Matokeo ya Kukata Mwenye Kazi Sehemu Katika Mshahara wa Mfanya Kazi na Kuongeza Sehemu Yake

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Assalamu Alaykum Sheikh, Allah (SWT) akuhifadhi na atupe nusra kupitia kupitia wewe, Amiin.

Katika nchi nyingi za magharibi tuna utaratibu unaoitwa Mpango Wa Pensheni. Unakuwa hivi; mfanyakazi anachangia kiasi fulani cha fedha kutoka katika mshahara wake na kuikabidhi kampuni anayoifanyia kazi. Kampuni pia huchangia kiasi fulani cha fedha ambacho hakitokani na mshahara wake kulingana na kiasi mfanyakazi alichochangia. Mfanyakazi akifikia umri wa kustaafu ile kampuni inamlipa pensheni yake aliyochangia na kampuni pia kile kiasi cha fedha ilichochangia.

Baadhi ya mashirika huekeza ile michango iliyotolewa na mfanyakazi katika vitega uchumi vyengine kama kununua hisa katika mashirika yanayofanya biashara za ulevi na riba.Na baadhi ya mashirika hayawekezi kabisa zile fedha.

Unaweza kutueleza ikiwa mpango huu wa pensheni unaruhusiwa katika Uislamu? Kwa sababu wengi wetu katika eneo langu tumeshatia saini na mashirika yetu, kwa vile jambo hili limefanywa lazima na serikali.

Nataraji swali langu liko wazi. Allah akulipe kheri.

Waalaykumu Salam Warahmatullah Wabarakatuh,

Jibu:

1.Mwajiri akikubaliana na mwajiriwa kumtibu afya yake au kumpa mshahara wa kiinua mgongo(malipo ya kustaafu) baada ya umri maalum, malipo yanayotokana na sehemu katika mshahara wa mfanya kazi yanayokatwa katika muda maalum, na huongezewa na fungu maalumu analolichangia mwajiri… Muamala huu wa muajiri kwa waajiriwa wake pindi ikiwa jambo hili limeambatana na mkataba uliopitishwa tayari kati ya mwajiri na waajiriwa kama ni sharti la mkataba wa kazi. Hillo ni kwasababu mkataba wa asili ni mkataba wa kuajiriwa, na hili linajulikana. Mwajiri kujifunga kumtibu mwajiriwa au kumlipa mshahara wa kustaafu ni sharti lililoambatana na mkataba wa kazi. Na masharti katika mikataba haizuiliwi isipokuwa pakipatikana nass inayoyazuia kama yakihalalisha haramu au yakiharamisha halali, hapana haja ya nass iyajuzishe ili yajuzu bali yanahitaji kukosekanwa kwa nass kuyazuia. Kutoka kwa Kathir bin Abdillah bin Amr bin Auf  Almuzany kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba Mtume (SAW) amesema: “Na Waislamu lazima wajifunge na masharti yao isipokuwa sharti linaloharamisha halali au linalohalalisa haramu”. Imepokewa na Tirmidhy. (Angalia Shakhsiyyah juzuu ya tatu, mlango wa Humkul Wadh’I – Al-Shart)

Huu upande mmoja, ama upande mwengine, kile anachopewa mfanyakazi ni sehemu inayotokana na fungu la malipo ya mfanyakazi lililokatwa na akaongezewa na mafungu kutoka kwa mwajiri. Mwajiri anaweza kumpa mwajiriwa wake katika mali yake kiasi ambacho anapenda.

2.Ama ikiwa mkataba wa matibabu ya afya  au malipo ya kustaafu ni mkataba hasa wenyewe kidhati yake, yaani kwa mfano, kuanzisha taasisi ikatangaza kwa umma kwamba anaetaka imtibu pindi akiumwa au anaetaka kupata malipo ya kusataafu  baada ya umri maalumu basi atupe sisi kiasi fulani cha fedha kila mwezi…Mkataba huu haujuzu kwasababu ni mkataba usioepukana na kitu kisichojulikana… Mkataba huu ni batili haujuzu

  1. Ama kuhusu taasisi kujishughulisha na mali kwa haramu… Ikiwa jambo hili linafanyika kwa kukubali kwako, yaani ukikubali kujishughulisha na riba kwa kile unachokitoa cha fedha, na ikiwa hujakubali basi haiwi(ile taasisi haijishughulishi na riba). Hapa itakuwa haifai wewe kukubali kule kujishughulisha na riba. Ama ikiwa kule kujishughulisha (na riba au mfano wake) ni bila ya ridhaa yako, yaani si chaguo lako bali wao wanazishughulisha (zile fedha) bila ya ridhaa yako, ni kwa mujibu wa kanuni tu za lazima za nchi, basi huna chochote dhidi yako (yaani huna kosa lolote)…

Kwa ufupi: Ukiwa ni mfanya kazi, na kwa mujibu wa kanuni za lazima za nchi, mwajiri anakata fungu kutoka katika mshahara wako na yeye anakuogezea fungu, na anaekeza mali(fedha) hizi bila yaw ewe kutoa maoni yako yoyote katika hilo, yaani bila ya ridhaa yako, bali ni kwa mujibu wa kanuni za lazima za nchi tu. Na baada ya umri maalumu anakulipa malipo ya kustaafu au anakutibu kiafya… Inafaa wewe kuchukua haya malipo ya kustaafu na matibabu. Kwasababu yote hayo ni kwa mwajiri kukata fungu kutoka katika mshahara wako. Nayo ni kwa mpango wa lazima(wa serikali).

Haya ndio ninayoyatilia nguvu. Allah ndie mjuzi zaidi na Mbora zaidi wa hekima.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashta

04, Raibiu Than 1440H – 11,  December 2018

Maoni hayajaruhusiwa.