Ramadhani Itusukume Kujiamini kwetu

8

Mwezi wa Ramadhani unasonga mbele. Mwezi ambao huunganisha Umma wetu mtukufu katika Ibada tukufu ya kufunga ambayo ni nguzo katika nguzo za dini yetu ya Kiislamu.

Hapana shaka yoyote kwamba Ramadhani ni mwezi wa kujipinda kwa nguvu zetu zote kwa kila aina ya Ibaadat kama kukithirisha kuisoma Qur-ani tukufu, kuswali swala ya tarawehe, kubakia itikafu miskitini, kuomba dua, kutaka maghfira, kutoa sadaka na mengi mengineyo katika yale yanayostawisha fungamano letu moja kwa moja kwa Allah (Taala). Kwa hakika mwenye kuyabeza hayo amejinyima thamani kubwa ya mwezi huu mtukufu Ramadhani.

Hata hivyo, katika mwezi huu pia ni wajibu tuutanue upeo wetu kinyume na tulivyozoea 
kuichukulia haiba ya Ramadhani kwamba ni mwezi wa Ibaadat za kiroho tu. Kwa udhati ikiwa tutaichukulia Ramadhani kwa mtizamo wa upande mmoja wa Ibaadat za kiroho tu tutakua tunaufanyia dhulma mwezi huu mtukufu.

Hii ni kwa sababu Qur-ani inatukumbusha kwamba mwezi huu ndio iliposhushwa kuwa muongozo kwa watu wote katika kila kipengee cha maisha yetu. Yawe mambo ya Ibaadat kama swala, dhikri, hijja, itikafu, sadaka. Pia kwa upande wa pili katika mambo ya muamalati (mjumuiko wa watu) kama kuuziana, utawala, vita, ndoa n.k. Kwa hivyo mwezi huu mtukufu utukumbushe na utuharakishe kuubeba msimamo wetu wa asili nao ni kuuchukua Uislamu kama mfumo kamili na bora kwa kila kipengee cha wanadamu wa zama zote.

Kwa bahati mbaya tangu kuibuka mfumo batil wa kibepari mwishoni mwa karne ya 18 miladia na kuangushwa Dola ya Kiislamu [Khilafah Uthmania] katika mwaka 1924 [miladi], fikra ya kuitenganisha dini na maisha (secularism) imekua ikipigiwa debe na kufanywa ndio kaulimbiu na makafiri, wakala wao katika vibaraka, wanafikra wao, wanavyuoni waovu kiasi cha kuwachanganya baadhi ya Waislamu na kupelekea kuifanya dini ya Kiislamu kana kwamba ni dini ya masuala ya Ibaadat fulani fulani tu.

Huu ni msiba mkubwa! uliowapelekea baadhi ya Waislamu kupoteza thika [confidence] ya dini yao na kuufanya Uislamu kama dini mithili ya dini nyengine kama ukiristo, ubudha na uhindu, kwa kuiwasilisha kuwa ni dini ya kulialia sana kwa kufanya Ibada za kiroho tu bila ya kuwa na suluhisho lolote maishani, na badala yake kutegemea ubepari kutatua matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Wakati Ramadhani ikiwa ukingoni hatuna budi Waislamu kurejesha tena ufahamu wetu wa asili na kurejesha thika/confidence ya dhati kwa kwa dini yetu

#UislamuniHadharaMbadala

8 Comments
 1. Also I ve shared your site in my social networks!

 2. Live TV says

  Thank you for great article. look forward to the continuation.Live TV

 3. turffontein live stream free says

  Thank you for great article. look forward to the continuation.-mediathek vox

 4. hey dudes kids says

  lso thank you for allowing me to comment!. – hey dudes for kids

 5. Shoe Palace says

  For the reason that the admin of this site is working no uncertainty very quickly it will be renowned due to its quality contents. Shoe Palace

 6. air jordan 1 shoes says

  Very nice blog post. definitely love this site.

 7. their explanation says

  The scenery is breathtaking, thank you! recommended you read

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.