Mafunzo Kutoka Vita Vya Ahzab (Shawwal 5AH)

8

Risala Ya Wiki No. 12

Shawwal 1439 Hijri
Julai 2018 Miladi

Vita vya Ahzab vilitokezea mwezi wa Shawwal (Mfungo Mosi) mwaka wa 5AH. Tamko ‘Ahzab’ lina maana ya makundi na vinajuilikanwa kama vita vya makundi kutokana na kukusanyika na kujumuika kwa pamoja makafiri wa kiyahudi, maquraish na makabila kadhaa ya kiarabu dhidi ya Dola tukufu ya Kiislamu Madina.

Mayahudi ndio waliochochea na kuyakusanya makabila ya kiarabu dhidi ya Mtume SAAW. Mayahudi wa Banu Nadhiir baada ya kufukuzwa ndani ya Madina kutokana na khiyana yao ikiwemo jaribio lao la kumuuwa Mtume SAAW walizidi kuwachukia Waislamu na kuandaa mikakati ya kuisambaratisha nguvu ya Dola ya Kiislamu. Ujumbe rasmi wa Banu Nadhir ulikwenda kukutana na Maquraishi na kuwataka washirikiane pamoja kuuzima Uislamu, kadhalika wakayatumia ujumbe kama huo makabila mengine ya kiarabu kwa dhamira ya kuunda jeshi la pamoja dhidi ya Dola ya kiislamu. Hatimae ushirikiano huu uliowakusanya pamoja na kuwajumuisha na kuunda jeshi kubwa la pamoja la Mayahudi,Maqureish, Banu Ghatfan, Banu Muraa, Banu Fazara,Banu Ashja, Bani Sulaim, Banu Sa’d, Banu Asad, pamoja na vikabila vyengine vidogovidogo vya kiarabu.
Jeshi la makafiri lilikaribia askari 10,000 likiongozwa na Abu Sufian bin Harb likashika njia kuelekea Madina.

Mtume S.AA.W baada ya kupata taarifa ya jeshi hilo aliwakusanya masahaba na kuwataka ushauri wa mbinu muafaka ya kivita itumike na hatimae ushauri wa Salman Fursy R.A. ulikubalika ambapo alishauri kutumia mbinu ya kuchimbwa handaki maeneo ambayo hayakuwa na kizuizi cha kuingia ndani ya mji wa Madina ili liwe kama ngome baina yao na makafiri na kizuizi cha kuingia ndani ya mji. Mtume SAAW binafsi alishiriki kikamilifu na masahaba zake kwa siku kadhaa kufanikisha mbinu hiyo ya uchimbaji wa handaki hilo.

Wakiwa kama binadamu baadhi ya Waislamu walikumbwa na khofu na kutetereka kutokana na ukubwa wa jeshi la makafiri, lakini katika kipindi kama hiki Mtume S.AA.W si tu aliwamakinisha Waislamu huku akiwa ndani ya handaki, bali pia aliwabashiria masahaba kutimia kwa ajenda ya Uislamu ya kutawala na kuuweka ulimwengu chini ya Dola ya kiadilifu ya Kiislamu. Katika kuchimba handaki hilo alisikika Mtume SAAW akisema:
‘Allahu Akbar nimepewa funguo za Sham. Naapa kwa Allah hivi sasa nayaona makasri yake mekundu. Allahu Akbar nimepewa Fursi (Persia). Naapa kwa Allah hivi sasa nayaona makasri ya Madain yaliyo meupe. Allahu Akbar nimepewa funguo za Yaman. Naapa kwa Allah ninaangalia milango ya Swanaa sehemu hii niliposimama’.

Bishara hizi zilikuwa ni matumaini makubwa kwa Waumini na kuchukuliwa kama vichekesho na viroja kwa makafiri na wanafiki na huku wakiambizana.
‘Muhammad anatuahidi kupata hazina za Kisra na Kaisar ilhali yakuwa hakuna anaejiaminisha nafsi yake hata kwenda haja’.
Mtume S.AAW pamoja na masahaba wake 3000 walitoka kulilinda handaki ili makafiri wasipate fursa ya kulivuka. Jeshi la makafiri lilishangazwa na mbinu hii mpya katika Bara Arabu na kuamua kulizingira. Mayahudi wa Banu Nadhiir walipeleka ujumbe kwa mayahudi wenzao wa Banu Quraidha ambao bado walikuwa chini ya mkataba wa amani na Dola ya Kiislamu ili wafanye khiyana/ usaliti dhidi ya Waislamu kwa kuwataka kuungana na jeshi la Ahzab, na wakaitika mwito huo.

Kwa hivyo, hatari kubwa ikawakabili Waislamu. Makafiri waliendelea kuidhiki Madina kwa kuizingira huku wakitafuta nafasi ya kuivamia kati kati, hadi pale Muislamu mpya aliesilimu punde bwana Naim bin Mas’uud RA. alipofanikiwa kwa mbinu ya kuwagombanisha makafiri baina yao, na Allah Taala akatia khofu nyoyoni mwao na kuibuka mazingira ya kutoaminiana na kuanza kuzozana. Zaidi ya hayo Allah Taala aliwapelekea mvua kubwa, radi na upepo mkali uliosambaratisha makambi yao na usiku huo huo wa dhoruba hiyo wakatawanyika na majeshi yao yakarejea makwao kwa aibu na fedheha.

Miongoni mwa mafunzo muhimu katika vita hivi ni Ummah wa kiislamu kuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali ama katika ulinganizi, au katika mambo mengine yote mara Khilafah itakaposimama Inshaallah, kama alivyotuonesha Salman Fursi RA. na Naim bin Mas’uud RA. Lakini pia fundisho jengine tusikate tamaa na Nusra ya Allah Taala hata katika mazingira magumu kiasi gani

‘Na bila shaka neno letu limekwishatangulia kwa waja wetu waliopewa utume.Yakuwa wao ndio watakaonusuriwa na kuwa jeshi letu ndilo litakaloshinda’

(TMQ 37:171-173)

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania

24 Shawwal 1439 Hijri | 08-07-2018 Miladi

https://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

8 Comments
  1. Good post! We will be linking to this particularly great post on our site. Keep up the great writing

  2. Live TV says

    I really like reading through a post that can make men and women think.<a href="https://www.toolbarqueries.google.lt/url?sa=t

  3. live racing dubai says

    I think the admin of this site is really working hard for his website since here every stuff is quality based data.-vox gratis streamen

  4. crazy hot deals says
  5. boys hey dude shoes says

    I really like reading through a post that can make men and women think. – girls hey dudes

  6. Great post Thank you. look forward to the continuation.

  7. read review says

    The information you shared is very valuable, thank you for sharing! you could check here

  8. Colette_S says

    I like this blog very much, Its a very nice place to read and find info.Blog range

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.