Kilio Cha Baba Mzazi Wa Mtuhumiwa Wa Ugaidi

بسم الله الرحمن الرحيم

Wiki iliyopita mimi na Mwanaharakati mwenzangu Issa Dadi Namwao wa Hizb ut Tahrir hapa Mtwara tulimtembelea kumjulia hali Mzee Suleiman Mkaliaganda katika eneo la Chikongola
Mzee Mkaliaganda amekuwa mgonjwa kwa muda sasa akiumwa na kifua, hernia nk.
Mzee wetu huyu ambaye ni mstaafu bandari ya Mtwara ni baba mzazi wa mwanaharakati mwenzetu Waziri Suleiman Mkaliaganda ambaye amekuwa mahabusu hapa Mtwara katika Gereza la Lilungu kwa miaka 4 kwa tuhuma za ugaidi na kwa kisingizio kilekile cha uonevu kwamba ushahidi haujakamilika.
Kilio kikubwa cha mzee Mkaliaganda ni mustakbali wa mtoto wake ambae yuko mahabusu na suala la afya yake hasa ukizingatia uwezo wa wengine wanaomuhudumia ni mdogo.
Kwa hakika ni jambo la huzuni kubwa na kutia uchungu na hali ya kukosekana ubinadamu, kuona mtuhumiwa anashikiliwa mahabusu miaka mingi kwa uonevu huku familia yake kama wazazi na watoto wanamuhitajia.
Taasisi za kusimamia haki wanapaswa kuliangalia hili kwa ubinadamu na kwa uadilifu zaidi.
21/06/2021
Omari Ramadhani
Mtwara Mjini
Chanzo : Bin Rama
Picha : (Mtuhumiwa Waziri Mkaliaganda akiwa na binti yake)

Maoni hayajaruhusiwa.