Bayan Msikiti Mweupe Mtongani Dsm

Masoud Msellem Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habar Hizb ut Tahrir Tanzania akitoa bayan baada ya swala ya Ijumaa msikiti Mweupe Mtongani Dar es Salaam;

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ
Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha.
(Maida:15)

– Katika hii (maida:15) Allah (swt) amemuita Mtume Muhammad (saw) ni Nuru
– Muongozo aliokuja nao Mtume Muhammad umekuja ili kumtoa Mwanadamu kwenye kiza cha kila dhulma na kumpeleka kwenye Nuru.
– Ili tujue Nuru aliyokuja nayo Mtume Muhammad (saw) ni kuyaangalia maisha waliyokuwa wakiishi waarabu kabla ya kuja uislamu
– Makureishi walikuwa wakiabudu masanamu waliyotengenza wenyewe kisha wakiyaabudu, hii ni kuonyesha walikuwa duni kifikra na hata kufikia kutengeneza miungu ya tende kisha wanapokuwa na njaa huyala kiungo kimoja kimoja.
– Kuuwa watoto wao wa kike kwa kuogopea umasikini na idhilali waliyokuwa wakiona kipindi hicho.
– Dhulma kwa wanyonge katika uchumi waliyokuwa wakitenda watawala mabwanyenye
– Mtume Muhammad (saw) aliibadilisha hali hiyo na kueneneza nuru kwa ulimwengu
#MuhammadNiNuruKwaUlimwengu

Maoni hayajaruhusiwa.