Brexit Yathibitisha DemokrasiA ni Mchezo wa Kuigiza

Brexit ni mpango maalumu wa Uingereza kujitoa katika Jumuia ya Ulaya ambao ulifikiwa tarehe 23 Juni 2016 uliofikiwa baada ya waingereza kupiga kura ya maoni chini ya serikali iliyoongozwa na David Cameron, ambapo asilimia 51.9 sawa na kura 17.4 milioni zilikubali mpango wa kujitoa dhidi ya asilimia 48.1 sawa nakura 16.1 milioni.

Mpango huu ulipelekea Waziri Mkuu Cameron ajiuzulu kwa kushindwa, kwani yeye na chama chake walikuwa hawakubali Uingereza kujitoa.

Kuazia tarehe 29 Machi 2017 ikawa ndio tarehe rasmi ya kuanza mchakato wa miaka miwili chini ya Waziri Mkuu mpya Theresa May, na kuangalia namna mahusiano yatakavyokuwa kati ya Jumuiya ya Ulaya na Uingereza. Mazungumzo yalianza rasmi trehe 19 Juni 2017.

Pamoja na ridhaa ya wapiga kura wa Uingereza, na makubaliano ya Waziri Mkuu May na Jumuiya ya Ulaya (EU) ya novemba 25, 2018, Bunge la Uingereza lilipiga kura Januari 15 kukataa makubaliano hayo.

Jambo hili limemfanya Theresa May aaibike na kuanguka kisiasa ndani ya chama chake na pia kwa vyama vyengine na raia wa kawaida. Hivyo, inaweza kupelekea kuanguka kwa serikali yake au hata kama haitoanguka bado ushawishi wake utakuwa mdogo.

Pia tayari kumeanza kuwepo tetesi na takwimu zinazofanywa na taasisi tofauti kuwa waingereza wengi waliounga mkono mpango wa Brexit wamebadilisha mawazo yao, na sasa hawataki Uingereza kujitoa katika jumuiya hiyo.

Katika jambo hili kuna mambo mengi yakujiuliza kuhusu demokrasia.

Kwanza, ikiwa wananchi wa Uingereza wameona wajitoe katika Jumuia ya Ulaya na wameshinda kura ya maoni kiasi cha kupelekea Waziri Mkuu wa wakati ule David Cameron kujiuzulu, ni kipi sasa kinachochelewesha na kupelekea watu kuanza kukusanya takwimu upya juu ya jambo ambalo hata hatua ya kujitoa kwenyewe haijatekelezwa?

Pili, kwanini kuanze kampeni ya kurejesha tena kura ya maoni ili wananchi wapige kura tena kama waendelee au wasiendelee?

Tatu, kwanini Jumuiya ya Ulaya isiheshmu maamuzi ya kidemokrasia yaliyofanywa na wananchi wa Uingereza, na badala yake inaweka mashinikizo mazito na magumu ili kuwalazimisha waingereza wabakie ndani ya jumuiya hiyo, pamoja na kuwa wao (Jumuiya ya Ulaya) hudai kuwa ni vinara na waumini wakubwa wa demokrasia?

Kwanini waingereza walazimishwe kurudi katika kura ya maoni hata hawajajitoa, lakini mawazo ya raia hao hao yanapobadilika juu ya watawala wao, husubiriwa hadi watawala wamalize muhula wao wa kutawala, ndio ipigwe kura nyengine?

Kwa upande mwengine, pia kumeshuhudiwa katika serikali ya Theresa May mzozo mkubwa na mgongano wa kisiasa kiasi cha kupelekea kujiuzulu kwa mawaziri wake wengi kwa kutofautiana imma na yeye au na misimamo ya masharti ya Jumuiya ya Ulaya . Kwa mfano, Waziri wa Masuala ya Kujitoa katika Jumuiya ya Ulaya David Davis alijiuzulu 9 Juni 2018, na nafasi yake kuchukuliwa na Dominic Raab ambaye nae pia alijiuzulu Novemba 5, 2018. Bila ya kutaja mawaziri wengine wengi akiwemo pia Boris Johson aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni na Jumuiya ya Madola.
Baadhi ya wanasiasa hao walikuwa katika mchakato wa mazungumzo ya Brexit huko Brussels. Mzozo huu wa kugawanyika kwa wabunge pia umeoneshwa na Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza Tony Blair huko Davos.

Ukiangalia kwa makini juu ya mpango huu wa Brexit utagundua kuwa waingereza walio wengi hawakubaliani na Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa kuangalia maslahi yao ambayo wengi wamejikuta wakipoteza ajira zao au kupata mishahara midogo hasa kwa kuwepo na wimbi kubwa la uhamiaji kutoka Ulaya, hususan Ulaya Mashariki ambalo limekuja kuhodhi nafasi hizo za ajira.

Vilevile, kwa upande wa mabepari wa Uingereza, kujitoa katika Jumuiya ya Ulaya ni hasara kubwa kiuchumi na kibiashara kwao, kwani itawaondoshea rasilimali watu rahisi ya vibarua (cheap labor) kutoka nchi wanachama, ambao kwa kuwanyonya huwangizia mabilioni ya faida, bila ya kusahau kunufaika na soko kubwa lisilo na vikwazo vyovyote la Schengen lenye idadi kubwa ya watu wasiopungua 419,392,429.

Jee kwa uongo huu haijawadhihirikia Waislamu na wenye upeo miongoni mwa wasiokuwa Waislamu kuwa mataifa ya kibepari ni mataifa ya kinafiki, hujifanya kuhubiri na kulazimisha demokrasia nchi changa, ilhali nchini kwao huitumia kuwa ni mchezo wa kuigiza, upuuzi na udanganyifu, wakijifanya kuiunga mkono inapowafikiana na maslahi yao, na kuitupa chini inapogongana nayo, hata kwa gharama ya kuteseka na kuwatia dhiki raia wao.

فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنْ الأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ (الحج: 30

“…Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, na jiepusheni na kauli (mfumo) wa uwongo”
(TMQ AL-HAJJ: 30)

23 Jumada al-awwal 1440 Hijri | 29-01- 2019 Miladi

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania

https://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.