Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Kuhusiana na Tukio la Kumbukumbu ya 99 ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah

بسم الله الرحمن الرحيم

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake na maswahaba zake, na wafuasi wake …

Kwa Ummah wa Kiislamu kwa jumla, umma bora uliotolewa kwa wanadamu… na kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir haswa, ambao Mwenyezi Mungu amewakirimu kwa ubebaji Ulinganizi Wake kwa ikhlasi na imani… na kwa wageni wa tovuti, wanaozuru kutokana na mapenzi ya kheri na nuru inayobeba kwa wote: Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Katika siku hii, miaka tisini na tisa iliyopita, mhalifu wa zama hizi Mustafa Kamal aliivunja Khilafah, na ingawa hili lilikuwa peupe hadharani, na kunakiliwa kwa dalili, bali kwa dalili zaidi ya moja, kuwa huu ni ukafiri wazi wa kufutilia mbali utawala wa Uislamu, na kwamba watekelezaji uhalifu huu wanastahili kupigwa vita kwa upanga kwa mujibu wa Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), iliyo simuliwa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Junada ibn Abi Umaiya aliyesema:

Tuliingia kwa ‘Ubada bin As-Samit hali ya kuwa yeye ni mgonjwa. Tukasema, “Mwenyezi Mungu akupe afya. Je, hutuelezi na sisi Hadith uliyoisikia kutoka kwa Mtume (saw) na ambayo kwayo Mwenyez Mungu huenda akakunufaisha?” Akasema, “Mtume (saw) alituita na tukampa Ahadi ya Utiifu kwa Uislamu, na miongoni mwa masharti ambayo kwayo alichukua Ahadi hiyo kwetu, بَايَعَنَا عَلَى السَّمْعِ وَالطَّاعَةِ فِي مَنْشَطِنَا وَمَكْرَهِنَا وَعُسْرِنَا وَيُسْرِنَا وَأَثَرَةً عَلَيْنَا وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ» “ilikuwa ni kwamba tutasikiza na kutii (maamrisho) kwa tunayo yapenda na tunayo yachukia na mazito kwetu na mepesi kwetu na kumtii kiongozi na kumpa haki yake hata kama yeye hatatupa haki yetu, na tusizozane naye isipokuwa tukiuona ukafiri ulio wazi ambao tunao uthibitisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”

Jukumu lilikuwa ni kupigana naye na kujitolea muhanga kwa hili kwa gharama yoyote ile, namna itakavyokuwa kubwa. Lakini dhalimu huyu Ummah hawakumkabili kwa anayostahiki, kummaliza! Hivyo basi historia ya Ummah ikaingia giza, Ummah ambao ni bora uliotolewa kwa wanadamu uliokuwa na Dola moja ya Khilafah, uliokuwa ukiogopewa, na kubeba Haki na uadilifu, sasa umekuwa ni mipasuko zaidi ya hamsini, ukiwa umegawanyika miongoni mwao, umeshindwa nguvu na wale wasiokuwa na huruma juu yao, na kupuuzwa mambo yao. Na sio hili tu, bali wanatawaliwa na watawala Ruwaybidha (wajinga) ambao ni watiifu, wanajisalimisha kwa makafiri, na wafuasi wa wakoloni, utajiri wao ndio unaopeleka uchumi wa maadui hawa wa Dini ya Mwenyezi Mungu. Ama uchumi wa nchi na watu wao, umezorota na kufujwa, watu wake hawanufaiki nao, bali hali yao inaeleza yote (kama vile mifugo walio jangwani wanaokufa kwa kiu ilhali maji (mzigo) yamebebwa migongoni mwao). Hili linafanyika machoni na masikioni mwa watawala Ruwaybidha (wajinga) hawa. Umasikini umeenea miongoni mwa watu, isipokuwa kwa pote la watawala na wapambe wao, ambao hupata zawadi iliyofinikwa kwa fedheha na aibu kwa huduma yao kwa mabwana zao wakoloni, khiyana kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waumini, na kizuizi katika njia ya Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al-Hakim.

Enyi Waislamu, Khilafah ndio kadhia nyeti ya Waislamu, ambayo kwayo Hudud (mipaka) huchungwa, heshima huhifadhiwa, ardhi hukombolewa, na Uislamu na Waislamu hutukuzwa, na yote haya yameandikwa katika Kitabu cha Al-Aziz Al-Hakim, na Sunnah ya Mtume Wake (saw), na Ijma’ ya Maswahaba zake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Inatosheleza kwa Muislamu kuyasoma mambo matatu yafuatayo ili kutambua ni jinsi gani Khilafah ni faradhi nzito na kubwa iliyoje; nayo ni haya yafuatayo:

Kwanza: Maneno yake, swala za Mwenyezi Mungu na salamu zimshukie yeye, yaliyo simuliwa na At-Tabarani katika Al-Ma’jam Al-Kabeer kutoka kwa Asim, kutoka kwa Abu Saleh, kutoka kwa Muawiyah, aliyesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), akisema:

«مَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مَيْتَةً جَاهِلِيَّةً» “Yeyote anaye kufa na hana shingoni mwake ahadi ya utiifu (kwa mtawala) amekufa kifo cha kijahiliya.”

Hii ni dalili ya ukubwa wa dhambi kwa Muislamu aliye na uwezo kutofanya kazi ya kumsimamisha Khalifah ambaye atampa bay’ah iliyo shingoni mwake, yaani ni dalili ya kumtafuta Khalifah anayestahiki bay’ah iliyo shingoni mwa kila Muislamu kupitia uwepo wake.

Pili: Lilikuwa ni jambo lililo washughulisha Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) la kusimamisha Khilafah na kumpa bay’ah Khalifah kabla ya kushughulika kwao na mazishi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Ingawa, kuharakisha mazishi ni jambo lililo hitajika na Shariah. Imeelezwa katika Ma’rifat Al-Sunan Wal Athar cha al-Bayhaqi: “Ash-Shafi’i amesema katika riwaya ya Abi Saeed: Inafadhilishwa zaidi kuharakisha kumzika maiti, endapo kifo kitathibitishwa.” Hii ni kwa maiti yeyote, vipi basi ikiwa maiti huyu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), licha ya hayo Maswahaba walifadhilisha kutoa bay’ah kwa Khalifah kuliko kumzika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na hivyo basi kuthibitishwa kwa Ijma’a ya Maswahaba kumsimamisha Khalifah kwa kuchelewesha kwao kumzika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) baada ya kufa kwake na kushugulika kwao na uteuzi wa Khalifah.

Tatu: Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, siku ya kifo chake, alikuwa ameweka muda maalumu wa kumchagua khalifah kutoka miongoni mwa sita (Maswahaba) walio ahidiwa Pepo, usiozidi siku tatu … Kisha akaagiza kuwa endapo Khalifah hatachaguliwa (hawataafikiana) katika siku tatu, wale watakaokuwa hawaafikiani watauawa baada ya siku tatu hizo. Na akawapa jukumu hilo watu hamsini miongoni mwa Waislamu kutekeleza hili, yaani kumuua yule asiyekubali, ingawa walikuwa wameahidiwa Pepo, na walikuwa katika watu wa Shura, na walikuwa katika Maswahaba wakubwa. Hili lilifanyika machoni na masikioni mwa Maswahaba, hakuna riwaya yoyote kuwa yeyote kati yao hakuafiki au alikataa hili. Hivyo basi ni Ijma’a ya Maswahaba kuwa ni haramu kwa Waislamu kubakia bila ya Khalifah kwa zaidi ya michana mitatu pamoja na usiku wake, na ni “mafungu mangapi ya siku tatu” yapetupitia, La Hawla Wa La Quwata Ila Billah! Hivyo basi Khilafah, Enyi Waislamu, ni kadhia muhimu na nyeti kwa Waislamu na ni kadhia iliyoje hii!

Enyi Waislamu, licha ya hili, hatukati tamaa na rehma ya Mwenyezi Mungu, ﴾إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ﴿ “Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri.” [Yusuf: 87]

Hususan kwa kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amewaahidi wale walio amini na kutenda mema kuwa atawafanya makhalifa (watawala) katika ardhi ﴾وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ﴿ “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [An-Nur: 55].

Vilevile, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara njema ya kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala wa kidhalimu ambao tunaishi chini yake. «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume.” [Imesimuliwa na Ahmad kutoka kwa Hudhayfah ibn al-Yaman, Mwenyezi Mungu awe radhi naye].

Lakini, tunathibitisha na kurudia yale tuliyo tangulia kusema, kuwa Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz atatunusuru ikiwa tutamnusuru, kupitia kuwa miongoni mwa wafanyi kazi wenye ikhlasi waaminifu. Ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kuwa malaika hawata teremshwa kufanya kazi kwa niaba yetu na kusimamisha Khilafah kwa ajili yetu, huku tukiwa tumeketi na kubarizi makochini mwetu! Bali, Mwenyezi Mungu (swt) huwateremsha malaika, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kutusaidia huku tukiwa tunafanya kazi, na hiyo ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu katika kila ushindi, ima iwe ni katika kusimamisha Khilafah kwa kazi ya kheri na kuimakinisha, au iwe ni katika ufunguzi na ushindi wa Mwenyezi Mungu kupitia kupigana katika njia yake (swt).

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuukirimu Ummah huu kwa kuasisiwa Hizb ut Tahrir, inayojitolea kwa kazi makinifu na ya ikhlasi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kurejesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah ya Uongofu. Ni kiongozi ambaye hawadanganyi watu wake. Ni chama ambacho kheri yake inang’aa, na wote ambao hawawezi kuhimili kheri hii wanaporomoka kutokana nayo. Hii ndiyo tunayo amini kuwa ndiyo hali na tunaamini kuwa mashababu (wanachama) wake wanaofanya kazi nayo wako makini na wenye bidii, wafanyakazi watiifu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, walio na hamu ya Akhera juu ya matarajio yao ya duniani. Na wanafanya kazi mchana na usiku, wakitaraji kupata Rehma za Mwenyezi Mungu; kuwa ahadi Yake (swt) na bishara njema ya Mtume Wake (saw) zitatimia kupitia mikono yao, na hili ni sahali kutimizwa na Mwenyezi Mungu.

Kwa kutamatisha, faradhi ya kusimamisha Khilafah, Enyi Waislamu, haiko tu juu ya wanachama wa chama hiki pekee, bali pia juu ya kila Muislamu mwenye uwezo, kwa hiyo tupeni nusra, Enyi Waislamu, na tupeni nusra Enyi majeshi ya Waislamu, na rejesheni izza ya Answar (walionusuru) walipoinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa sawa na Muhajirina, akawasifu na akawa radhi nao katika Kitabu Chake Kitukufu bila ya mipaka. Mbali na hayo kazi hii imefungika kwa wafuasi wake kwa wema (Ihsan).﴾وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿ “Na wale wali tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” [At-Taubah: 100]

Hii ni kwa sababu ya thamani, malipo makubwa, na utukufu wa kuheshimika ambao kazi ya kunusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na kusimamisha Khilafah iliyo nayo, kufikia hadi malaika kubeba mwili wa Saad bin Muadh, Sayyid al-Answar (Bwana wa Maanswar), Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kama ilivyo elezwa katika Al-Mustadrak juu ya Al-Sahihain na Al-Hakim kuhusu utukufu wa kitendo cha kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu.

Mwisho kabisa, yeyote atakaye inusuru kazi hii ya kusimamisha Khilafah kabla ya kusimama kwake, malipo yake ni mengi na makubwa kuliko kuinusuru Khilafah baada ya kusimama kwake ﴾لَا يَسْتَوِي مِنْكُمْ مَنْ أَنْفَقَ مِنْ قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ أُولَئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِنَ الَّذِينَ أَنْفَقُوا مِنْ بَعْدُ وَقَاتَلُوا وَكُلّاً وَعَدَ اللَّهُ الْحُسْنَى وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿ “Hawawi sawa miongoni mwenu wenye kutoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walio toa baadae na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Al-Hadid: 10].

Na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwa dhati kuwa kumbukumbu hii ya tisini na tisa iwe ndio utangulizi wa ushindi mkubwa wa Mwenyezi Mungu kabla ya kumbukumbu ya mia moja ya kuvunjwa Khilafah na kisha Khilafah ya Uongofu itang’aa tena ulimwenguni.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴿

 “Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Wa Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Jumatatu, 28 Rajab 1441 H                                           Ndugu yenu,

23/3/2020 M                                                                Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

                                                                                            Amiri wa Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.