Bishara za Wazi za Kurejea Khilafah

بسم الله الرحمن الرحيم

Imetimia miaka 100 tangu kuangushwa kwa dola ya Kiislamu ya Khilafah katika mwezi wa Rajab, 1342H. Ulimwengu umeishi sasa ni miaka 100 ukiwa unatawaliwa na kuendeshwa kwa sharia za kikafiri za kibepari, sharia zilizojaa kila aina ya uovu. Hapa tutaangazia kwa kifupi kwa dalili za kisheria na za kimazingira juu ya kurejea tena kwa Khilafah ili Uislamu utawale tena ulimwengu na kuukomboa ulimwengu kutokana na dhiki na mateso iliyopitia katika kipindi hiki cha miaka 100 ya kutokuwepo utawala wa Kiislamu duniani.
1. Ushahidi wa Quran Tukufu:
Allah Taala Anatoa ahadi kuwa atatunusuru Waislamu na kutupatia Khilafah kama alivyowapatia masahaba (Allah awaridhie).
وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya matendo mema kuwa atawafanya makhalifah katika ardhi kama alivyowafanya makahalifah wale waliokuwa kabla yao” (TMQ An Nur: 55)
Pia Allah Taala Anatangaza wazi kwamba makafiri watashindwa hata wakitumia rasilmali zao kwa kiwango gani kupambana na Uislamu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ
“Hakika wale waliokufuru hutoa mali yao ili kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha itakuwa khasara juu yao, kisha watashindwa…” (TMQ Anfal:36)
Na kushindwa makafiri huanzia duniani kwa kudhibitiwa chini ya dola ya Kiislamu, kisha akhera ni kuingizwa motoni milele.
Aidha, Allah Taala anaonesha wazi wazi kwamba suala la kuwanusuru Waislamu ni wajibu Aliyojiwekea Yeye mwenyewe kwa utukufu na nguvu Zake. Anasema Allah (SWT):
وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ (الروم: 47
“…..Na imekuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini” TMQ (Al-Rum: 47)
2. Ushahidi wa Sunnah
Zimekuja Hadith nyingi sahihi zinazoonesha bishara ya kurudi Khilafah kwa Ummah wa Kiislamu, hapa tutaleta baadhi:
Mtume SAAW anasema:
“Hakika Allah amenisogezea dunia yote nikaona kutoka mashariki mpaka magharibi. Na kwa hakika utawala wa Umma wangu utafika sehemu zote nilizosogezewa. Na nimepewa khazina mbili, nyekundu na manjano”. (Muslim)
Pia Ibn Habban katika kitabu chake Sahih Ahadith kutokamana na Al-Nawas Bin Sam’aan, Imam Ahmad katika Musnad na Al-Tabarani katika ‘Al-Kabeer,’ kutokamana na Salamah Bint Nufayl kuwa alisema Mtume:
“Makao makuu (uqr) ya dola ya Kiislamu yatakuwa Al-Shaam (Jordan, Syria, Palestine, Lebanon na Iraq).
Hadith hii inatupa bishara kuwa makao makuu ya dola ya Kiislamu yatakuwa Al-Sham, na hili bado halijawahi kutokea.
Katika Hadithi ya Al-Nu’man Bin Bashir amesimulia kutoka kwa Hudhayfah kuwa Mtume anasema:
“… kisha kutakuwa na (ufalme) wa kimabavu……………. kisha kutakuwa na Khilafah kwa Manhaj (njia) ya Utume.” (Ahmad na Al Tayalsi)
3. Ushahidi wa Kimazingira
Sasa tuangalie hoja za kimazingira ikiwemo kuongezeka idadi yta Waislamu na kutanuka Uislamu kila mahala kama matayarisho ya Khilafah
Leo duniani kuna wimbi kubwa la kuongezeka idadi ya Waislamu,mpaka mwaka 2016 Waislamu walikuwa bilioni 1.8 duniani (Swedish Nomad: Largest Religions in the world. 21/01/2020) na Uislamu ndiyo dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani ikiwa na kasi ya 1.84% (Foreign Policy: The World`s Fastest Growing Religions. 11/02/2020).
Aidha, vita ya Amerika nchini Afghanistan na kwingineko kama Iraq katika biladi za Kiislamu vinatudhihirishia uhalisia kuwa wakoloni mabepari makafiri hawana uwezo wa kupambana na Waislamu. Amerika imegharimika dolari trilioni 2, imepoteza wanajeshi 2400 na 20,000 wakijeruhiwa ikipigana na Wataliban 2000 pekee kwa muda wa miaka 20 (The New York Times: 9/12/2019) na bado hawajafanikiwa kuitawala Afghanistan yote.
Pia raia hususan katika ulimwengu wa Kiislamu kuchoshwa na watawala vibaraka wa makafiri kila siku zinavyosonga mbele, na vibaraka hao wa makafiri kupoteza mvuto kwa Ummah, na hata kutaka kupinduliwa.
Vuguvugu la nchi za Kiarabu “Arab Spring” iliyopelekea kuondoshwa kwa vibaraka wakongwe kama Husni Mubarak wa Misri, Muamar Gaddafi, Ben Ali wa Tunisia ni ushahidi wa wazi kuwa Umma umechoshwa na vibaraka.
Amma kabla ya vuguvugu hili hapo nyuma yametokea matukio mengi yanayoashiria Waislamu wamechoka na Ubepari na vibaraka wake, wanataka kutawaliwa na Uislamu wao na Khalifah muadilifu. Kwa mfano, Waislamu waliandamana kumuunga mkono Usama Bin Laden dhidi ya uvamizi wa Amerika nchini Afghanistani, kuunga mkono kupigwa Kijidola cha Mayahudi na Iraq nk.
Pia vibaraka kukosa kujiamini kama vile Hamid Karzai aling`ang`ania kuendelea kulindwa na vikosi vya Amerika akihofia watu wake, Raisi Musharraf aliamuru barabara zote zisafishwe alipokuwa akisafiri akihofia kushambuliwa. Pia vibaraka hao hata katika mikutano yao kama ya OIC wanalazimika kuwatukana makafiri mabwana zao ili waweze kupata uungwaji mkono wa watu wao. Hii inaonesha wazi kuwa Ummah haupo pamoja nao na kila siku unazidi kusonga mbele licha ya nguvu kubwa wanayotumia makafiri kuharibu taswira hii.
Aidha, kushtadi uadui wa makafiri kwa Uislamu na Waislamu katika kuwatesa, kuwaua, kuwadhulumu, kuvamia ardhi zao yote ni katika khofu na kutapatapa kwao. Makafiri wanaona kuwa Uislamu pekee ndiyo tishio kwa mfumo wao wa Kibepari baada ya kuanguka kwa mfumo wa Ujamaa, hivyo wanatamka wazi na wanaonesha uoga wao kwa Uislamu na kuita Uislamu wa kisiasa” Political Islam” kuwa ni tishio.
Watunga sera wan chi vinara wa ukafiri na viongozi wao wamekuwa waieleza wazi juu khofu yao na utawala wa Kiislamu. Kwa mfano, aliyekuwa raisi wa Marekani George W Bush aliwahi kuhadharisha kuhusu kurejea kwa Khilafah katika hotuba yake kwa Waamerika mnamo Oktoba 2005 aliposema kuwa:
“The militants believe that controlling one country will rally the Muslim masses, enabling them to overthrow all moderate governments in the region, and establish a radical Islamic empire that spans from Spain to Indonesia”
Tafsri:
“Wapiganaji (wa Kiislamu) wanaamini kuwa kudhibiti nchi moja kutachochea Waislamu wengi, kutawawezesha kupindua serikali zenye mrengo wa wastani na kuanzisha dola pana ya Kiislamu ambayo itaenea kutoka Hispania hadi Indonesia”
Kwa ushahidi huo kutoka katika Quran, Sunnah na mazingira ni wazi sasa bila ya tembe ya shaka kuwa kurudi kwa Khilafah ni jambo lipo mbele ya macho yetu. Hata hivyo kuamini bishara hizo ni upande mmoja, na wajibu wetu wa kutenda matendo ni jambo jengine lililo wajibu kwetu. Hivyo, tunatoa wito kwa Waislamu kuungana na Hizb ut Tahrir kufanya kazi ya ulinganizi ili kuziendea bishara na ahadi hizo za Allah Taala na Mtume wake saaw ili tuweze kufuzu duniani na akhera
….Isimamisheni Enyi Waislamu
Said Bitomwa
Risala Maalum ya Rajab – 4
27 Rajab 1442 Hijri
11 Machi 2021 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania
https://hizb.or.tz/
https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.