Ubepari: Mfumo wa Maadili Mabovu

Ni jambo la kawaida kila mara wanasiasa kuwaasa viongozi wa dini na wanajamii kwa ujumla kujitahidi kuwajenga vijana kwa maadili mazuri, wakionesha kuwa wengi wa vijana wamebeba mila za kimagharibi ambazo zimepelekea kudorora kwa maadili.

Suala la kuporomoka maadili kwa wakati huu linaonekana kupewa nguvu zaidi kutokana na kuwepo mjadala mkubwa juu wa baadhi ya wasanii wa muziki kuendelea kuonyesha wazi wazi tabia ambazo haziendani na maadili yaliyozoeleka katika jamii.

Suala la mmonyoko wa maadili linachukuwa nafasi mkubwa katika mijadala ya kitaifa na kimataifa ambapo madola kama Marekani, Uingereza ambayo ndio vinara na walinganiaji wakubwa wa demokrasia yamekuwa ni wahanga wakubwa wa mmomonyoko wa maadili.

Mada ya kuporomoka maadili inapaziwa sauti kila upande ikioneshwa na makundi mbalimbali ya watu katika jamii, kuwa vijana wengi wanapotea. Makundi ya kijamii kama viongozi wa dini, wanafikra, wanasiasa na watunga sera wanapiga kelele kwamba vijana wengi hususan wa mijini hawana tabia na maadili mazuri kutokana na kuiga mfumo wa kimagharibi.

Sababu kubwa ya msingi ya kuporomoka maadili ni mfumo wa kibepari uliojengwa juu ya usekula unaotenganisha dini na masuala mengine ya Umma, fikra ambayo pia inafundisha kutoipa dini umuhimu, amma kuitekeleza na kuiacha katika nyumba za ibada peke yake, ilhali kwenye maeneo mengine mtu atekeleze misingi ya kisekula ambayo huhimiza matendo machafu na maovu. Halkadhalika fikra hii ya kisekula imeleta dhana ya ‘uhuru’ unowasukuma vijana wengi na wanadamu kiujumla kutenda matendo maovu.

Mojawapo ya matokeo mabovu ya ubepari ni utumwa wa kimila, kitamaduni na kifikra kwa Waislamu na wanadamu kiujumla kuiga muono wake mbovu na tamaduni zake chafu. Hali hii ya kusikitisha imewafanya wengi kufikiri kwamba maendeleo ya kimada na mafanikio waliyofikia wamagharibi katika sayansi na teknolojia yanawafanya pia wafuzu kuwa kiigizo chema linapokuja suala la maadili.

Kupambana na mmomonyoko wa maadili ulimwengu wa tatu ikiwemo Tanzania kunahitaji kutupa na kuachana kimsingi na mfumo wa kibepari na kufuata mfumo mbadala ambao ni Uislamu.

Afrika chini ya Uislamu itakuwa ni sehemu bora kimaadili na kijamii kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo ilikuwa ni kiigizo.
Uislamu una nidhamu thabiti ya kijamii na nidhamu nyenginezo ambazo hudhamini utulivu na maadili mema kwa jamii na kwa wanadamu kiujumla.

#UislamuniMfumoMbadala

Kaema Juma

Maoni hayajaruhusiwa.