Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir Mwanachuoni Mkubwa Atta Bin Khalil Abu Rashta kwa Mnasaba wa Kumbukizi ya Miaka Mia Moja ya Kuangushwa Dola ya Khilafah Mwaka 1342 H /1924 M

بسم الله الرحمن الرحيم

Sifa njema anastahiki Allah, na rehema na amani zimfikie Mjumbe wa Allah, familia yake, maswahaba zake na wenye kumfuata. Ama baada ya hayo…

Kwa ummah wa Kiislamu kijumla na hasa kwa wabebaji da’wa; mashababu wa kike na wa kiume ili kurejesha Khiafah Rashida…

Katika masiku kama haya miaka mia moja iliyopita, mwishoni mwa Rajab 1342 H sawa na mwanzo wa Machi 1924 M waliweza makafiri wakoloni kuiua Dola ya Khilafah chini ya uongozi wa Uingereza wakati huo kwa kusaidiana na makhaini wa Kiarabu na Waturuki. Na akatangaza muovu mkubwa wa zama hizi Mustafa Kamal kuifuta Khilafah, kumzingira Khalifah huko Istanbul na kumtoa alfajiri ya siku hiyo. Hayo yalikuwa ni kwa malipo aliyoahidiwa na Uingereza kwa amri aliyopewa ili kumfanya awe rais mdhaifu wa jamhuri ya kisekula ya Uturuki. Hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa, kiasi kwamba kukatokezea mtikisiko mkubwa katika miji ya Waislamu kwa kumalizwa Khilafah chanzo cha utukufu wao na radhi za Mola wao.

Hakika muovu huyo alitangaza ukafiri wa wazi kwa kuifuta Khilafah baada ya kuwa ipo. Na ikawa ni wajibu kwa ummah kupigana nae kwa upanga kama ilivyoelezwa katika hadithi ya Mtume (SAW) waliyo wafikiana Bukharina Muslim, kutoka kwa Ubada bin Swamit (RA): «وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ» “Na kwamba tusipigane na mwenye utawala mpaka muone ukafiri wa wazi ambao muna ushahidi kwa Allah”.Isipokuwa ukatili wake mkubwa katika kumwaga damu ya ummah na hasa wanavyuoni kiasi kwamba aliwaua wengi, miongoni mwao ni sheikh Said Biran (ra) na akawafunga wengu. Haya yote yalikuwa na athari kwa ummah, haukuweza kusimama kumtikisa muovu huyo na wasaidizi wake hata kidogo kumfanya yeye na wasaidizi wake wapate hasara. Bali msimamo ulikuwa ni dhaifu haukufiakumsaga saga haini huyowa Allah, Mtume wake na waumini! Hivi ndivyo alivyo ‘okoka’ mtenda kufuru ya wazi kwa vitendo vyake vikali ili umma usimtupilie mbali!

Baada ya hapo tena ushawishi wa makafiri wakoloni ukatinga katika miji ya Waislamu, wakaigawa miji ya Waislamu, wakairarua hadi kufikia kiasi vipande hamsini na tano. Hayo ni matokeo ya mtikisiko wa kuvunjwa kwa Khilafah. Kisha juu ya mtikisiko huu wakazidisha mtikisiko mwengine, wakawapa mayahudi kijidola katika ardhi tukufu, Isra na Miraj yake Mtume (SAW), wakawapa kwasababu wabakie. Na sababu ya kwanza ilikuwa ni kulinda amani yake kupitia watawala vibaraka waliowazunguka hao mayahudi.Sio hili tu, bali watawala hawa walikuwa wakishindwa na mayahudi kila vita ambavyo visivyoweza kuepukika mpaka wakawapa kijidola cha wayahudi umbile kubwa zaidi na picha ambayo si yake. Hawakutosheka na hilo, wakafanya bidi katika kumpiga vita Allah na Mjumbe wake kwa kuihamisha kadhia kutoka kuliondoa umbo la kiyahudi huko Palestina kutoka mzizi wake wakahamishia kwenye mazungumzo na umbo la kiyahudi kwamba eti huenda wakaachia kidogo ardhi waliyoikalia mwaka 1967!

Kisha baada ya hapo wakaporomoka chini zaidi wakakimbilia utiaji saini na umbo la kiyahudi hata bila hajaachichia chochote katika ardhi!! Baadhi yao walitenda uovu huu wa utiaji saini nyuma ya pazia na baadhi wakatenda uovu huo wazi kweupe! Na baada ya kuongoza watawala wa Misri mbio hizi za udhalili na unyonge zikafuata taasisi na watawala wote wa Jordan, UAE, Bahrain, Sudan na Moroccona watawala wa Kisaudi wakasimama katikati ya njia wanazipungia mkono nchi hizo kwamba hakika wako nyuma yao pamoja na kwamba hawatoachwa nyuma ya msafara…Namna hii, wote wanakimblia katika uovu huu bila ya kujali udhalili uliowagubika kutoka utosini hadi miguuni mwao  ﴾سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ﴿.  “Wale waliotenda uovu watapatwa na udhalili mbele ya Allah na adhabu kali kwa vile walivyofanya vitimbwi”.

Kisha sio Palestina pekee walioichoma mkuki watawala hawa, bali pia waliisalimisha ardhi nyengine tohara katika ardhi za Waislamu, Kashmir wakaiunganisha washirikina wa Kihindu kwenye nchi yao…Urusi ikaichukua Crimea… Sudan ya kusini ikatenganishwa na kaskazini yake…Timor ya mashariki ikachukuliwa kutoka Indonesia… Na Cyprus, unaijua Cyprus?! Ni ngome ya Waislamu kwamiaka kadhaa, na leo eneo lake kubwa linatawaliwa na Greece…Waislamu wa Rohingya wanachinjwa Myanmar “Burma”, na wakikibilia Bangladesh serikali inawaminya vikali na kuwakusanya katika kisiwa cha “Basan Char” ambacho ni kisiwa hatari chenye mafuriko mara kwa mara na ambacho hakifai kwa makazi ya mwanadamu! Kisha Turkistan ya mashariki ambayo China imekuwa ikiikandamiza na kuitendea matendo ya kinyama, bali unyama ukafikia hatua ya kukifanya jela kisiwa hicho kwa watu huru kike kwa kiume, mauaji yakawa makubwa, wazi, si siri, mbele ya macho na masikio ya nchi katika miji ya Waislamu, amabazo zimekaa kimya cha kaburi, na zikizungumza husema ukandamizaji wa China dhidi ya Waislamu ni mambo ya ndani! كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً﴿ “Maneno mabaya yanayotoka katika vinywa vyao hawasemi ila uongo”

Ama nchi nyengine za Waislamu zinatawaliwa na watawala wajinga wanaozunguka pamoja na makafiri wakoloni kokote kule watakako zunguka. Hawahifadhi usalama wa nchi wala hawachungi haki za waja, utajiri wao unaporwa na heshima yao imepokwa, hawawashi wala hawazimi, hawana uzito wowote kwa makafiri wakoloni hasa Marekani. Bali huwaita vibaraka wake kwa yale yanayowazidishia idhalili na unyonge, huwambia: “Lau si sisi musingelibakia hata masiku machache katika viti vyenu vya enzi vya kipumbavu, tulipeni fedha muwezavyo bali zaidi ya uwezo wenu”. Ni kweli anaejidhalilisha inakuwa sahali kudhalilishwa!!

Enyi Waislamu: Hii ndio hali yenu baada ya kuondoka kwa Khilafah kiasi kwamba mataifa yamekuvamieni kutoka kila upande, kwani mulikuaje wakati muko chini ya kivuli cha Khilafah?Mumekuwa nyinyi ni ummah bora ulioletwa kwa ajili ya watu, ni wafuasi wa Muhammada (SAW) mwisho wa Mitume na kiongozi wa mujahidina… Mababu zenu ni Makhalifah waongofu na viongozi wa wafunguzi wa miji …Nyinyi ni vizazi vya aliyenusuru Salahudin aliyewatenza nguvu watu wa msalaba na mfunguzi wa Bait Al-Maqdis kutoka uchafu wao (watu wa msalaba) katika mwezi kama huu wa Rajab 583H…

Nyinyi ni vizazi vya Qutuz na Baibars waliowatenza nguvu Tatar… Nyinyi ni vizazi vya Muhammada Al-Fatih, Amiri kijana ambae alikuwa hata ajavuka umri wa miaka ishirini na tatu alipoifungua Constantinople mwaka 857 H /1453 M, Allah kamkirimu kwa sifa alizotoa Mtume (SAW) katika hadithi aliyoitoa Ahmad kutoka kwa Bishr Al-Khath’amy: «فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ» “Amiri bora ni wa mji huo na jeshi bora ni jeshi hilo”…Nyinyi ni vizazi vya Suleiman Al-Qanun ambae Wafaransa walimuomba msaada wa kuachiwa mateka mfalme wake katika karne ya kumi na sita 1525 M, lakini imesahau au inajitia kusahau kuwa ilimuomba msaada Khalifah wa Waislamu, ikaja kuuvunjia heshima Uislalmu na Mtume wa Uislamu bila ya kufuatiliwa na kuhesabiwa kwasababu ngao ya Uislamu imeondoka… Nyinyi ni vizazi vya Khalifah Salim wa III, ambae katika kipindi chake Marekani ilitoa kodi kila mwaka ili kuruhusiwa marikebu za Kimarekani kupita kwa salama katika bahari ya Atlantiki kuelekea bahari ya Mediterenian bila ya mashambulizi ya baharini yaKhilafah ya Uthmania dhidi ya marikebu za Marekani katika Jimbo la Algeria. Na kwa mara ya kwanza Marekani imelazimishwa kutia saini mkataba si kwa lugha yake bali kwa lugha ya Dola nyengine yaani Dola ya Uthmania katika mwaka 1210 H / 1795 M. Na Marekani hivi sasa inawatawala watawala wa Waislamu huku ikiwaambia lipeni fedha sisi ndio tunaokulindeni…

Nyinyi ni vizazi vya Khalifah Abdul Hamid ambae hakuhadaiwa na mamilioni ya dhahabu waliyomletea Mayahudi kuingia katika hazina ya Dola ili kuwaruhusu waikalie Palestina, na akasema manneo yake maarufu (Hakika kunyofolewa nyofolewa mwili wangu ni jambo jepesi kuliko mimi kuona Palestina imemeguka kutoka Dola ya Khilafah) kisha akaongeza (Mayahudi na wabakie na mamilioni yao …na siku itakaposambaratika Dola ya Khilafah hapo wataweza kuichukua Palestina bila ya fedha yoyote). Haya ndiyo yaliyotokea!…Nyinyi ni vizazi vya wavumbuzi wa saa na wakaitoa moja zawadi kwa Charlemagne ambae mmoja katika wafalme wakubwa wa Ulaya maalum kwa ajili yake. Na viongozi wake wakadhania imejaa majini na maafiriti! Hivi ndivyo tulivyokuwa katika fikra yetu inayong’aa na angafu na wao ndivyowalivyokuwa katika fikra duni ngonjwa!

Hivi ndivyo mlivyokuwa enyi Waislamu mlipokuwa chini ya kivuli cha Khilafah, na hivi ndivyo mulivyo fikia kivuli cha Khilafah kilipo ondoka. Basi zingatieni enyi wenye uoni…

Mwisho naelekea kwenu enyi watu wenye nguvu na ulinzi… Enyi vizazi vya Khalid, Salahudin na Muhammad Al-Fatih…

Nyie pekee ndio munaoweza vifua vya ummah kutokana na maadui zake ambao ni maadui wa dini yenu. Nyie pekee ndio mtakaoweza kuvunja udhalili uliofikiwa na Waislamu katika biladi zao, biladi za Uislamu… Mtakuwa na utukufu wa kuanzia na wa kuyahakikisha matarajio ya Ummah bali ummah mzima utakufuateni majeshi yake yote yakiwa nyuma yake na mbele yake. Kwa idhini ya Allah Mtukufu hamtakuwa peke yenu. Basi simameni kutekeleza wajibu wenu Allah akubarikini, simameni mutunusuru, muinusuru Hizb ut Tahrir kwa kusimamisha Khilafah Rashida. Bali hiyosio njia ya ushindi tu kwa wakia ulivyo lakini (Khilafah) katika daraja ya kwanza kabisa ni faradhi kubwa. Kwa kupatikana kwake husimamishwa ahkam, hutekelezwa hudud na bila ya hiyo (Khilafah) hukumu hazitekelezwi wala hadud juu ya watu… Na ambae hafanyi kazi ya kuisimamisha Khilafah na kumueka Khalifah hali ya kuwa ana uwezo, basi madhambi yake ni makubwa kama kwamba amekufa kifo cha kijahili kwa dalili ya dhambi mbaya: «…وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “…Na anaekufa hana bai’a katika shingo yake, huyo amekufa kifo cha kijahilia”… Waislamu wametekeleza sharia ya kumpa bai’a Khalifah kabla hata ya kutekeleza sharia ya kumtayarisha Mtume (maiti yake) na kuizika juu ya umuhimu wake na utukufua wake. Yote hayo ni kwa utukufu wa Khilafah na umuhimu wake…

Enyi watu wenye nguvu na ulinzi…Enyi watu wa nusra… Enyi wanajeshi wa Waislamu:

Hamna miongoni mwenu Mus’ab bin Umeir, As’ad bin Zurara, Usaid bin Hudhair na Sa’ad bin Muadh ambao walimnusuru Allah (SWT) na Mjumbe wake (SAW) wakafuzu duniani na akhera? Hadi kufikia Arshi ya Allah kutikisika kwa kifo cha Sa’ad bin Muadh kwa kuinusuru dini yake. Ametoa Bukhar kutoka kwa Jabir (RA) nimemsikia Mtume (SAW) akisema: «اهْتَزَّ العَرْشُ لِمَوت سعد بن معاذ»  “Arshi ilitikisika kwa kifo cha Sa’ad bin Muadh” … Hivyo hamna miongoni mwenu mtu muongofu atakaemnusuru Allah, Mtume wake na da’awa yake? Hakika ummah unakusubirini. Unakusunirini mulete Takbir walete Takbir pamoja nanyi na ipeperushwe bendera kwa mikono yenu wakuleteeni Lailaha Illa Allah. Kwa hili pekee ndio ummah utainuka na kusimamisha Khilafah Rashida yenye kutekeleza Uislamu ndani na kuubeba kwa ajili ya uliwengu kwa da’awa na jihad. Allah (SWT) aunusuru (ummah): ﴿إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ﴾  “Hakika sisi tunawanusuru Mijumbe yetu na wale walioamini katika masiha haya ya dunia na siku mashahidi watakaposimama”

Enyi wanajeshi wa Allah:

Hakika tunafahamu kuwa hawatashuka malaika mbinguni kutusimamishia Khilafah na kutuongozea jeshi kupata utukufu Uislamu na Waislamu, bali Allah (SWT) anateremsha malaika kutusaidia tukifanya kazi kidhati, kiukweli na ikhlas kurejesha maisha ya Kiislamu duniani na kusimamisha Khilafah. Hiyo ni ahadi isiyopingwa katika kitabu cha Allah (SWT) na hadithi za Mtume (SAW). Wala haliathiri hilo maneno ya wasemao kwamba kusimama kwa Khilafah leo ni ndoto tu. Bali hakika mwenye kusema kwamba kusimama kwa Khilafah nindoto, yeye ndie anayefanya bidi ya ndoto. Ama kusimama kwa Khilafah ni hakika ambayo lazima itokee kwa idhini ya Allah na hutiliwa nguvu na hakika nne zifuatazo:

YA MWANZO: Ahadi kutoka kwa Allah: ﴿وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ﴾ “Amewaahidi Allah wale wlioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kuwa atawafanya makhalifah duniani kama alivyowafanya makhalifah wale waliopita kabla yao”

YA PILI: Bishara kutoka kwa Mtume (SAW) yakurejea Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala huu wa mabavu. Anasema (SAW): «…ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»   “Kisha utakuwa utawala wa mabavu, utabakia kiasi ambacho Allah atataka ubakie. Kisha atauondoa atapotaka kuundoa,kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume”, kisha akanyamaza Mtume (SAW). [Ameitoa Ahmad kutoka kwa Hudhaifa]

YA TATU: Ummah una uhai na uko tayari, tena ni ummah bora ulioletwa kwa ajili ya watu: كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ  “Mumekuwa nyinyi ummah bora ulioletwa kwa ajili ya watu, munaamrisha mema na munakataza maovu na munamuamini Allah”, kwa hiyo hata ukilegea kwa sasa kutokana na kusimamisha Khilafah, uhakika wake ni kama kutulia kwa simba kabla ya kurarua…

YA NNE: Hizb kwa idhini ya Allah ni mukhlis kwa Allah (SWT) na mkweli kwa Mtume (SAW), inachapuza mwendo usiku na mchana kuhakikisha ahadi na bishara, na kama vile inathibitisha kauli ya Mtume (SAW): «لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ عَلَى الْحَقِّ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ كَذَلِكَ» “Halitaacha kundi katika ummah wangu kuwa wenye kushinda kwa haki hawatadhuriwa na anaewaacha mkono mpaka ije amri ya Allah hali ya kuwa wao wako hivyo”. Ameitoa Muslim kutoka kwa Thauban.

Hakika yoyote katika hizi nne inatosha kusema kwamba kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah sio mazigazi. Basi zote nne kwa pamoja?! Basi kwa hiyo, kusimama kwa Khilafah ni hakika yenye kutokea katika wakati ambao hauko mbali kwa idhini ya Allah. Na kwamba kuthibiti kwake na kumakinika kwake baada ya kusimama kwake ni jambo lenye kuhakikishwa akipenda Allah. Na kwamba majengo ya madola makubwa leo yataporomokea mbali. Na dola hizi kihakika ni dhalili mbele ya Allah na mbele ya waja wa Allah. Aliyoyafanya kiumbe mdogo tu (COVID-19) hazionekani dola hizo na kiongozi wake; Marekani kuzungumzia hilo… Na angalieni nini kilichotendeka katika chaguzi zake, kundi moja linauona ni wizi na udanganyifu na jengine linauona ni ushindi mkubwa! Na halitosheki na mashambulizi ya mdomo bali linashambulia taasisi rasmi na kupoteza roho kwa mashambulizi ya silaha katika jengo la kiongozi wa Ubepari. Na makundi hayo mawili yalikuwa yanalingania demokrasia duni! Huu ndio ulimwengu leomkubwa mbele ya mdogo… Na hautaokolewa isipokuwa kusimama kwa dola ya Uislamu, dola ya Khilafah kwa njia ya Utume…

Enyi ndugu wa Kiislamu: Tulikuwatunafanya kazi na kunyenyekea kwa Allah ili isimame Khilafah kabla ya kumbukizi ya miaka mia moja, na ikawa yanatupitia masiku katika miaka hii sabiini ya umri wa Hizb, tukawa tunakurubia kuishika Khilafah kisha inapotea. Pamoja na hayo sisi hatukati tamaa na rehema ya Allah. Sisi tunafanya kazi na macho yetu yanaiangalia Khilafah na nyoyo zinadunda kwa ajili yake, na sote tumekinai kusimama kwake, kwani Mtume (SAW) ametueleza hayo na ametubashiria:  «…ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»  “Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume”. Na yote haya yote ni hakika inayozidisha hima na kutia nguvu azima na kuchochea harara upya na kumfanya mja kiumbe chengine, kutoka hali ya aliyeghumiwa kwa kufikwa na janga kwenda kwenye hali ya mwenye furaha na faraja kwa kutokea janga.

Hivi ndivyo alivyotueleza Mwenye elimu zote na Mwenye habari zote:فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً * إِنَّ مَعَ  الْعُسْرِ يُسْراً “Hakika pamoja na uzito huja wepesi. Hakika pamoja na uzito huja wepesi”. Na hivi ndivyo alivyotueleza mkweli mwenye kusadikishwa katika hadithi tukufu: «وَلَنْ يَغْلِبَ عُسْرٌ يُسْرَيْنِ»  “Katu uzito hautashinda mepesi mawili”. Na pia barua ya Umar kwa Abu Ubaida: “Hakika katu haiwi shida ila Allah atajaalia badala yake ufumbuzi na katu uzito hautashinda mepesi mawili”. Kwa hiyo faraja inakuja kwa idhini ya Allah Bwana wa viumbe wote. Na Khilafah itasimama kupitia mikono waumini wa kweli, na italimaliza umbo la kiyahudi na Palestina itarudi kuwa mji wa Kiislamu. Na Roma itafunguliwa baada ya kwisha funguliwa ndugu yake (Konstantinopoli) na koo tohara zitadhihirisha kauli ya Mwenye nguvu Mwenye kushinda: ﴾وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وزهق الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً﴿ “Na sema haki imekuja na batili imetoweka kwa hakika batili ni yenye kutoweka tu”. Na dunia itajaa sauti za Takbir na ardhi itang’aa nuru ya Uislamu: «لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزّاً يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلّاً يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ»  “Nina apa jambo hili litafika unapofika usiku na mchana na wala hatoiacha Allah nyumba ya udongo na ya manyoya isipokuwa Allah ataiiingiza dini hii kwa nguvu za Mwenye nguvu au kwa udhalili wa dhalili, ataingiza iza kwayo Allah ataupa iza Uislamu, na udhalili kwacho Allah ataudhalilisha ukafiri”. Ameipokea Ahmad kutoka kwa Tamim Al-Dar.

Hakika tunafahamu kwamba maadui wa Uislamu watachukulia kutokea haya ni muhali na wanarejea maneno ya wenzao wenye kufanya mzaha: ﴾غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ﴿ “Imewaghururi hawa dini yao”. Lakini kama ilivyokuwa maneno hayo ni maangamizi kwa wasemaji wake, na Allah akaipa nguvu dini yake na akawanusuru watu wake. Vilevile leo ni maangamizi dhidi yao, Allah Mwenye kushinda Mwneye hekima yuko pamoja na waja wake wenye kumtegemea yeye, wenye ikhlas kwake (SWT) wakweli kwa Mtume (SAW), ambao wanafanya kazi kwa bidii ya dhati bila ya nyoyo na viungo vyao kuiacha kauli yake Taala: ﴾إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً﴿  “Hakika Allah ni Mwenye kushinda jambo lake hakika amejaalia kila kitu kipimo maalum”. Hawa kila    siku inayopita wanajikurubisha kwenye kadar hii﴿وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ“Na Allah ni Mwenye kushinda juu ya jambo lake lakini watu wengi hawajui”

Wasalamu Alaykum Warahmatullah Wbarakatuh.

Jumamosi, 29 Rajab 1442 H Ndugu Yenu
13/3/2021 M Ata Bin Khalil Abu Al Rashtah   
Amiri wa Hizb ut Tahrir

“Bofya Hapa uDownload Pdf”

Maoni hayajaruhusiwa.