Kiboko ya Marekani ni KHILAFAH sio Mahakama ya ICC

Jumatatu, 11 Septemba 2018; kwa mara ya kwanza ulimwengu ulishuhudia hotuba ya Mshauri Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Marekani -John Bolton alitangaza “Leo, tukiadhimisha tukio la Septemba 11, nataka kutoa ujumbe uliowazi kabisa kwa niaba ya raisi. Marekani itatumia kila njia ndani ya uwezo wake ili kuwalinda raia wetu na wale wa washirika wetu kutokana na mashtaka ya dhulma kutoka kwa Mahakama hii haramu. Hatutoshirikiana na Mahakama ya Uhalifu Ulimwenguni (ICC). Hatutoipatia msaada wowote ICC… Tutaiwacha ife yenyewe. Hata hivyo kwa kila dhamira na malengo, tayari ICC imekufa kimtizamo wetu. Marekani itawapiga marufuku na kuwafungulia mashtaka mahakimu na viongozi wa mashtaka wa Mahakama ya ICC, itaziwekea vikwazo fedha zao ambazo ziko katika mzunguko wa fedha nchini Marekani na pia kampuni au nchi yoyote itakayoshirikiana na Mahakama ya ICC katika uchunguzi wa Amerika. Kwa mpangilio wa Urasilimali, hatutambui mamlaka yoyote ya juu isipokuwa katiba ya Marekani. Raisi huyu hatoruhusu raia wa Marekani kushtakiwa na maafisa wa ng’ambo, na hatoruhusu mataifa mengine kutuamulia namna ya kujitetea.

Matamshi hayo makali yametokana na matukio yafuatayo:

Kwanza: Kiongozi wa Mashtaka wa ICC alitoa ombi mwaka jana 2017 ili kufanyike uchunguzi kutokana na madai ya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan, ambao ungejumuisha chochote kilichofanywa na jeshi la Amerika na maafisa wao wa kijasusi. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya ICC ya 2016 iliyosema kuna msingi wa uwezekano kuwa jeshi la Marekani lilifanya unyama katika vituo vya siri vya kudhibiti watu ndani ya Afghanistan vikiendeshwa na CIA, na kwamba serikali ya Afghan na Taliban walifanya uhalifu wa kivita. [bbc.com, 11/09/2018]

Pili: Mnamo Mei 2018, Palestina (PLO) kupitia Waziri wa Kigeni Riad Malki alikutana na Kiongozi wa Mashtaka wa ICC na kuiomba rasmi Mahakama hiyo ifungue uchunguzi kamili juu ya madai ya uhalifu uliofanywa na umbile la Kiyahudi la Israel ndani ya Eneo la Jerusalem Mashariki, West Bank na Gaza kuanzia Juni 2014. [bbc.co.uk, 22/05/2018] Hili limepelekea Ubalozi wa PLO Marekani kufungwa.

Kauli hiyo imedhihirisha nukta zifuatazo:

  1. a) Mahakama ya ICC ni chombo cha wa Magharibi hususan Umoja wa Ulaya (EU) ambao ni wanachama na wadhamini wakuu wa Mahakama hiyo ikiongozwa na Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na Canada. Hivyo basi ukali na upole wa makucha yake daima unategemea maslahi ya wadhamini wake. Mfano Walioshiriki Vita vya Kuivamia IRAQ ni Marekani na Uingereza lakini hatukusikia Mahakama ya ICC imefungua uchunguzi na kuwachukulia hatua wanajeshi wa Uingereza! Pia Nchini Ujerumani, Uingereza, Canada, Ufaransa, Kenya n.k kumetungwa sheria za kidhalimu za kupambana na Uislamu (Misimamo Mikali na Ugaidi) ambazo zimepelekea watu wengi kuuawa na kupotezwa hadi wa leo hawajulikani walipo. Mahakama hiyo iko kimya. Hivi sasa Waislamu wanauawa na Umbile la Kiyahudi huko Palestina na ilhali Syria nako Urusi inawaua kwa mabomu na ambaye pia ni mwanachama wa Mahakama hiyo iko kimya wala haimfungulii mashtaka!
  2. b) Marekani haiko tayari kupangiwa na kuhesabiwa na EU. Imejaa jeuri na kudhihirisha uadui wa wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hili liko wazi kutokana na vitendo vyake ikiwemo pamoja na vita vyake dhidi ya Misimamo Mikali na Ugaidi ambavyo vimeelekezewa Uislamu na Waislamu ulimwenguni popote walipo. Na kattu Marekani haitaki kuhesabiwa na taasisi yoyote (ICC, Makampuni au Serikali) kuhusiana na uhalifu wanaoufanya ulimwenguni. Hususan tukizingatia wakati huu ambapo Marekani imo vitani kiuchumi dhidi ya EU na inatafuta kila aina ya vijisababu kuishughulisha EU na kuisukuma ijisalimu katika mikataba yake na sera zake za kiulimwengu zilizofungamanishwa na mwito wa “Marekani Kwanza.”

Kiboko ya Marekani na washirika wake ni Dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume. Kiongozi wake akiwa Khalifah aliyefungwa na Sheria ya Kiislamu inayotokamana na Qur’an na Sunnah katika kusimamia mambo ya raia wake na Uislamu ulimwenguni. Khilafah itaitizama Marekani na washirika wake ikiwemo umbile la Kiyahudi kama nchi adui kwake kutokana na dhulma dhidi ya Waislamu na Uislamu. Hivyo basi kuichangamkia Marekani kama ilivyoichangamkia mwaka 1783 pale ambapo Marekani ilijitosa katika ulingo wa kimataifa kupitia manuari zake kuelea bahari ya kimataifa na kutiwa mkononi na jeshi la majini la Khilafah karibu na Algeria. Mwaka 1793 manuari 12 zaidi za Marekani zikashikwa tena. Nakupelekea mnamo Machi 1794 Bunge la Marekani (Congress) kumuidhinisha Raisi Washington kutumia sarafu za dhahabu 700,000 kujenga manuari madhubuti itakayoweza kuhimili mashambulizi ya manuari za Khilafah. Mwaka mmoja baadaye Marekani ilisalimu amri na kutia saini Mkataba wa Barbary kati yake na Khilafah. Neno Barbary likimaanisha kuwa Wilaya ya Afrika Kaskazini ikijumuisha Algiers, Tunis na Tripoli zilizokuwa chini ya Khilafah ya Uthman.

Masharti ya Mkataba wa Barbary yalikuwa ifuatavyo:

  1. Mkataba huo utaigharimu Marekani kulipa kwa wakati mmoja kima cha dola 992,463.
  2. Meli za Marekani zilizoshikwa zitarudishwa na Manuari ya Marekani itaruhusiwa kuelea katika bahari ya Atlantiki na Mediteranean.
  3. Ili kuruhusiwa Nukta ya 2, Marekani ilipe dola 642,000 kwa thamani ya dhahabu.
  4. Marekani itakuwa ikilipa kodi ya kila mwaka ya dola 12,000 kwa thamani ya dhahabu kwa kutumia kalenda ya Kiislamu ya Hijria
  5. Marekani ilipe dola 585,000 ili kuwakomboa wanajeshi wa Marekani walioshikwa.
  6. Marekani kuunda meli ya chuma ya kisasa nchini Marekani kwa gharama zake ikishakamilika waikabidhi Khilafah kama uhuru wao Marekani. (Gharama za meli hiyo baada ya kuisha iligundulika kuwa iliwagharimu Marekani mara 30 zaidi kinyume na makadirio yao ya awali)

Huu ulikuwa mkataba ulioandikwa kwa lugha rasmi ya Khilafah wakati huo ikiwa ni Kituruki na kutiwa saini na Raisi Washington wa Marekani. Na hivyo kuingia katika historia kuwa mkataba halali wa kwanza kuwahi kufungwa kwa lugha ya kigeni na wa pekee kwa Marekani kusaini kuwa wamekubali kulipa kodi ya kila mwaka kwa taifa jengine. Mkataba huu uliendelea mpaka ilipoanguka Dola ya Khilafah.

Hivyo ndivyo Marekani ilivyoshughulikiwa zama hizo na ndivyo itakavyoshughulikiwa punde tu Khilafah itakaposimama tena hivi karibuni kwa Idhini na Uwezo wake Mwenyezi Mungu. Na hapo ndiyo Marekani itajua kuwa Waislamu na Uislamu na wanyonge wote duniani watakuwa wamepata mtetezi wa kweli na mwenye kuhesabu madhalimu kikweli wala sio ICC na mfano wake ikiwemo Umoja wa Mataifa n.k.

#UislamNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.