Makafiri Wanakiri Nguvu ya Waislamu ni Khilafah

Mnamo siku ya Jumatatu tarehe 3 Machi 1924, ulimwengu ulipambazukiwa kwa taarifa kwamba Mustafa Kemal ndani ya Uturuki ameshaivunja rasmi dola ya Khilafah.
Usiku wake Khalifah wa mwisho Abdul- Abdul-Mejid II, akafungiwa virago vyake, kusekwa ndani ya gari akiwa na mkoba wa mkononi na vijipesa akafukuziliwa mbali ndani ya Uturuki, na kwa udhati hakurejea tena.
Uhuru wa Uturuki rasmi ukatambuliwa kufuatia utekelezaji wa Mkataba wa
 Lausanne uliowekwa saini tarehe 24 Julai 1923, mwaka mmoja nyuma. 
Uingereza na washirika wake wakaondoa majeshi yao yaliyokuwa yakishikilia Uturuki tangu mwishoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia.
Kufuatia qadhia hii, kuliibuka upinzani mkubwa ndani ya Bunge la Uingereza dhidi ya Waziri wao wa Mambo ya Nje, Lord Curzon kufuatia hatu ya kuutambua uhuru wa Uturuki.

Ndipo (Waziri ) Lord Curzon alipojibu ndani ya Bunge hilo: 
“(Jamani msiwe na wasi wasi) Udhati wa mambo ni kuwa Uturuki imeshakufa, na haitohuwika milele, kwa sababu tumeshaangamiza roho ya nguvu yake, nayo ni Khilafah na Uislamu ”
#3machisikuyahuzuni

Maoni hayajaruhusiwa.