22 Ramadhan

بسم الله الرحمن الرحيم

Siku kama hii 22 Ramadhan mwaka wa 273Hijria Imam Ibn Majah alifariki dunia akiwa na miaka 64.

Imam Ibn Majah ni mwanachuoni maarufu katika fani ya Hadithi ambaye alifanya kazi kubwa ya kukusanya Haditihi katika kitabu chake cha Sunan Ibn Majah.

Jina la Ibn Majah kwa ukamilifu ni Abū ‘Abdullāh Muḥammad ibn Yazīd ibn ‘Abdullāh al-Rab‘ī al-Qazvīnī alizaliwa mwaka 209 Hijiria akitokana na asili ya Kifursi (Iran).

Kitabu chake cha Sunan Ibn Majah, kinahesabika kuwa ni kati ya vitabu sita mashuhuri vya Hadithi (al-Kutub al-Sittah). Kitabu hicho kina Hadithi 4341 ndani ya mijalada (volumes) 37.

22 Ramadhan 1441 Hijri – 15 Mei 2020 M

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.