Mwito Wa Swala Ya Jeneza (Ghayb) Kwa Ndugu Zetu Waliouwawa New Zealand

Kwa waislamu wote

Asalaam Alaykum,
Ijumaa iliyopita (15/03/2019) ndugu zetu Waislamu 50 waliuawa kinyama na kwa dhulma wakiwa misikitini kwa Swala ya Ijumaa huko nchini New- Zealand.
Kwa kuwa Ummah wetu ni Ummah mmoja, na maumivu yake ni kama ya kiwiliwili kimoja, tunawaomba kwa heshima kubwa tutekeleze Sunna ya kuwaswalia (Swalatul ghayb) ndugu zetu hao waliouwawa
Tutekelezeni ibada hiyo ikiwa pia ni dhima mbele ya Mola wetu ya kukemea dhulma waliyotendewa Waislamu wenzetu.

Tunawaomba Waislamu washiriki katika ibada hiyo tunayoitarajia kufanyika misikiti mbali mbali. Masjid Rahma, Buguruni kwa Madenge ni mmoja wapo utakaotekeleza mara baada ya Ijumaa ya tarehe
22/03/2019
Jazakum llah

Ndugu yenu
Sheikh Mussa Kileo,
Imamu Mkuu
Masjid Rahma Buguruni – Dar es Salaam
na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano kwa Umma
Hizb ut Tahrir Tanzania
Mob:0658 39 39 95
Pepe: kileoccc@gmail.com

Maoni hayajaruhusiwa.