isipokuwa kuzing’oa kwa mizizi yake, la sivyo mpito kutoka janga moja hadi jengine hautakuwa na mwisho, na haijulikani maafa mengine yatakuja kwa hali gani mikononi mwa wafisadi hawa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Maoni hayajaruhusiwa.