Ni Kipi Kilicho Nyuma ya Mgogoro Baina ya Saudi Arabia na Qatar?

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali.

Trump alisema katika mkutano wa waandishi habari akiwa na mwenzake wa Romania katika ikulu ya White House mnamo 9/6/2017: ((…wahusika wakuu katika eneo wamekubaliana kusitisha ufadhili wa ugaidi, ima kifedha, kijeshi au hata kusaidia kimaadili. Taifa la Qatar, kwa bahati mbaya, kihistoria limekuwa mfadhili mkubwa wa ugaidi. Na kwa kutokea kwa mkutano huo, mataifa yalikuja pamoja na kuongea nami kuhusu kuikabili Qatar juu ya tabia yake. Kwa hivyo tukawa na uamuzi wa kufanya: tuchukuwe barabara rahisi, au hatimaye tuchukue kitendo kigumu lakini kinachostahili?

Ni lazima tukomeshe ufadhili wa ugaidi. Nimeamua, pamoja na waziri wa kigeni Rex Tillerson, makamanda wetu wakubwa na wanajeshi, wakati umewadia kutoa wito kwa Qatar kukomesha ufadhili…)) [Al-Youm As-Sabi’, 9/6/2017]. Je, hii yamaanisha kuwa mgogoro baina ya Saudi Arabia na Qatar umesukumwa na Trump? Ikiwa hii ni kweli, kwa nini Trump anachukua hatua hii, akitambua kuwa kambi kubwa ya Kiamerika katika eneo iko Qatar? Vyombo vya habari pia vimenasibisha msimamo wa Qatar juu ya iran, kundi la Ikhwan, au Hamas, kama sababu ya uhasama wa kisiasa baina ya Saudi Arabia na Qatar. Tuelewe vipi taarifa ya Trump kuambatana na yale yanayokorogwa katika vyombo vya habari? Na mgogoro huu waelekea wapi? Je utapelekea kujiondoa au kufukuzwa kwa Qatar kutoka katika jumuia ya ghuba? Shukran.

Jibu

Kwanza: ndio, anayesukuma mgogoro huu uliojitokeza ni Amerika. Kwa maana nyengine, ni raisi wa Amerika Trump, lakini kabla ni fafanue juu ya hilo, naanza na sehemu ya mwisho ya swali. Baadhi wanafikiri kuwa sababu ya mgogoro wa ghuba wa Qatar, kama ulivyo ripotiwa na vyombo vya habari au kama unavyo chochewa, ni usaidizi wa Qatar kwa (kundi la) Ikhwan al-Muslimeen au ushirikiano wake wa kimikakati na Iran, huku wengine wakisema kuwa sababu halisi ya mgogoro huu ni kutokana na uhasama wa jadi baina ya familia ya Hamad na familia ya Zayed ulioanza miaka ya sabiini wakati Imarati ilipobuniwa. Hii ilipelekea Saudi Arabia kumfuata mshirika wake, Imarati kushambulia Qatar. Kuna waandishi waliosema kuwa mgogoro huu wa kuitenga Qatar unahusishwa na ‘Israel’. Kwa mfano ni nukuu ya CNBC kutoka kwa Jake Novak:

“Kijuu juu, ni sahihi kabisa kusema mfarakano huu wakufurahisha baina ya Saudi Arabia na Qatar ni kuhusiana na Iran kwani wasaudi wamelengwa na jinsi gani ya kupunguza nguvu na athari za Iran katika Masharaki ya Kati zinazo endelea kukua, lakini ukizama ndani kidogo, yanaonekana zaidi ya hayo, nayo ni kuwatenga waqatari katika wakati huu maalum kuna uhusiano na nchi nyengine: Israel” (Arabi 21, 7/6/2017)

Lakini kwa kufikiria na kudadisi kwa undani kila kitu kilichotokea, hukana mambo haya; si mageni, na Qatar imekuwa ikiyafanya kwa muda mrefu, wala hayakufanywa upya hivi sasa. Ukuruba wa Qatar kwa Iran unajulikana na uhusiano wake na Hamas ni maarufu pia. Zaidi ya hayo, athari ya mahusiano kati ya Qatar na serikali inayokaliwa na mayahudi ya Palestina na mahusiano kati ya nchi hizi na Saudi Arabia na Imarati pia hayakufichika, na hata mahusiano ya kikabila hayafikii kiwango hiki cha hali ya juu. Mambo haya yote yalikuweko kabla ya mgogoro na yatakuweko hata baada ya mgogoro; kwa hivyo, sizo sababu halisi.

Pili: sababu halisi, kama nilivyotangulia kutaja mwanzoni, ni Amerika au Trump na kutambua hili, tunarudia mambo yafuatayo:

1 – Tangu mwanzoni mwa karne hii, Qatar imekuwa “jiko” kuu la siasa za kiingereza katika eneo hili. Al-Jazeera imekuwa jukwaa kuu la habari kukatiza siasa ya Amerika na kushambulia vibaraka wa Amerika katika eneo hili. Jambo jengine ni pesa za kisiasa ambazo zimekuwa smaku kubwa ya kisiasa kuvutia nguvu za kisiasa. Kupitia vifaa hivi viwili, Qatar imepata mafanikio makubwa hususan katika harakati za kiislamu zinazotambuliwa kama za ‘kati na kati’ nchini Palestina, Misri, Libya, Tunisia na kwengineko, na Doha nchini Qatar imekuwa pepo ya viongozi wa harakati hizi na kitovu cha kupanga na kuharibu siasa na vibaraka wa Amerika. Na kama ilivyo tabia ya Uingereza kujifanya iko pamoja na Amerika huku ikitaka kuiharibia mambo yake, Qatar imeuelewa vyema mchezo wa Uingereza, na tangu 1991, iliikaribisha kambi ya kiamerika ya Al Udeib ambayo ndio makao makuu ya kitovu cha utoaji amri za kijeshi la Amerika (American Central Command) na ni kambi muhimu ya angani ambayo kwayo ndege za kiamerika hurukia kwenda kueneza mauaji na uharibifu miongoni mwa Waislamu Iraq, Afghanistan, Syria na Yemen. Huu ulikuwa wakati ambao Uingereza ilikuwa ikijenga “jiko” lake la kisiasa nchini Qatar mpaka lilipo malizika na kujitokeza katika mwanzo wa karne hii.

Kisha, jukumu la Qatar, kama mtumwa wa Uingereza, lilikuwa kwa ulaini kuambatana na mpango uliochorwa. Amerika ilikerwa na jukumu hili la Qatar kufikia nukta ya hasira zilizompelekea George W. Bush, mwana, kukadiria kukipiga bomu kituo cha Al-Jazeera kulingana na habari zilizo chapishwa na DW mnamo 22/11/2005:

(Gazeti la kiingereza “The Daily Mirror” mnamo Jumanne lilinukuu waraka wa ‘siri ya juu’ kwa afisi ya waziri mkuu wa Uingereza kutoka kwa raisi George W. Bush kwamba mnamo 2004 alifikiria kuyapiga bomu makao makuu ya kituo cha runinga ya setlaiti cha ‘Al-Jazeera’ nchini Qatar) (DW 22/11/2005). Huu ndio umekuwa msimamo wa eneo la Ghuba mpaka alipoingia mamlakani mfalme Salma wa Saudi Arabia.

Saudi Arabia imesimama na Amerika, na tangu hapo idara ya Obama iliamua kumuamini kibaraka wake Salman na jukumu muhimu katika eneo, nalo ni, upande mmoja, kuhitilafiana na jukumu la Qatar na kulitawala, na upande mwengine, kuambatana na mipango mipya ya kiamerika. Kwa hivyo, imelipa nguvu jukumu la vibaraka wa Amerika na imeuchukuwa utesi kati ya Saudi Arabia na Qatar kufikia hatua inayo hatarisha jukumu lote la Qatar. Na baada ya kuingia madarakani raisi mpya wa Amerika Donald Trump mapema mwaka huu, siasa ya Amerika imekuwa kali zaidi na isiyo pinda katika kukabiliana na kadhia nyingi za kimataifa, ikiwemo Qatar.

2 – Wakati wa ziara ya Trump jijini Riyadh mnamo 20-21/5/2017, aliwakusanya pambizoni mwake viongozi 50 Salman akiwa ubavuni mwake. Kwa kugusia ufadhili wa Qatar kwa ugaidi, Qatar ilitambua kupitia wadaku wa Kiingereza kuwa Amerika imeanza hatua kali za kulinyanyua jukumu la Saudi na kuvuruga jumuku la Qatar na Uingereza katika eneo la ghuba. Kujibu hatua hii, taarifa za Qatar zilitolewa siku mbili baada ya Amiri wa Qatar kurudi kutoka Riyadh.

Shirika la habari la Qatar lilinukuu taarifa za Amiri wa Qatar, Tamim Al-Thani, mnamo 23/5/2017: “Kile kinacho ianika Qatar kutokana na kampeni dhalimu ikisadifiana na ziara ya raisi wa Amerika katika eneo, inayo lenga kuihusisha (Qatar) na ugaidi… Tunashutumu tuhuma za  kufadhili ugaidi… hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kututuhumu ugaidi kwa sababu wame iorodhesha Ikhwan al-Muslimeen kama kundi la kigaidi.

Alitoa wito kwa Misri, Imarati na Bahrain kurudia upya msimamo wao dhidi ya Qatar… Kuna uhusiano imara na Amerika licha ya mambo yasiyo kuwa mazuri yalioko kwa sasa ya idara ya Amerika tukiwa na imani kuwa hali hii haitaendelea kwa sababu ya uchunguzi wa mahakama dhidi ya dosari na ukiukaji mipaka wa raisi wa Amerika, na kambi ya Al Ubeid inawakilisha himaya kwa Qatar kutokana na matarajio ya nchi jirani, lakini ndio fursa pekee ya Amerika kumiliki athari ya kijeshi katika eneo, na Qatar haijui ugaidi wala misimamo mikali, na ingependa kuchangia kupatikana uadilifu na amani kati ya Hamas, muwakilishi halali wa wapalestina, na Israel, kwa kuendeleza mawasiliano na pande zote.

Qatar imefaulu kujenga mahusiano imara kwa Amerika na Iran wakati huo huo kwa sababu Iran inawakilisha athari ya kieneo na ya kiislamu ambayo haipaswi kudharauliwa na si busara kuyakuuza mambo kwayo (athari). Taarifa hizi zaashiria kuwa Qatar inamtuhumu Trump kuwa nyuma ya kampeni dhidi ya Qatar ya kuituhumu kufadhili na kuunga mkono ugaidi. Taarifa hizi zilikuja pindi baada ya kongamano la Trump pamoja na wawakilishi wa serikali zilizoko katika ulimwengu wa kiislamu ambapo Trump alikuwa makini kuonyesha mafanikio yake katika kuziongoza serikali hizi kufikia malengo ya Amerika na utiifu kwa Amerika. Trump alisema katika kongamano hili kuwa, baadhi ya nchi, akikusudia Qatar, zinafadhili ugaidi. Kwa hivyo, taarifa za Qatar ni sawa na jibu kwa Trump kwa kuwa inataka kumzamisha na kutaraji kuwa atang’atuliwa mamlakani kutokana na uchunguzi wa mahakama dhidi yake.

3 – Mkusanyiko wa wafalme 55, maraisi na viongozi (wa ujinga na uharibifu) wa Ghuba na biladi za kiarabu na kiislamu huko Saudi Arabia, unawakilisha kujitolea kwa Saudi kufuata mpango wa Amerika wa kuonyesha uongozi wa Saudi eneo hili. Hii haikuwa ishara ya kimakosa kutoka Washington inayotaka kuviweka visima vya mafuta katika utumizi wake chini ya kisingizio cha tishio la Iran upande mmoja, na kuuzima moto wa athari ya Uingereza katika nchi za Ghuba kwa kuufanya uongozi wa Saudi ndio wenye kudhihiri na kuzifanya nchi za Ghuba zilizosalia kutembea nyuma ya Saudi Arabia, yaani, nyuma ya siasa ya kiamerika.

Hivyo basi, Saudi Arabia hainge weza kuvumilia wale wanaosimama dhidi ya uongozi wake katika eneo, na macho yake yalikuwa wazi kwa Qatar na ilikuwa inasubiri tu tukio litakalo itia Qatar motoni.

Kwa hivyo, ilikuwa mkali kwa taarifa za Qatar dhidi ya Saudi Arabia na Amerika zilizo chapishwa na shirika la habari la Qatar mnamo 23/5/2017. Licha ya kuomba radhi kwa Qatar, Saudi Arabia haikukubali maelezo ya Qatar, lakini ikaziona taarifa hizi kama thibitisho la kukataa kwa Qatar siasa ya kisaudi na jukumu la Amerika ililompa Salman, ndipo mgogoro ukaanza. Saudi Arabia ilijitoa kimasomaso na kutangaza kukata mahusiano na Qatar, ilionyesha ukali dhidi ya Qatar kwa kusimama dhidi ya uongozi wa Saudi katika Ghuba, huu ni mmuliko wa misimamo imara ya idara ya Trump. Hatua za Saudi Arabia zilikuwa kali dhidi ya Qatar na zilikuwa zimepita mpaka mnamo 05/03/2014 ilipo muondoa balozi wake kutoka Qatar, iliyo onekana kama kuzingirwa kwa Qatar. Kuwa na athari kubwa na kufuata njia ya Amerika, zikaja hatua za kisaudi za kushtua; waqatari walipewa masaa 48 pekee kuondoka nchini humo.

Kwa kukubalina na njia ya ushtuaji ya kiamerika, sambamba na mienendo ya Saudi na kwa kusadifiana nayo, Misri iliirudisha ndege ya abiria ya Qatar na kutoiruhusu kuingia eneo lake pasi na kutoa ilani mwanzoni na ndivyo zilivyo fanya nchi nyenginezo washirika wa Saudi dhidi ya Qatar.

Inaoneka kana kwamba Qatar ilishtuliwa na maamuzi haya ya kuisusia wala haikuyatarajia. Waziri wa kigeni wa Qatar, Mohammed Bin Abdulrahman Al-Thani, alisema katika mahojiano na BBC mnamo 6/6/2017 kuwa “Hatua zilizochukuliwa dhidi ya nchi hii ni za kushtua, na kilichotokea ni “Adhabu ya kijumla ya nchi tatu katika eneo hili ambazo zimejaribu kulazimisha ususiaji wa Qatar na watu wake…”

Qatar haipaswi kuonekana kama kakamavu katika kuikabili Amerika au vibaraka wake, kama Saudi Arabia, isipokuwa kuwe na nchi kubwa inayoisaidia na kusimama nyuma yake kufanya hilo, ambayo bila shaka ni Uingereza, ambayo Qatar inafuata siasa yake kwa siri, bali hata dhahiri! Lengo la Uingereza ni kuiharibia Amerika na kuvuruga mipango yake ya kumakinisha athari yake katika eneo, haswa eneo la Ghuba, na kwa hivyo iliwaagiza vibaraka wake ndani ya Qatar kufanya hivyo. Uingereza haikutarajia matokea yake kuwa ya kushtua kana kwamba ilikuwa inatarajia kuondolewa kwa mabalozi kama mnamo 2014, na mambo yamalizike pasi na natija kubwa, haswa kule kuwa Qatar yatumia kuwepo kwa kambi kubwa ya kiamerika humo kama himaya. Na kwa hivyo ilinukuliwa katika taarifa za Amiri wa Qatar zilizo chapishwa na shirika la habari la Qatar mnamo 23/05/2017, ambapo ilizifuta baadaye na kudai kuwa tovuti yake ilivamiwa: “Kambi ya Al Udeid inawakilisha himaya kwa Qatar kutokana na matarajio ya nchi jirani, lakini ndio fursa pekee ya Amerika kumiliki athari ya kijeshi katika eneo.” Hili ndilo Qatar inalotegema kuinyamazisha Amerika, huku ikivuruga na kuingilia dhidi ya Amerika na vibaraka wake katika eneo kupitia kituo chake cha Al Jazeera. Iliipa Amerika kambi kubwa zaidi katika eneo, na hivyo basi ikashangazwa na vitendo hivi vya kikatili.

4 – kwa hivyo, sababu halisi ya mgogoro huu ni jukumu jipya la Salman lililochorwa na Trump; kuwa kiongozi wa eneo la Ghuba, kutabikisha siasa ya Amerika, na kumzuia yeyote katika vibaraka wa Uingereza kuiingilia au kuivuruga, na kwa kuwa Qatar ndio iliochanguliwa na Uingereza kutekeleza jukumu la Uingereza la kuingilia na kuvuruga mipango ya Amerika katika eneo hili na kutabikisha mipango ya Uingereza, hatua ya ukali isiyokuwa ya kawaida ilichukuliwa dhidi ya Qatar. Amerika ndio dereva nyuma ya Salman katika mgogoro huu wala haikuficha hili, lakini ilikuwa ikijifichua pole pole kuwepo nyuma ya yale yaliyotokea na yanayo endelea kutokea:

Mtandao wa Al-Arabiya uliripoti mnamo 6/6/2017 taarifa ya afisa wa ngazi ya juu katika idara ya Amerika kwa shirika la habari la Reuters: “Kiwango kikubwa cha tabia ya Qatar kina ogopesha sio tu majirani zetu wa Ghuba bali Amerika vile vile”. Afisa wa ngazi ya juu katika idara ya Amerika aliliambia shirika la habari la Reuters mnamo Jumatatu kuwa Amerika haitaki kuona ‘mfarakano wa kudumu’ baina ya nchi za Ghuba, baada ya nchi kadhaa za Ghuba na za kiarabu kuamua kukata mahusiano na Qatar mnamo Jumatatu kutokana na madai ya kusaidia makundi yenye misimamo mikali na Iran, afisa huyu aliongeza kusema: “Twataka kuwaleta katika muelekeo wa sawa.”

– Shirika la BBC liliripoti mnamo 6/6/2017: (Raisi wa Amerika Donald Trump alidokeza athari ya ziara yake ya Ghuba ya hivi karibuni juu ya uamuzi wa kukata mahusiano na Qatar, na Trump akasema alipokea habari wakati wa ziara yake kuwa Doha inafadhili harakati za “ki mfumo zilizo na misimamo mikali.”

“Wakati wa ziara yangu ya hivi karibuni Mashariki ya Kati, nilieleza kwamba kamwe hakuwezi kuwepo tena ufadhili wa mfumo ulio na msimamo mkali. Viongozi wakainyoshea kidole Qatar – tamaza!” akaandika.

“Ni vizuri sana kuiona ziara ya Saudi Arabia huku mfalme wake na nchi 50 tayari zikilipa. Walisema watachukua hatua ngumu dhidi ya ufadhili wa misimamo mikali, na maregeleo yote yalikuwa yanaelekea kwa Qatar. Pengine huu utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa tishio la ugaidi!” baadaye akaendelea.

Taarifa za Trump mnamo 9/6/2017 zinafichua na kuthibitisha kuwa Amerika iko nyuma ya mshawasha wa Saudi:

(Raisi wa Amerika Donald Trump mnamo Ijumaa alisema kuwa Qatar isimamishe kufadhili ugaidi haraka iwezekenavyo na alitaraji kuwa kongamano la Riyadh litakuwa ni mwanzo wa kumalizika kwa ugaidi. “Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Romania ikuluni white house alisema, kwamba Qatar kihistoria imekuwa ni nchi inayo fadhili ugaidi.” (Sky News Arabia, 9/6/2017)

Donald Trump alisema: “…wahusika wakuu katika eneo la Ghuba wamekubaliana kusitisha ufadhili wa ugaidi, ima kifedha, kijeshi au hata kimaadili. Taifa la Qatar kwa bahati mbaya, kihistoria limekuwa mfadhili wa ugaidi kwa kiwango kikubwa. Na kwa kutokea kwa kongamano hilo, mataifa yalikuja pamoja na kusema nami kuhusu kuikabili Qatar juu ya tabia yake hii.”

(Kwa hivyo tulikuwa na uamuzi wa kufanya: Je, tufuate barabara sahali au hatimaye tuchukue kitendo kigumu lakini kinachostahili? Lazima tukomeshe ufadhili wa ugaidi. Nimeamua pamoja na waziri wa kigeni Rex Tillerson, magenerali wetu wakuu na wanajeshi, wakati umewadia kutoa wito kwa Qatar to kukomesha ufadhili wake…)(Al-Youm As-Sabi’,9/6/2017)

5 – Ama kuhusu ni wapi mgogoro huu wa Qatar unapo elekea, Qatar imepigwa na butwaa na misimamo hii migumu kutoka kwa vibaraka wa Amerika, Saudi Arabia na Misri ambao vibaraka wa Uingereza kama, Imarati, Bahrain na wengineo, wamefuata katika ile mbinu ya Uingereza ya kugawanya majukumu kama tulivyotaja katika jibu la swali tulilotoa mnamo 9/4/2017 ambapo tulisema: (… Kwa hivyo ni wazi kuwa Uingereza inagawanya majukumu ya vibaraka wake kwa njia inayoonekana kugongana, lakini mwishowe hufikia lengo la Uingereza; haiwaweki vibaraka wote katika upande mmoja, haswa katika nchi ambazo kuna karata kadhaa). Qatar, kama tulivyo sema, haikutarajia mgogoro huu kukua kwa nguvu na ukali. Hatua za Saudi zilishtua; mabalozi wa Qatar walipewa masaa 48 kuondoka nchini mwake. Kwa kukubaliana na mbinu ya kiamerika ya kutia mshtuko na kwenda sambamba na hatua za Saudi, Misri ilizirudisha ndege za abiria za Qatar na ikazikataza kuingia eneo lake kabla ya kuzipa ilani mwanzo, na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa nchi nyenginezo washirika wa Saudi Arabia dhidi ya Qatar.

6 – Je, hili litapelekea kujiondoa au kufurushwa kwa Qatar katika jumuia ya Ghuba? Inawezekana kama hatua ya mwisho, lakini inatarajiwa sana kuwepo na uwezekano wa kutatua mgogoro huu. Dola mashuhuri za kiulimwengu kama Amerika na Uingereza, zote zina hamu Qatar ibakie katika jumuia ya Ghuba kwa malengo tofauti tofauti ambayo kila mmoja anayataka.

Kwa Amerika, inataka Qatar, kama ilivyotajwa juu, kuwa chini ya uongozi wa Saudi Arabia; yaani, kutekeleza maslahi ya Amerika bila ya kuingilia au kuvuruga kwa sababu tofauti tofauti. Amerika inataka kambi yake iwe imara na kutekeleza majukumu yake bila ya kukatizwa. Inatambua kuwa Uingereza iko nyuma ya Qatar, na kwa kupitia mbinu zake za kijanja, inaweza kuiletea kambi yake matatizo mengi ikiwa Qatar itajiondoa katika jumuia ya Ghuba. Hivyo basi, Amerika inaitaka Qatar kutabikisha mipango yake na kuwa sehemu ya muelekeo wa Saudi na wakati huo huo kubakia katika jumuia ya Qatar.

Uingereza nayo inataka kuibakisha Qatar katika jumuia ya Ghuba kwa sababu, ndani ya jumuia hii, inaweza kufanya kazi nyuma ya pazia yake kutabikisha mipango ya Uingereza kulingana na muelekeo wa Uingereza ambayo ina sura mbili; inaonyesha urafiki upande wa mbele, na kudunga kisu upande wa nyuma. Kwa hivyo, kile kinacho tarajiwa kama tulivyotaja juu ni suluhisho litakalo zunguka katika kuzuia hatima ya kuraruka kati ya Qatar na jumuia ya Ghuba isipokuwa labda hii itokee kama “hatua ya mwisho”, lakini kamwe hili halitarajiwi haswa kwa mustakbali wa karibuni kwa sababu zifuatazo:

A – Hotuba ya Trump mnamo 9/6/2017 iliyotajwa juu haikuacha nafasi kwa Qatar kulegeza msimamo kwa sababu alilizungumzia hilo:

“Taifa la Qatar kwa bahati mbaya, kihistoria limekuwa mfadhili wa ugaidi kwa kiwango kikubwa. Na kwa kutokea kwa kongamano hilo, mataifa yalikuja pamoja na kusema nami kuhusu kuikabili Qatar juu ya tabia yake hii. Kwa hivyo tulikuwa na uamuzi wa kufanya: Je, tufuate barabara sahali au hatimaye tuchukue kitendo kigumu lakini kinacho stahili? Lazima tukomeshe ufadhili wa ugaidi. Nimeamua pamoja na waziri wa kigeni Rex Tillerson, magenerali wetu wakuu na wanajeshi, wakati umewadia kutoa wito kwa Qatar to kukomesha ufadhili wake…”                  (Al-Youm As-Sabi’,9/6/2017)

Inajulikana kuwa Qatar haitungi siasa zake yenyewe, bali Uingereza huitungia, na siasa ya sasa ya Uingereza haikabiliana na Amerika hadharani, haswa katika hatua ya sasa ambayo ni hatua ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya; inajaribu kuwa karibu nayo hata juu ya sakafu.

B – Mawazo ya Trump ni kama ya mfanyi biashara, upande wa kifedha ndio ulio na athari zaidi. Ikiwa Qatar italipa kinachomvutia Trump, huenda akamuagiza Salman kulegeza msimamo! Mtafiti wa kiamerika Jonathan Kristol mshirika katika Taasisi ya Siasa ya Kiulimwengu (World Policy Institute), alisema: “Pesa alizonazo Donald Trump ndani ya ikulu ya white house ndio ufunguo wa mgogoro wa kukatwa kwa Qatar na Saudi, Imarati na Bahrain”, alifafanua katika makala yake kuwa njia pekee kwa Qatar kushinda shinikizo la kidiplomasia na la kiuchumi la Saudi ni kupitia Amerika kuingilia kati pamoja na vibaraka wake wa kisaudi kwa njia ya pesa, kulingana na CNN…” (Arabi 21, 6/6/2017).

Yaani, mtazamo unaotarajiwa zaidi ni kuwa kuna suluhisho kupitia pesa za Qatar au kujisalimisha kwa Qatar! Na twasema kuwa kinacho tarajiwa zaidi ni kuwa Uingereza itakapo amini kuwa maslahi yake wakati wowote yanahitaji kujiondoa kwa Qatar kutoka kwa jumuia (ya Ghuba),  itajiondoa, na ikiwa yanahitaji kubakia kwake, itabakia kwa sababu Qatar haiendeshi siasa yake wenyewe, lakini Uingereza ndio yenye kuendesha!

7 – Kutamatisha, hakuna kheri yoyote inayotarajiwa kutoka kwa vibaraka wa Amerika nchini Saudi Arabia, Misri na wale waliowafuata katika kadhia hii ya kukata mahusiano; wamezisalimisha biladi za kiislamu na watu wake kwa maadui wa Uislamu na Waislamu kwa badali ya kubakisha viti vyao vya utawala, vyenye miguu mibovu ambayo leo au kesho yaweza kuvunjika. Zaidi ya hayo, hakuna kheri yoyote inayo tarajiwa kutoka kwa Qatar inayo endeshwa nyuma ya Uingereza kupewa miradi ya uharibifu dhidi ya Waislamu; imeipatia Amerika kambi kubwa zaidi ambayo ndege zake hurukia kwenda kuua na kuangamiza watoto wa Waislamu Syria na Iraq na kuharibu majumba yao. Pia inaunga mkono kuhifadhi amani na dola ya kiyahudi; imeifanya Hamas kulegeza msimamo kwa kuiga Fatah katika kuweka miungano. Zaidi ya hayo, imeziathiri baadhi ya harakati za Syria kwa pesa zake za sumu kwa kuzishurutisha kuingia katika majadiliano na serikali ya kihalifu huko. Inawahadaa wale walio na mitazamo ya kiislamu na kuwaghuri kwa pesa na makao ili kuwavutia kulegeza msimamo na kubadilisha mielekeo na fikra zao. Yote haya ni katika jukumu lake ovu ililochorewa na Uingereza. Kwa hivyo ni uchali na karibu na uhaini kuihurumia serikali hii au nyengineyo kwa kisingizo cha (qaida ya) ‘la khafifu katika madhara mawili’; kadhia za umma hazipimwi katika mizani ya madhara na madhara khafifu, bali hupimwa kwa mizani ya haki na batil. Watoto wa umma lazima wapinge serikali hizi zinazofanya khiana kwa Allah (swt), Mtume wake (saw) na kwa waumini, na hawana budi kufanya kazi na wafanyi kazi mukhlisina kuzing’oa na kuasisi dola yao; bishara ya Mtume wao mtukufu (saw); Khilafah Rashidah itakayo simamia mambo yao katika usalama na amani majumbani mwao, njiani na safarini mwao, itakayo leta izza kwa Uislamu na Waislamu na itakayo dhalilisha makafiri wakoloni, na hapo ndipo Trump na wapambe wake na vibaraka wake watakapo fikwa na janga miilini mwao na majumbani mwao.

وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Na Allah ni Mshindi juu ya jambo lake lakini wengi watu hawajui” [Yusuf: 21]

16 Ramadhan 1438 AH
11/6/2017 CE

 

Maoni hayajaruhusiwa.