Mti wa Fitna

Mti wa fitna unakuwa kimaumbile katika kipindi ambacho hakuna dola ya khilafah. Lakini uwepo wa khilafah mti huu wa fitna hauwezi kupata nafasi ya kukua.

Na katika fitna kubwa ambazo zipo Katika ulimwengu wa kiislamu sasa ni hizi zifuatazo;

1. Fitna ya ulinganizi wa mfumo wa kisekula demokrasia na dola za kizalendo na kwa masikitiko zaidi zinalinganiwa na wale kuonekana ni wenye elimu mbele ya macho ya waislamu kwasababu ya maslahi ya kidunia.

2. Fitna za kuwakufurisha waislamu na kuhalilisha damu zao. Fikra zilizotengezwa kwa makusudi na wamagharibi kupitia magenge ya watu katika waislamu. Na kuwakufurisha wote ambao hawakubaliani nao kimtazamo. Kama walivyofanywa ibn Saudi na mwenzake ibn Wahab na hata kufikia kuuawa waislamu wakiwaita na washirikina makafiri hawana tawheed. Au genge la Albaghdady aliemaliza kazi aliyotumwa na wamagharibi huko Katika ardhi ya Shamu.

3. Fitna kuwatukuza makafiri juu ya Waislamu na kuhalalisha kuvunjiwa heshima zao na kuporwa Mali zao na ardhi zao na matukufu yao. Kama tunavyoshudia yanayofanywa na watawala wa miji ya waislamu kama Uturuki, Oman, Misri, Pakistan, Saudi, Iran, …

4. Fitna na kuingiza mambo kwenye dini mambo ambayo hayana asili yoyote Ile Katika dini. Kama vile visa vya kumtukuza Hussein ibn Ally radhi za Allah ziwe juu yao. Kama wafanyavyo mashia kisa cha kwamba Unaweza kuwasikiliza hao wajinga wakimtukuza Hussein kuliko hata Mtume saw, Jibrili na Maswahaba wote na wakati mwingine wapo wanaomsifu kuliko hata Mwenyezi Mungu. Na msiba mkubwa ninausikia na kwa yule mwenye kuwasikia hawa Madajjali wanaompa Hussein sifa hizo akanyamaza kimya. Na kwa Jina la Hussein wamehalalisha na kuharamisha hali ya kuwa Hussein kwa hayo hausiki hata kidogo.

5. Fitna ambayo Imekuwa kwa uwazi ya kuwatukana Maswahaba matusi mabaya na wakeze Mtume saw, kwa kutokuwepo kwa Khilafah ni fitna ya kuwatukana Maswahaba na wake za Mtume saw.

6. Fitna ya baadhi ya masufi Kuyatukuza makaburi kinyume na utaratibu wa kisheria kiasi cha kufikia kuonekana wazi kuwa wanaabudu makaburi.

7. Fitna ya kuhalalisha haramu za Wazi kama vile ulaji wa Riba, na kupiga kura kuchagua viongozi watakaokwenda kuhukumu kinyume na sheria za Allah. Kwa msingi wa maslahi kwanza. Msingi ambao bila ya shaka ni msingi wa kikafiri. Na msingi wa kiislamu ni halali na haramu tu.

8. Fitna ya kupuuzia mambo ya lazima Katika dini kama swala……….na kuonekana ni mambo ya khiyari kwa muislamu kuyafanya.

9. Fitna ya waislamu kukaa kimya Katika suala la kurejesha dola ya kiislamu ya kiulimwengu khilafah, kana kwamba ni jambo ambalo haliwahusu pamoja na kuwa khilafah ni mama wa faradhi zote. Na ndio nguzo imara itakayowaweza Kutekeleza Sheria zote ambazo Allah ametaka zitekelezwe.

10. Fitna ya upuuziaji wa waislamu katika changamoto na madhila yanayowafika ndugu zao waislamu Katika maeneo mbalimbali duniani kama vile mauaji, ubakaji…….kana kwamba yanayowafika waislamu wenzao hayawahusu.

11. Fitna ya baadhi ya watu katika waislamu kuona kuwa juhudi za kutaka kurejesha maisha ya kiislamu kwa kuurejesha serikali ya Kiislamu ya kiulimwengu khilafah, ni kuleta vurugu. Na wakasimama kuhamasisha utiifu kwa serikali za kidemokrasia zinazohukumu kwa ukafiri.

Niaminini hata kutolewe darsa na khutba maelfu kwa maelfu haziwezi kuondosha fitna hizi Isipokuwa dola ya kiislamu khilafah ndio inaweza kuondosha fitna hizi. Na hazitaondoka fitna hizi Isipokuwa kwa dola ya kiislamu khilafah. Kwani dola hiyo kwa kutumia nguvu zake na umadhubuti wa hoja zake na nguvu ya fikra yake itaondosha fitna zote hizi ambazo zimewafika waislamu.

Ama darsa na khutba zinatumwa kwenye internet na katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuzungumzia fitna hizo haziwezi kuondosha fitna hizo itakikanavyo. Na maamuzi ya kuwaua wenye kufanya vitendo hivyo kama wanavyofikiria baadhi ya watu kuwa ndio njia sahihi ya kuondosha kutazidisha mashaka zaidi na zaidi.

Na Sheikh Khatibu Imran Abuu Khaliil
Mwanachama Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.