Kuritadi Kwa Kafiri Kutoka Katika Dini Yake

 بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh Sheikh mwenye heshima. Hakika mimi si mweledi wa lugha ya Kiarabu, lakini nina swali:

Nini hukmu katika Dola ya Kiislamu, kwa mfano, mkristo katika watu wa dhima (ahlu dhimma) akitoka katika dini yake kwenda katika dini ya uyahudi au kinyume chake? Huyu haitwi murtadi, lakini je ana hukmu ya murtadi na je hakubaliwi isipokuwa Uislamu? 

Jawabu:

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh,

Hakika swali lako liko wazi, na Allah akupe baraka kwa kufanya bidii ya kuandika swali kwa lugha ya kiarabu.

Na jawabu la swali lako ni kama ifuatavyo:

Nyuma limeshatangulia kutoka jawabu katika mas-ala ya kwamba hadithi: «مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ»

“Mwenye kubali dini yake muueni” hufanya kazi kwa Muislamu tu, ambae ameritadi akatoka katika Uislamu na haifanyi kazi kwa kafiri ambae ataacha dini yake na kwenda katika dini nyengine ya ukafiri… Na kwa kuzidisha maelezo ya jawabu nasema haya yafuatayo, na Allah ndie Mwenye kuwafikisha:

1-Murtadi kisheria ni “mwenye kuacha dini ya Uislamu”. Amesema Allah Mtukufu:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَنْ يَرْتَدَّ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ذَلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ﴾

“Enyi ambao mumeamini, mwenye kuritadi kati yenu akatoka katika dini yake, basi punde hivi Allah ataleta watu anaowapenda na wao wanampenda, wapole kwa waumini, wakali kwa makafiri. Wanapigana jihadi katika njia ya Allah na wala hawahofu lawama za mwenye kulaumu. Hizo ni fadhila za Allah humpa amtakae. Na Allah ni Mwenye wasaa na Mjuzi” .

Na akasema Allah Mtukufu:

﴿وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَنْ دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا وَمَنْ يَرْتَدِدْ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾،

“Hawataacha kukupigeni vita mpaka wakutoeni kutoka katika dini yenu ikiwa wataweza, na mwenye kutoka katika dini yake miongoni mwenu, na akafa hali ya kuwa ni kafiri, basi hao amali zimeporomoka duniani na akhera. Na hao ni watu wa motoni wataishi humo milele

Kwahiyo, neno murtadi ni maalumu kwa mtu muislamu ambae ameuacha Uislamu akenda kwenye dini nyengine.

2-Ama yule anaeacha dini yake ambae si Muislamu akaenda kwenye dini nyengine au akaenda kwenye upagani (hana dini), huyu mafuqahaa humuita kwa neno “Mwenye kuhama”… Imeelezwa katika kitabu chenye mambo mengi (encyclopedia)  cha kifiqhi cha Kuwait: (…Na uhusiano kati ya mwenye kuhama – almuntaqil – na murtadi ni kuwa kila mmoja kati yao katoka katika dini yake, isipokuwa murtadi ametoka katika dini ya haki na kwenda batili, na mwenye kuhama ametoka katika batili kwenda kwenye batili)

3-Hukmu ya murtadi kwa maana hii, ni yule aliyeacha dini ya Uislamu kwenda kwenye ukafiri. Huyu huuliwa baada ya kutakiwa na mtawala atubu. Na zimepokelewa kuhusu kuuliwa kwake huyu hadithi kadhaa, zilizowazi na zenye kubainisha, kati ya hizo:

-Amepokea Albukhari kutoka kwa Ikrima kutoka kwa Ibn Abass kwamba Mtume (SAW) amesema:

«مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ».

“Mwenye kubadili dini yake muueni”

-Amepokea Albukhari kutoka kwa Abdillah amesema: kasema Mtume (SAW):

«لَا يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَّا بِإِحْدَى ثَلَاثٍ النَّفْسُ بِالنَّفْسِ وَالثَّيِّبُ الزَّانِي وَالْمَارِقُ مِنْ الدِّينِ التَّارِكُ لِلْجَمَاعَةِ»،

“Si halali damu ya mtu Muislamu isipokuwa kwa mambo matatu, nafsi kwa nafsi, na mzinifu aliyehifadhika, na aliyetoka katika dini (ya Uislamu) ambae ameacha jamaa’a”.

Na katika mapokezi ya Muslim ya hadithi hii:

«لَا يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَّا بِإِحْدَى ثَلَاثٍ الثَّيِّبُ الزَّانِي وَالنَّفْسُ بِالنَّفْسِ وَالتَّارِكُ لِدِينِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَمَاعَةِ».

“Si halali damu ya mtu Muislamu anaeshuhudia ya kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa ila Allah na kuwa mimi ni Mjumbe wa Allah isipokuwa kwa moja kati ya matatu, mzinifu aliyehifadhika, na nafsi kwa nafsi, na mwenye kuacha dini yake ambae mwenye kuachana na jamaa’a”.

4-Hadithi zilizotajwa katika kipengee cha (3) hazifanyi kazi kwa mwenye kuhama (almuntaqil) kutoka katika dini ya ukafiri kuelekea kwenye dini nyengine ya ukafiri au kwenye upagani… Hadithi ya Mtume (SAW):

«مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ»،

 Mwenye kubadili yake muueni”, aliyekusudiwa hapa si mwenye kubadili dini yoyote tu, bali aliyekusudiwa hapa ni mwenye kubadili dini ya Uislamu akatoka akaenda kwenye dini nyengine. Na yanatiliwa nguvu haya na:

-Kauli ya Mtume (SAW) aliyoipokea Bukhar:

«وَالْمَارِقُ مِنْ الدِّينِ التَّارِكُ لِلْجَمَاعَةِ»

Na aliyetoka katika dini (ya Uislamu) ambae ameacha jamaa’a” . Na kauli yake aliyoipokea Muslim:

«وَالتَّارِكُ لِدِينِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَمَاعَةِ»

Na mwenye kuacha dini yake ambae mwenye kuachana na jamaa’a”. Na mwenye kuacha jamaa’a  ni mwenye kuacha jamaa’a ya Waislamu, yaani ni Muislamu aliyetoka katika dini ya Uislamu.

-Amepokea Tabarani katika kitabu cha Al-Kabiir  kutoka kwa Bahzi bin Hakiim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake amesema: kasema Mtume (SAW):

«مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ، لا يَقْبَلُ اللَّهُ تَوْبَةَ عَبْدٍ كَفَرَ بَعْدَ إِسْلامِهِ»

Mwenye kubadili dini yake muueni, Allah hakubali toba ya mja aliyekafiri baada ya Uislamu wake”.

Na Haithami kasema kuhusu hadithi hii: Watu wake ni waaminifu, na katika riwaya hii mwisho wa hadithi unatafsiri mwanzo wake, yaani mwenye kubadili dini yake ni yule mwenye kukufuru baada ya Uislamu wake.

-Na Tabarani amepokea katika kitabu cha Al-Kabiir kutoka kwa Muadh bin Jabal, kwamba Mtume (SAW) alimuambia wakati alipompeleka Yemen:

«أَيُّمَا رَجُلٍ ارْتَدَّ عَنِ الإِسْلامِ فَادْعُهُ، فَإِنْ تَابَ، فَاقْبَلْ مِنْهُ، وَإِنْ لَمْ يَتُبْ، فَاضْرِبْ عُنُقَهُ…»،

“Mtu yeyote aliyeritadi akatoka katika Uislamu basi mlinganie, akitubu mkubali, akiwa hajatubu mpige (mkate) shingo yake…”. Na kataja Ibn Hajar katika kitabu cha Fat-hul Baarii hadithi ya Muadh akasema: (Imetokezea katika hadithi ya Muadh kwamba wakati Mtume (SAW) alipompeleka Yemen alimwambia:

«أَيُّمَا رَجُلٍ ارْتَدَّ عَنِ الْإِسْلَامِ فَادْعُهُ فَإِنْ عَادَ وَإِلَّا فَاضْرِبْ عُنُقَهُ وَأَيُّمَا امْرَأَةٍ ارْتَدَّتْ عَنِ الْإِسْلَامِ فَادْعُهَا فَإِنْ عَادَتْ وَإِلَّا فَاضْرِبْ عُنُقَهَا»

“Mtu yeyote aliyeritadi akatoka katika Uislamu mlinganie, akirejea sawa, na kama hakurejea mpige shingo yake (muue). Na mwanamke yeyote aliyeritadi akatoka katika Uislamu mlinganie, akirejea sawa, na kama hakurejea mpige shingo yake – muue”. Na sanadi yake ni nzuri – hasan.  Na wazi katika hadithi kuwa maneno yanamuhusu Muislamu aliyeritadi akatoka katika dini Uislamu.

5-Kwa hiyo, hukmu za kuritadi kutoka katika Uislamu hazifanyi kazi kwa mwenye kuhama (al-muntaqil)  kutoka katika dini ya ukafiri kwenda katika dini nyengine ya ukafiri au kwenda kwenye upagani. Hivyo basi, haadhibiwi mwenye kuhama kutoka katika uyahudi  kwenda kwenye ukristo au kwenye dini nyegine ya ukafiri kwa huko kuhama kwake kutoka ukafiri kwenda kwenye ukafiri … Na vilevile, hatenzwi nguvu kuukumbatia Uislamu isipokuwa asilimu kwa khiyari yake… Pamoja na angalizo, kwamba mwenye kuhama katika waliopewa kitabu (ahlul-kitaab): mayahudi na wakristo, akahama kutoka katika dini yake na kwenda kwenye dini isiyokuwa uyahudi au ukristo, kama vile akahama kuelekea kwenye umajusi, au kaacha dini na kwenda kwenye upagani, hakika yake katika hali haifai kwa Waislamu kula kichinjwa chake. Na akiwa mwenye kuhama katika waliopewa kitabu (Ahlul-kitaab) kwenda katika dini nyengine ya ukafiri isiyokuwa ya waliopewa kitabu, atakapokuwa mwanamke mtu huyu, basi haifai kwa Muislamu kumuoa… Hilo ni kwa sababu, wale inaofaa kula vichinjwa vyao na kuoa wanawake wao ambao si katika Waislamu ni waliopewa kitabu (ahlul-kitaab) mayahudi na wakristo tu. Na muda wa kwamba mtu amehama kutoka katika uyahudi au ukristo kwenda kwenye dini zisizokuwa hizo katika dini za kikafiri, basi huyo anatoka katika duara la yule anaefaa kuliwa vichinjwa vyao na kuoa wanawake wao. Kasema Allah Mtukufu:

﴿الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ﴾.

“Leo mumehalalishiwa kwa ajili yenu vizuri, na vyakula vya wale waliopewa kitabu halali kwenu, na vyakula vyenu halali kwao, na wanawake waliojihifadhi katika waumini na wanawake waliojihifadhi katika wale waliopewa kitabu kabla yenu (pia ni halali kwenu) pindi mukiwapa mahari yao, mukafunga nao ndoa bila ya kufanya uzinzi wala kuwaweka kinyumba”  (Maida:5)

6-Hakika ya rai ambayo tunayoipa nguvu katika mas-ala haya kuhusu mwenye kuhama kwa maana iliyobainishwa  ni hiyo tuliyoieleza hapo juu. Na ziko rai nyengine za mafuqahaa katika mas-ala haya, unaweza ukayarejea katika vitabu vya fiqhi… Lakini kama nilivyotaja punde tu, kwamba rai tunayoitia nguvu kuhusu mwenye kuhama ni hiyo tuliyoieleza hapo juu kwa mujibu wa dalili ambazo tumezibainisha. Natarji mas-ala haya yatakuwa yamekaa wazi.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashtah

15 Ramadhani 1440 H

20/05/2019

Maoni hayajaruhusiwa.