Sisi Kama Waislamu Tuko Katika Hali Ngumu Tokea Kuanguka kwa Khilafah, Sio Tokea kwa Mripuko wa Virusi vya Korona!

بسم الله الرحمن الرحيم

[وَإِذَا مَسَّ الإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَآئِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَى ضُرٍّ مَّسَّهُ كَذَلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ]

“Na mtu akiguswa na shida hutuomba nae kaegesha ubavu, au kakaa au kasimama. Lakini tukimuondoshea shida yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondoshee shida iliyompata. Ndio namna hiyo wamepambiwa warukao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda” [Surah Yunus: 12]

Kuna watu wengi wanashughulishwa sana na kuvunjika moyo wanapopatwa na madhara, shida au magonjwa. Hivyo, huanza kuwa wachaji Mungu zaidi na kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) azuie na kuwaondolea maafa haya. Wanaomba, kutarajia na kutumaini kuwa maombi yao yatajibiwa. Lakini Mwenyezi Mungu (swt) anapoondoa matatizo yao na maafa, hugeuka na kuzama kwenye kiburi chao kama kwamba hakuna kilichotokea kwao na haraka husahau kipindi cha shida pia humsahau Mwenyezi Mungu (swt).

Bila shaka, ni jambo zuri na jema pindi Muislamu anapotaka msaada na hifadhi kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kutarajia kuwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndiye anaye weza kuleta faraja katika mambo yake. Hata hivyo, watu wasiombe kwa Mwenyezi Mungu wakati wa shida tu, bali wamkumbuke Yeye pia wakati mambo yao yanaendelea vizuri na hakuna chochote kilicho kosekana katika maisha yao. Zaidi ya hayo, Muislamu asitafsiri jambo kuwa ni zuri au baya katika tukio, bali atarajie “kheri” katika kila jambo na ajishughulishe juu ya namna ya kuamiliana nalo kwa mizani ya Kiislamu. Mtume (saw) amesema:

 «عَجَبًا (لِأَمْرِ) الْمُؤْمِنِ لَا يَقْضِي اللهُ لَهُ قَضَاءً إِلَّا كَانَ خَيْرًا لَهُ، إِنْ أَصَابَتْهُ ضَرَّاءُ فَصَبَرَ كَانَ خَيْرًا لَهُ، وَإِنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ فَشَكَرَ كَانَ خَيْرًا لَهُ، وَلَيْسَ ذَلِكَ لِأَحَدٍ إِلَّا لِلْمُؤْمِن»

“Ajabu ya jambo la muumini; kuna kheri kwake katika kila jambo na hili halipo kwa yeyote isipokuwa muumini. Akipata neema akashukuru kwa Mwenyezi Mungu, huwa ni kheri kwake. Na ikimfika dhara akasubiri huwa ni kheri kwake.”

Kama mtu atahusisha fahamu hiyo ilio elezwa hapo juu kwa tatizo la maambukizi ya Korona hivi leo, inadhihirika wazi kuwa watu wengi huhisi kujitolea kwao kwa Uislamu baada ya mripuko wa virusi hivi, na kutarajia zaidi sasa kuliko muda mwengine kwa ulinzi wa Mwenyezi Mungu (swt). Watu hawa hufikiri kuwa wako katika hali ngumu hivi sasa. Hisia hizi huzuka kwa sababu wao, muda huu, wameathiriwa BINAFSI kwa tukio. Hudhania kuwa maradhi haya ni “shari” kwao na hutafuta uokozi popote wanapo weza, hata humuomba Mwenyezi Mungu (swt) na hufikiri kuwa Mwenyezi Mungu (swt) hajui kilichomo ndani ya nyoyo zao.

Lakini swali muhimu ni Je, Waislamu kwa pamoja kama Ummah, hawakuvamiwa na kirusi kikubwa zaidi kabla ya mripuko wa kirusi cha Korona? Nacho ni Demokrasia na mipango yake ilio duni dhidi ya Uislamu? Je, haukuwa Ummah umevumilia maafa makubwa tokea Khilafah ya Uislamu ilipo vunjwa? Je, haukuwa Ummah ni wenye kuteseka kila siku katika nchi zilizo vamiwa? Je, haukuwa Ummah ukihofu mabomu na makombora ya maadui wa Uislamu? Je, haukuwa Ummah katika matatizo ya kutekeleza Uislamu duniani kote? Hawakuwa ni wenye kuwekwa magerezani ili kuachana na imani zao? Je, maelefu ya Waislam hawakuwa ni wenye kufa kwa njaa kila siku? Je, wanawake wa Kiislamu hawakuwa wakinajisiwa na kuteswa?

Hivyo, je, Muislamu anapaswa kufikiria kuwa yuko katika hali ngumu hivi sasa baada ya mripuko wa Virusi vya Korona au anapaswa kufikiria kuwa Waislamu kama Ummah wako katika hali ngumu kwa muda mrefu? Hii ina maana kuwa mripuko wa virusi vya Korona haupaswi kuwashtua Waislamu katika mtazamo wa matatizo ya kimaisha. Wasiufadhilishe Uislamu pekee wakati wanapo athiriwa binafsi kwa tatizo; wawe siku zote na ufahamu kuwa hivi leo Ummah kwa pamoja uko katika hali ngumu kwa kuwa hauna tena Dola na mlinzi.

Hata hivyo, hisia hizi zisiwe za hamasa tu na za kipindi kifupi wakati wa maambukizi ya virusi vya Korona; ziwepo muda wote na muumini muda wote ajitahidi kwa ajili ya Uislamu na Ummah wake na sio tu kwa ajili ya utulivu wa nafsi yake.

Lakini jambo la kufurahisha ni kuwa Mwenyezi Mungu (swt) Ndiye anaye samehe zaidi ya matarajio, anakubali toba na kusamehe makosa yetu. Yeye ndiye anaye yafinika madhambi yetu na kutuhifadhi kutokana na athari zake, hivyo tunaweza kuendelea kutubu bila ya kuona aibu wala kusutwa na nafsi. Hata kama madhambi ni mengi au makubwa kiasi gani, Al-Ghafuur huyafinika. Hivyo, hatujachelewa na kila Muislamu anaweza kutubu, kujitolea kwa ikhlasi kwa Uislamu na asiwe na hofu kila siku ya maisha yake mafupi kuhusu virusi hivi vipya, bali ahofu kuhusu mazingira machungu ya Ummah wake. Anaweza kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume na kukamilisha jukumu lake kwa Ummah wake.

“Lengo la Hizb ut Tahrir ni kuregesha maisha ya Kiislamu na kubeba da’wah ya Uislamu, yaani kufanikisha lengo la kutatua kadhia nyeti inayowahusu Waislamu. Kuregesha maisha ya Kiislamu humaanisha kuwaregesha Waislamu kuishi Kiislamu katika ardhi ya Uislamu na katika mujtamaa wa Kiislamu, ambapo fikra za Kiislamu na hamasa za Kiislamu zinatawala, na ambapo nidhamu na sheria za Kiislamu zinatekelezwa. Hivyo, masuala yote ya kijamii yataendeshwa kulingana na sheria za Mwenyezi Mungu (swt), na mtazamo unao tawala katika mujtamaa utakuwa ni Halali na Haramu. Haya yatakuwa chini ya kivuli cha Dola ya Kiislamu ambayo ni Khilafah ambapo Waislamu watamchagua Khalifah na kumpa bay’ah kwa kusikiliza na kumtii juu ya sharti la kuwa atawaongoza kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake, na juu ya sharti la kuwa ataubeba Uislamu kama risala kwa ulimwengu kupitia ulinganizi na Jihad. Chama hiki kinalenga kuamsha Ummah kwa njia sahihi kupitia fikra angavu ambayo imechukuliwa kutoka katika Itikadi ya Kiislamu. kinataka kuuregesha Ummah wa Kiislamu kwenye utukufu na izzah yake ya awali, ili uweze kuchukua nafasi ya uongozi kutoka kwa dola, mataifa na watu wengine, na kuregea katika nafasi ya kuwa dola nambari moja ulimwenguni, kama ilivyo kuwa nyuma ambapo ilisimamia ulimwengu na kuchunga mambo yao kwa mujibu wa sheria za Uislamu. (Njia ya Hizb ut Tahrir ya Kuleta Mabadiliko)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na Amanah Abed

 #Covid19           #Korona           #كورونا      

Maoni hayajaruhusiwa.