Mwezi Mtukufu Utuhamasishe Waislamu Kulinda na Kutetea Matukufu Yetu

0

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunatoa pongezi za dhati kwa Ummah wa Kiiislamu Tanzania na ulimwengu mzima kwa kuanza mwezi wa Ramadhan. Mwezi wa baraka, maghfira na wa kuchwa huru na moto wa Jahannam.

Ummah wa Kiislamu Mashariki na Magharibi wanaukaribisha na kuupokea kwa mapenzi makubwa mwezi huu wa Ramadhani kutokana na hadhi na utukufu wake. Hivyo basi, pia ni jambo la wajibu ndani ya mwezi huu kuukumbusha Ummah wetu jukumu la kufanya kazi ya daawa (ulinganizi) bila ya kuchoka ili tuweze kwa ukamilifu wake kulinda, kutetea na kuadhimisha matukufu yetu. Miongoni mwa matukufu hayo ni yafuatao:

  1. Maisha, hadhi na heshima ya Waislamu.

Leo tunashuhudia kiulimwengu namna Waislamu wanavyodhulumiwa, kudhalilishwa, kuuliwa, kuteswa

nk.Umwagaji damu wa karibuni zaidi ni ule uliotendwa  siku chache zilizopita na kijidola cha Mayahudi

kwa kuwaua bila ya hatia Waislamu (mashahid) zaidi ya 50, katika harakati za kutetea ardhi ya

Waislamu kufuatia hatua ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem. Zaidi ya hayo, damu

ya Waislamu inamwagwa kila dakika ndani ya Syria, Yemen,Iraq, Afghanistan, Burma, Jamhuri ya

Afrika ya Kati, Somalia nk. Bila ya kusahau ukatili na madhila makubwa ya Waislamu ndani ya mikono

ya makafiri na vibaraka wao (katika majela yao), pia ubakaji na kuvunjiwa heshima  wanawake wa

Kiislamu na vizee, mambo yanayotendeka kila mahala.

  1. Utukufu wa kitabu cha Quran.

Kuinusuru na kuilinda Quran Tukufu kwanza ni kuhifadhi hadhi yake, lakini pia kwa kuipa haki ya kuteremshwa kwake, nayo ni muongozo wa kila kipengele cha maisha ya mwanadamu. Quran ni tukufu, iliteremshwa ndani ya mwezi huu mtukufu na kwa Umma mtukufu. Hivyo,ni jambo lisiloingia akilini akilini kuadhimisha utukufu wa Ramadhani bila ya kuadhimisha utukufu wa Quran, kwa kuwa tumeuipata mwezi wa Ramadhan kutokana  na Quran.

  1. Hadhi na utukufu wa Mtume (saaw).

Leo kuna kampeni ovu ya kiulimwengu ya kumdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume (saaw) kwa kisingizio cha ‘uhuru wa maoni’. Makafiri bila ya aibu wala haya wanaekeza kwa jitihada kubwa katika kuufanikisha uovu huo, kiasi cha hata kudiriki kuwashawishi Waislamu ati wakubali kubeba fikra kuwa kumkashifu Mtume (saaw) kuwa ni jambo la kawaida. Mtume (saaw) mwenye mapenzi na huruma kubwa kwa Ummah wake, basi ni wajibu juu ya Umma wetu nao kuonesha mapenzi na huruma zaidi kwake.

  1. Misikiti Mitakatifu

Fiqhi ya Kiislamu imeweka bayana juu ya Misikiti Mitakatifu (Haram), ambayo ni mitatu, kwa masikitiko makubwa kwa Haramu zote tatu, Waislamu hawana fursa kwa ukamilifu kuitumia Misikiti hiyo kwa ibada ipasavyo. Misikiti miwili Mitukufu ya Masjid Haram wa Makka na Masjid Nabawi wa Madina imo ndani ya mikono ya watawala vibaraka ambao wanaitumia Misikiti hiyo  kama duka lao la kifamilia kujipatia faida, ilhali Masjid Al-Aqswa umo katika mikono ya wavamizi waliolaaniwa, kijidola cha Mayahudi cha “Israel”. Basi mwezi wa Ramadhani utuhamasishe  zaidi na zaidi kuzikomboa Haram zote tatu.

Kuweza kulinda, kuhifadhi na kutetea matukufu yetu kwa ukamilifu kunahitaji iwepo nguvu na mamlaka ya dola ya Kiislamu ya Khilafah, dola hiyo ndio nguzo na ngao ambayo Waislamu watakuwa nyuma yake katika kuyachunga na kuyasimamia mambo yote. Basi mwezi huu mtukufu wa Ramadhani utuhamasishe kufanya kazi kwa ajili ya suluhisho hilo.

ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ عِنْدَ رَبِّهِ

“Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi”

 [Al-Hajj: 30]

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.