Mashindano Ya Tahfidh Quran Na Tafsiri.

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Tanzania upande wa Zanzibar wameandaa mashindano ya tahfidh Quran na Tafsiri yaliofanyika Tarehe 26 Rajab 1443H sawa na 27-02-2022M katika viwanja vya Fuji Bububu Zanzibar.
Jumla ya Madrassa tano zimeshiriki katika mashindano hayo yalioanza saa 3.00 asubuhi hadi 6.00 mchana.
Mgeni rasmin alikuwa ni Ustadh Ali Amour- Mjumbe wa Afisi ya habari Hizb ut Tahrir Tanzania.
Masha Allah wanafunzi walionesha umahiri wao na kufurahia sana mashindano hayo na kuiomba Hizb ut Tahrir Tanzania kuendelea na jambo hilo zuri.

Maoni hayajaruhusiwa.