Muanguko wa Utawala wa Kisekula Umekaribia Mno Kuanguka na kwa Dhulma yake Dhidi ya Wanawake!

Kufuatia mazungumzo yaliyofanywa na kitengo cha wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia mnamo siku ya jumapili, kilichofanyika 8/12/ 2019 katika manispaa ya Al-Morouj, ambapo Ustadhat Zainab Al-Dajbi aliwasilisha mada iliyojulikana kwa jina la “Shinikizo la nchi za kiimla za kimagharibi kupitia mashirika ya kijamii”, mtu aliejitambulisha kama mwanausalama, alifika katika nyumba ya wazazi wake, ameolewa na ni mama pia anaishi katika makazi yake, mwana uslama huyo alimuagiza baba yake kwamba ustadhat anatafutwa na kikosi cha wanausalama kwaajili ya uchunguzi na upekuzi.

Ili kumshinikiza zaidi walimchukua kaka yake ili kumfanya ustadhat aende haraka badala ya kumuuita kwa njia za kisheria, lakini baada ya ufatiliaji mkubwa kaka yake aliachiwa.

Lakini pia mwanasheria wake aliwapigia simu siku nzima hawakupokea, tarehe 11/12/2019 kwa muda tofauti tofauti, simu iliita kati ya 5:45 asubuhi hadi saa kumi jioni, mpaka pale alipopokea ujumbe maalum kwamba anahitajika. Wakatumia dharura kwa kusema kwamba kiongozi wao hayupo, na kwanini wamechelewa kujibu wito hadi muda wa jioni.

Kufuatia kuchelewa huko walikubaliana kupanga siku nyingine ya kukutana ambayo ni jumatano, 12/12/2019, lakini pia walichelewa na kufika saa kumi na moja jioni wakati ambapo mahakama haifanyi tena kazi na watu wa ulinzi haukuweza kunyanyua sauti zao kulalamika kwa mwendesha mashtaka.

Hivyo basi, sisi kitengo cha wanawake cha ofisi ya habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia:
Tunachukulia kwamba haya yote yanatokea kwasababu Zainab Al-Dajbi anauhusiano na Hizb ut Tahrir ambacho ni chama kinachofata mlengwa wa kiudalifu wa kisiasa, ukizingatia maadhui ya mada yake.

– Tunahitaji kuonyesha kwa ummah kwamba yanayomkuta Ustadha Zainab Al-Dajabi ni kumtafutia tuhuma za kisiasa kwa kuzitumia taasisi kama vile usalama na mahakama ili kuendeleza vita vilivyotengenezwa na mawakala wa kimagharibi dhidi ya watu waaminifu kwa nchi zao.

– Tunawakumbusha mawakala wa kimagharibi ambao maslahi yao yameguswa katika mazungumzo ya Ustadha Zainab Al-Dajabi mwanachama wa Hizb ut Tahrir, kwamba udhalilishaji wa mwanamke sio katika tabia za wanaume.

– Tunawakumbusha maadui wa nchi wanaotishia kuwafunga watu na kuwakamata na aina nyingine kama hizo kwamba haziwezi kumvunja moyo Ustadha Zainab wala mwanachma yoyote wa Hizb ut Tahrir kuacha kusongesha mwito wa usimamishaji wa Khilafah (Caliphate) kwa kufata njia ya utume.

– Tuna mjulisha kila mtu kwamba sisi, kitengo cha wakinamama wa Hizb ut Tahrir, hatutishwi na kitisho chochote kitachotuzuia kuacha mwito wa kusimamisha faradhi.

– Mbinu hizi za kidikteta kutoka katika mfumo unaojiita wa kidemocrasia, unajinadi kudhamini uhuru, tunazichukulia ni kama mbinu za watu na mfumo ulioshindwa, kimaadili na kisiasa.

– Tunaukumbusha mfumo huu wa kisekula uliopitwa na wakati kwamba haki ni lazima ionekane na dhulma ni ishara ya kuanguka kwa mfumo huu.
Allah (swt) amesema : ( ﻭَﺳَﻴَﻌْﻠَﻢُ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻇَﻠَﻤُﻮﺍ ﺃَﻱَّ ﻣُﻨْﻘَﻠَﺐٍ ﻳَﻨْﻘَﻠِﺒُﻮﻥَ )
“Na wafanyao dhulma watajua ni mgeuko wa namna gani watakao geuka” [Ash-Shu’ara: 227].
Allah ni mkweli wa juu kabisa.

Ustadha Hanan Al-Khumairi
Msemaji mkuu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia

(Tafsiriwa)
Kwa hisani ya: Central Media Office – Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.