Muislamu na Ujinga

Ujinga ni jambo ambalo limeleta madhara mengi katika jamii ya waislamu. Na madhara yanaendelea kuutafuna Ummah wa kiislamu kila uchao. Na msiba mkubwa zaidi ni watu wengi katika Ummah wa kiislamu kusoma hawataki au kujiendeleza kusoma wasivyovijua pia wamekuwa wazito. Lakini hawakubali kuwa ni wajinga. Na miongoni mwa madhara makubwa yanayowafika waislamu kutokana na ujinga ni haya.

1. Kutokana na ujinga muislamu amekufa akitetea batili. Kama kufa akitetea vyama vya kidemokrasia au kufa akitetea nchi yake dhidi ya waislamu wenzake…..

2. Kutokana na ujinga umepelekea muislamu akatolewa Katika dini yake (kuritadi)

3. Kutokana na ujinga wa waislamu imekuwa ni vyepesi kwa makafiri kupenya Katika safu za Waislamu na kufanya watakavyo.

4. Kutokana na ujinga Muislamu anawahudumia makafiri dhidi ya Uislamu.

5. Kutokana na ujinga Muislamu amekuwa ni mwenye kumuabudu shetani. Au mifumo yake kama vile secular, demokrasia, ujamaa,……

6. Kutokana na ujinga tumemfanya adui ndio rafiki na rafiki ndio adui.

7. Kutokana na ujinga ibada zetu zinaharibika kwa kufanywa ndivyo sivyo na maasi yetu yanazidi.

8. Kutokana na ujinga utawapeleka Wengi Katika moto wa jahanamu. Kwa kufanya yasiofaa na kuacha yanayofaa.

Tiba ya ujinga ni Elimu. Na hii Ina maana kwamba mwanzo wa kuondosha matatizo ya waislamu ni Elimu. Na elimu hapa ni Elimu ya sheria na fikra na siasa inayotokana na Itikadi ya kiislamu. Na mwanzo wa mabadiliko unaanza kwa kubadilisha akili.

Ni wajinga wangapi ambao hudhani kuwa ni wasomi, na kila unavyozidi ujinga wa mwanadamu ndio anavyodhani kuwa yeye ni mjuzi zaidi. Na kila mwanadamu anavyozidisha elimu ndio hujiona kuwa yeye ni mjinga hafahamu Isipokuwa kidogo tu.

Kosa kubwa ni kumkinaisha mjinga anaejiona anajua Bali lililobora ni kumkinaisha ambaye anajiona hajui au ana elimu ndogo na anatafuta elimu.

Na jambo bora Katika mjadala jumla ni kubainisha Mstari ulionyooka juu ya ile mistari iliyopinda pinda. Kisha kujadiliana na yule anaetaka kufahamu na sio mwenye kutaka mjadala ili aonyeshe makosa ya mwenzake na nguvu za hoja zake na usahihi wa Rai yake na ufasaha wa ulimi wake.

Tiba kwa wajinga haiwi kwa kuwasifu au kuwaita kwa sifa ya ujinga, Bali inakuwa kwa njia ya upole na Kujaribu kuwaelewesha na kuwaonyesha lililosawa. Na kuwa weka upande wetu Katika vita yetu dhidi ya maadui zetu kiujumla. Na kuwaacha na kuwatenga ina maanisha ni kuwaacha kuwa ni kiwindwa cha maadui zetu kwa sababu ya ujinga wao. Na ina maana kwamba kuelemea kwao kwa upande wa maadui zetu ni kuzidisha kundi la wapinga haki. Kwani kwa vyovyote vile mwisho wa siku wao ni sehemu Katika sisi. Na mwanzo tulikuwa kama wao lakini Allah alituneemesha kwa kutupa elimu na utambuzi.

Na tambua kuwa kumuongoza kwako mtu Katika njia sahihi na kheri na kukamatana na dini ni kheri kwako kuliko dunia na vilivyomo. Na wajinga kukupuuzia Usikate tamaa kwani kazi ya kuwazindua watu na kuwaonyesha haki na kuwaongoza Katika njia ambayo Allah anairidhia ndio njia ya Manabii. Nao hawakukata tamaa wala hawakupumzika wala hawakukubali Katika ajenda mbovu za watu wao pamoja na tabu walizozipa.

Tahadhari sana isije ikakuhadaa elimu yako, huenda ukawa mjinga usiejijua, na ukawa adui wa dini yako na Ummah wako hali ya kuwa hujui. Usijigambe sana kwa kuwa wewe ni mwanazuoni mkubwa sana Bali pendelea kusema mimi mwanafunzi, penda kuwasikiliza wengine, jadili miono yao, na zingatia kuwa yale unayoona kwa wenzio sio sahihi kuwa ni makosa yawezekana kuwa ni sahihi. Na yako unayoona kuwa ni sahihi inawezekana yakawa sio sahihi. Na tambua kuwa maafa ya elimu ni kiburi na majivuno. Hivyo kuwa mnyenyekevu na msikivu kwa wengine.

Na tambua hata uwe na elimu kiwango gani jua ni kidogo tu. Na ukiwa na mtazamo huo siku zote utajiona na kiumbe dhaifu mjinga wa vingi.

Ujumbe.
Tufahamu kuwa wanaomuogopa Allah kisawasawa ni wale wajuzi, wasomi. Kwa maana uchamungu kwa mjinga vigumu kukaa pamoja.

( ۗ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ)
“Hakika wenye kumuogopa Allah katika waja wake ni wale wasomi Hakika Allah ni Mtukufu na msamehevu”  [Surat Fatir 28]

Na Ifahamike siku zote hawalingani wenye kujua na wasiojua. Hivyo basi kila mmoja ajitathimini mwenyewe, je yeye ni mjinga na ujinga wake umempa madhara Gani mpaka Sasa, na je ujinga wake utamuweka sehemu gani siku ya kiama.

Au yeye ni katika ni miongoni mwa wenye kutafuta elimu ili aweze kujikinga na madhara ya ujinga.

Au yeye mwanazuoni na neema ya elimu aliyopewa anaitendea haki, na kumpelekea kuwa mchamungu au ujuzi wa vitabu vingi kichwani lakini elimu aliyonayo haimsukumi kuwa mchamungu wala kuisimamia haki kwa kufuata njia ya Manabii.??

By Sheikh Khatibu Imran Abuu Khaliil
Mwanachama Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.