Syria na Majaribio yanayojirejea kuipaka Matope Hizb Ut Tahrir

0

Jaribio la kuinasibisha Hizb ut Tahrir na ISIS halikufanikiwa licha ya juhudi kubwa inayoendelea. Kwa hivyo, mashambulizi mapya ziada yalihitajika kwa ajili ya kukidhoofisha chama hiki kilichojizatiti kufanya kazi ya kurejesha utawala wa Khilafah Rashidah kwa kupitia manhaj ya Utume. Dola ambayo kwa mujibu wa Sharia ya Kiislamu ndio njia pekee itakayoweza kuutabikisha Uislamu katika maisha na ndio suluhisho pekee la mashaka yote yanayowakumba Waislamu. Jaribio la karibu zaidi la kitoto lililokosa haya kupitia chombo cha habari limeibuka likidai eti makundi kutoka Hizb ut Tahrir yanaungana na makundi makundi ndani ya Syria.

Hizb ut Tahrir ndani ya Syria tungependa kueleza yafuatayo:

Kwanza, Hizb ut Tahrir haikuasisiwa leo, bali ni chama (cha kitambo) cha kisiasa kilichoasisiwa toka mwaka 1953 na Sheikh Taqiyyuddin Al-Nabhan (Rahimahu Allah). Ni chama cha kilimwengu ambacho kazi yake imesambaa katika nchi nyingi za Kiislamu na katika baadhi ya nchi nyengine za kilimwengu, na hivi sasa kinaongozwa na Mwanachuoni mkubwa Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al Rashta.

Chama kinashikilia (tabanni) mjumuiko wa fikra na mafahim (concepts) zinazopatikana katika vitabu vyake mbalimbali. Pia chama kimechukua njia maalumu inayoandama na manhaj ya Mtume (SAAW) katika kurejesha dola.
Njia hii hutegemea zaidi misuguano ya kifikra, mivutano ya kisiasa na kupitia utafutaji nusra (nguvu za ushindi) kutoka kwa watu wenye nguvu, athari na ushawishi. Ni njia iliyothibitishwa ambayo haibadiliki kwa kubadilika kwa zama wala eneo, na kamwe haitobadiliki kwa kubadilika kwa hali kwa sababu imethibiti kutokana na misingi ya kisharia kutokana na na dalili za kisharia.

Pili, majaribio haya ya upotoshaji wa wazi wa vyombo vya habari yamedhamiriwa kuichafua Hizb ut Tahrir katika bongo za Waislamu ili waiepuke na kutafuta uhalali wa kuipaka matope na kuichafua fikra ya Khilafah inayoilingania.

Tatu, mashambulizi ( shutma )zote za kuichafua Hizb na kupotosha ufahamu wa Khilafah zitaondoka mikono mitupu na kushindwa kama shutuma nyingine zilivyoshindwa kabla ya hizi, kwa uwezo ya Allah Taala, vitimbi vya wasaliti vitarejea katika shingo zao wenyewe. Allah SW Anasema:

إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنْ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لاَ يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ

“Hakika Allah huwalinda wale Walioamini. Hakika Allah hampendi kila khaini na aliyekufuru”

[Al-Hajj: 38]

Ahmad Abdul Wahab
Kiongozi wa Afisi ya Habari
Hizb ut Tahrir – Wilaya ya Syria

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.