Salamu Za Eid Kwa Waislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hakika umemalizika mwezi wa Ramadhani wenye kheri nyingi mno, na leo tupo katika Sikukuu ya Eid ul-Fitri yenye baraka. Sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunawapa hongera Waislamu wote wa Tanzania na Umma wote wa Kiislamu ulimwenguni kwa kuingia katika siku hii ya Eid. Tunamuomba Allah SWT Ajaalie kuwa ni Eid njema na yenye furaha.
Hakika funga yetu imeambatana na hali ngumu yenye kiza, kuanzia hali ya njaa na umasikini iliyogubika pia na kuenea kwa maovu. Pamoja na hayo yote Waislamu wamefunga kwa mapenzi,ucha Mungu,subra na yakini. Hii ni dalili njema,nasi tunamuomba Allah Taala Atukubalie swaumu zetu na visimamo vyetu na Atusamehe mapungufu yetu na makosa yetu. Amiin.
Enyi Waislamu,
Ramadhani imemalizika kwa mara nyingine tena ilhali Waislamu hawana Khalifah wa kusimamia mambo yao, kuchunga ibada zao, kuilinda miji yao na heshima zao, na kutetea matukufu yao. Mayahudi kwa mara nyengine wamefanya uadui kwenye Msikiti wa Aqsa wenye Baraka na kwa Waislamu wa Palestina ilhai hakuna wa kuwatetea. Aidha, China nayo imewateka, kuwazuiya, kuwaadhibu na kuwalazimisha kula mchana wa Ramadhani Waislamu wa Turkistani ya Mashariki na wala hakuna wa kuwasaidia Waislamu hao. Matatizo yamekuwa mengi katika miji wa Waislamu na wala hakuna wa kuwaondolea .
Enyi Waislamu,
Kwa hakika mmesifika katika mwezi wa Ramadhani kwa sifa tukufu sana katika sifa za Waislamu za kujifunga na halali na kujiepusha na haramu. Mataminio yenu mliyaweka nyuma na mkaelekea kwa Allah Taala kwa kutaka Radhi Zake tu. Basi fahamuni kuwa hivi ndivyo mnavyotakiwa kuwa katika Ramadhani na katika miezi mingine. Jambo hilo la kufungamana na amri ni la lazima, iwe katika swala,funga,katika kumpa baiá Khalifah, katika kutekeleza hududi,na katika hukmu nyingine zote za kisheria. Kwani zote zinatoka kwa Allah SWT Aliyesema :
﴿ ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً﴾
“Ingieni katika Uislamu wote”
Kuingia katika Uislamu wote humaanisha kuutekeleza Uislamu kivitendo katika nyanja zote za maisha, na jambo hilo haliwezekani ila kurejesha upya maisha ya Kiislamu kwa kumtawaza tena Khalifah kwa kuanzia katika nchi kubwa za Kiislamu na baadae kuenea dola hiyo ya Kiislamu duniani kote, ikiujaza ulimwengu masharika na magharibi kwa uadilifu na nuru kwa Idhini ya Allah Mtukufu.
Enyi Waislamu,
Hizb ut Tahrir Tanzania inakuhimizeni msipoteze fursa, inakuiteni mfanye kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashidah ambayo ni ngao na kinga ya Waislamu. Aidha,inawakumbusha ulazima wa kushikamana na hukmu za kisheria ndani ya siku ya Eid na kutokuchupa mipaka ya Allah SWT kwa kisingizio cha furaha ya Eid. Basi simamieni vyema familia na watoto wenu (katika Eid) na waleeni (wakati wote) kwa mujibu ya sheria ya Kiislamu.
Na mwisho tunamuomba Allah SWT Atukubalie amali zetu na Aifanye Eid hii ni yenye kheri na baraka kwa Waislamu wote popote walipo.
Hizb ut Tahrir Tanzania
01 Shawwal 1444 Hijria

Maoni hayajaruhusiwa.