Kukithirisha Dua Kwa Ajili Ya Ndugu Zetu Mahabusu Katika Masiku Matukufu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni miaka miwili na nusu sasa tangu wanachama watatu wa Hizb ut Tahrir Tanzania: Ustadh Ramadhan Moshi (41), Waziri Suleiman (33) na Omar Salum Bumbo (51 ) kunyakuliwa kisha kubambikiziwa mashtaka ya uongo yanayotokana na sheria ya kikoloni na ya kibaguzi ya ‘ugaidi”.

Kwa kipindi chote hicho, wakati ndugu zetu hao wakiwa mahabusu, licha ya kuwa mbali na familia zao, ndugu, marafiki na kusita kwa shughuli zao za uzalishaji, pia wamerundikwa katika mahabusu zenye mazingira duni kibinadamu na kesi yao imekuwa ikitajwa tu kila wiki mbili, bila ya kuanza kusikilizwa, kwa kisingizio cha kutokamilika ukusanyaji wa ushahidi ati kwa mwaka mzima!

Tunamuomba Allah Taala katika masiku haya matukufu awatoe ndugu zetu hawa katika mikono ya dhulma na uonevu.
Tunamuomba Taala kwa utukufu na nguvu zake awakomboe Waislamu wote waliodhulumiwa hapa Tanzania wakiwemo ndugu zetu wa Jumuiya ya Uamsho na wengineo mashariki na magharibi.

Aidha, tunamuomba Allah SW awakomboe pia wasiokuwa Waislamu wanaonyimwa haki zao na kutendewa dhulma bila ya hatia.

Mwisho, tunamuomba Allah Taala awaangamize kwa maangamizo makubwa maadui wa Uislamu na Waislamu, na wale wote wanaodhulumu wanadamu kwa jumla.

Amiin

23 Ramadhan 1441 Hijria -16 Mei 2020 M

Maoni hayajaruhusiwa.