Udhalilishaji wa Kijinsia ni Matokeo ya Mfumo Mchafu wa Kibepari
Unyanyasaji na mateso dhidi ya wanawake na watoto umekuwa ni tatizo sugu na lililoenea karibu nchi zote duniani. Vyombo vya habari vya ndani na nje vimekuwa vikiripoti kila leo juu ya taarifa za dhulma hii kubwa.
Juu ya kuwepo kwa kile kinachoitwa juhudi za kupunguza tatizo hilo, zikiwemo uundwaji wa madawati ya kijinsia, kuundwa sheria kali, kuwepo idara za wanawake na watoto nk., bado jinamizi hili linaendelea kuiandama jamii. Uhuru wa wanawake na haki za watoto imekuwa ni kauli mbiu za kuonyesha kuwa tawala katika nchi zinajali na kuchukuwa hatua dhidi ya hili tatizo.
Mtafaruku wa janga hili ni matokeo yasiyoepukika ambayo zaidi hukuzwa na fikra za kisekula na ‘fikra huria’ (liberal concepts) zilizobuniwa na wanaadamu na kubebwa na mfumo wa kibepari wa kimagharibi. Mfumo ambao huweka suala la maslahi na starehe kuwa ndio malengo makuu na kipaumbele cha maisha ya mwanaadamu. Juu ya msingi huo, fikra kama ya ‘usawa wa kijinsia’ imetumika kubomoa maadili bora ya kijamii yaliyokuwapo hasa katika jamii za Kiislamu. Mahusiano machafu kupitia dhana ya ‘uhuru’ na kukimbilia matamanio na uchoyo wa nafsi yamedumaza mambo yote yenye kujenga heshima, utu na hadhi ya mwanamke, watoto na jamii kwa ujumla.
Kwa mujibu wa jarida la Huffington Post la April 5, 2017, katika Marekani, nchi inayojigamba kuwa ni mlinzi mkuu wa haki za binaadamu na wanawake, takriban wanawake milioni 18 wamekuwa wahanga wa kubakwa tokea mwaka 1998. Kwa kila siku zaidi ya watu 570 wanakumbwa na mashambulizi ya kijinsia katika nchi hiyo.
Kiulimwengu, kwa mujibu wa World Report, kati ya wastani wa watu 800,000 wanaotoroshwa kimagendo kupitia mipakani kila mwaka, asilimia 70 (70%) hutoroshwa kwa ajili ya ngono, na hufanyika kwa wasichana wenye umri wa chini ya miaka 16. Kwa mujibu wa takwimu, karibu katika kila nchi udhalilishaji wa kijinsia umekuwa ukipanda kwa kasi.
Haya yote hujitokeza chini ya mfumo huu ‘huria’ wa kisekula wa kibepari ambao leo umetawala kitaifa na kimataifa. Ni matokeo ya mfumo wa kibepari usioweza kushughulikia ipasavyo na masuala nyeti ya ubinadamu. Hivyo, mfumo wa ubepari kwa kutaka kujificha mgongo wazi na kujihakikishia kudumu kwake umekuwa daima ukifunika uoza unaoikumba jamii yao, na wakati huo huo kukashifu na kubomoa thaqafa/utamaduni na muundo wa nidhamu ya kijamii ya Kiislamu.
Matokeo yake hushuhudiwa kuongezeka unyanyasaji, vurugu na mparaganyiko katika jamii hasa katika ngazi ya familia, ambapo hayo huwa ni matokeo ya mpango kabambe iliyopangwa. Mpango huo hulenga kutawala ardhi za Waislamu na kutekeleza nidhamu ya hukmu ya kisekula- isiyomtambua Mungu Muumba ambayo huvuruga misingi thabiti ya kijamii nk.
Mkakati wa makafiri kutuwekea vyombo kama taasisi na jumuiya za wanawake za kudai haki sawa, watetezi wa haki za wanawake na watoto, mashirika ya haki za binaadamu, yote ni mipango ya makafiri wakoloni dhidi ya maadili mema.
Natija ya harakati hizo ndio kama leo ambapo suala la ndoa huwekewa vipingamizi, kama kucheleweshwa wanawake kuolewa kwa kisingizio cha masomo nk. Imekuwa ni kosa katika taratibu za kisekula za kimagharibi tunazobebeshwa, kwa mwanamke aliyekwisha baleghe kuolewa kama hajamaliza shule, lakini huwa si kosa akifanya zinaa ilimradi hapati mimba.
Huu ndio mfumo batil na mchafu wa kibepari unaoeneza ufisadi katika ardhi. Mfumo unaotakiwa kutupiliwa mbali, na badala yake kuchukuwa mfumo bora wa Kiislamu.
Jamii ya Kiislamu iliyobeba thaqafah ya Kiislamu chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah ilikuwa ni ya kupigiwa mfano katika ulimwengu na kuirejesha tena jamii hiyo ni suala la kufa na kupona, kwani ndio itakayotufanya tuishi katika hali ya kuhifadhika, kumridhisha Allah Taala, Muumba wetu na kurejesha izza yetu kwa mara nyengine Inshaallah.
(Source: Violence against Women and Children —hizb-ut-tahrir.info)
Risala ya Wiki No. 19
22 Safar 1440 Hijri | 31-10- 2018 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania
https://hizb.or.tz/
https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania
Maoni hayajaruhusiwa.