Mashindano ya Seera ya Mtume S.A.W 1442 Hijria

بسم الله الرحمن الرحيم

Mashindano ya Maisha ya Mtume Rahma na amani ziwe juu yake
Yalifunguliwa na Dua kutoka Kwa Ustadh Juma wa Masjid Rawdha
Mahala: Masjid Raudhwa Lumumba Mwanza .
Tarehe: 29/11/2020
Muda: Yalianza saa mbili kamili asubuhi mpaka Saa saba muda wa Swala ya adhuhuri
Mgeni Rasmi: Sheikh Fadhil Salim ambaye ni Mjumbe wa kamati ya masheikh Bakwata mkoa wa Mwanza (ambaye alikuwa Mwakilishi wa Shekh wa Mkoa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke wa mkoa wa mwanza)
Mashindano: Walikuwapo washiriki wa aina mbili nao ni Wanafunzi wa madrasa kwa viwango vya chini yaani msingi (ibtidai) kwa Madrasa mbali mbali maeneo tofauti tofauti Mkoani mwanza pamoja na wanafunzi wa Mahad yaani viwango vya secondary na kuendelea (Mutawasita, Thanawi)
Waliwasilisha mada kuhusu Maisha ya Kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw)
Nasaha Jaji Mkuu wa Mashindano: Sheikh Issa Nassibu (Mwanachama wa Hizb Ut-Tahrir Tanzania)
Mada: Tupambane na propaganda za kumchafua kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) kwa kumwelezea Maisha yake halisin na kufuata mafunzo yake.
Nasaha Mgeni Rasmi: Sheikh Fadhil Salim (Mjumbe wa Kamati ya Mashekh Bakwata Mwanza akimuwakilisha Shekh wa Mkoa Mwanza)
Mada: Tushikamane na Umoja wa Kiislamu
Zawadi kwa washiriki jumla pamoja na washindi zilitolewa na Mgeni Rasmi.
Kukhitimisha Mashindano kwa Dua kutoka kwa Shekh Amir Zuber wa Masjid Rawdha
Matukio kwa Picha

 

Maoni hayajaruhusiwa.