Uzuri wa Ulipaji Deni

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali kutoka kwa:

  1. (Asma Jube)

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh,

Mtu akikopa tani moja ya chuma, chambilecho wasemaji, arejeshe tani moja na ziada kwa utashi wake huria bila ya ombi au shinikizo kutoka kwa mkopeshaji… Je huo sio ulipaji mzuri?… Nategemea mutatuelimisha). Mwisho

  1. (Umm Ahmed)

Kama inavyotajwa si halali kukopesha kitu mtu ili akurejeshee kidogo au kingi, ila akulipe sawa na kile ulichomkopesha aina yake na kiwango chake, Jazakallah Khayra. Lakini mimi nimepata mkanganyiko wa neno ulipaji mzuri. Na kwanini hauhisabiwi kuwa ni riba ikiwa ziada yoyote katika aina na kiwango kama ilivyotajwa katika jawabu huhesabiwa kuwa ni riba? Je hamkutueleza kwanini tumeizingatia hadithi ya Mtume (SAAW) wakati alipokopa ngamia ndama na akarejesha aliyebora wa miaka minne kuwa ulipaji mzuri na tukazingatia kuwa mwenye kukopa tani moja ya chuma akarejesha tani moja na nusu kuwa ni riba? Je kwani hapakutajwa kuwa haifai kuzidisha aina na kiwango? Mwisho.

  1. (Aliyethabiti na ahadi ya Allah)

Assalamu Alaykum Sheikh wetu mkarimu, Allah akulipe kheri… Pameelezwa kwenye jawabu… Na ni wajibu kurejesha deni kwa mwenyewe bila ya ziada “ya manufaa” kama si hivyo basi itakuwa riba… Je hii ziada unakusudia..ziada yoyote iliyoshurutishwa na mkopeshaji wakati wa kukopa… Ama bila ya kutaja sharti haifai kule kuzidisha?).Mwisho

Jawabu kwa maswali haya matatu kwa kuwa ni ya maudhui moja:

Waalaykum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,

Kuhusu yaliyopokewa katika hadithi ya Mtume (SAAW) juu ya ulipaji mzuri, hiyo haina maana kuzidisha katika idadi au katika kipimo cha wingi au cha ujazo bali ina maana katika idadi yenyewe na kipimo cha wingi chenyewe na kipimo cha ujazo chenyewe, lakini inafaa (kulipa) kwa kilichokizuri zaidi ya hicho (kilichokopwa). Basi kwa mfano, mtu akikopa kwa mtu ngano ya kiwango cha kilo gram 10, inafaa kumrejeshea ngano iliokuwa nzuri zaidi lakini kwa kiwango kile kile cha kilo gram 10. Na kwa mfano, akikopa pishi kumi za mchele, inafaa kumrejeshea mchele mzuri zaidi  lakini kwa kipimo kilekile yaani pishi kumi, na akikopa mbuzi, inajuzu kumrejeshea mbuzi aliyemzuri  zaidi lakini sio mbuzi wawili… Huu ndio ulipaji ulio mzuri. Bali sio kuzidisha katika kipimo cha ukubwa au cha ujazo au cha idadi

Hivyo ndivyo inavyofahamika hadithi ya Mtume (SAAW) iliyotajwa katika jawabu letu lilitangulia,  na haya hapa ndiyo maelezo yake:

Kutoka kwa Abii Rafi’i amesema: “Mtume (SAAW) alikopa ndama wa ngamia mmoja akamjilia (akaletwa) ngamia wa sadaka akaniamrisha nimlipe mwenyewe ngamia wake, nikamueleza sijampata katika ngamia isipokua ngamia bora wa miaka minne. Mtume (SAAW) akasema mpe yeye, kwani mbora wa watu ni yule mbora zaidi wa kulipa”. Ameipokea Abuu Daud na wengine.

Yaani alimrejeshea ngamia mzuri na bora zaidi kuliko yule ngamia aliyekopa lakini kwa idadi ile ile yaani alimlipa ngamia mmoja.

Na haya ndio yaliyokuja katika jibu letu kuhusu kukopa kwa mfano tani moja ya chuma na kurejesha tani moja na nusu kuwa haifai bali ni kipimo kilekile.

Kwa ufupi, ni kwamba ulipaji mzuri haina maana kuzidisha katika kipimo cha ukubwa au ujazo au idadi bali kwa kipimo cha ukubwa (wazn) kilekile na cha ujazo ule ule na cha idadi ileile, lakini inafaa kuwa ni aina bora atakapotaka mkopaji kulipa kilicho bora bila ya kuwekewa sharti hilo na mkopeshaji, kwasababu Mtume (SAAW) alilipa kilichokizuri na bora zaidi bila kuwekewa sharti na mkopeshaji.

(Na ama kukopa inafaa katika mbea hizi sita na nyenginezo na kila kinachomilikiwa, na ni halali kukitoa katika milki na riba haingii humo ila itakapovuta manufaa, kutokana na yale aliyopokea Alharith bin Abii Usama kutokana na hadithi ya Ali (RA) kwa lafdhi “Hakika ya Mtume (SAAW) amekataza mkopo wenye kuvuta manufaa”. Na katika riwaya nyengine “Kila mkopo unaovuta manufaa basi hiyo ni riba”. Na huvuliwa kutoka hilo kile kinachokua katika upande wa ulipaji mzuri bila ziada kutokana na yale aliyoyapokea Abu Daud kutoka kwa Abii Rafi’i amesema: Mtume (SAW) alikopa ndama wa ngamia mmoja akamjilia (akaletwa) ngamia wa sadaka akaniamrisha nimlipe mwenyewe ngamia wake, nikamueleza sijampata katika ngamia isipokua ngamia bora wa miaka minne. Mtume (SAAW) akasema mpe yeye, kwani mbora wa watu ni yule mbora zaidi wa kulipa”).

Wala hapasemwi kwamba hiba na zawadi vinafaa atakapolipa deni zaidi kwa kipimo cha ukubwa au idadi au ujazo kwa ridhaa ya nafsi bila ya sharti kuwa inafaa. Hapasemwi hivyo kwasababu  hili linajuzu ikiwa halikuambatana na maudhui ya mkopo, lakini ziada hapa imetokezea kwasababu ya mkopo, basi hiyo (ziada) ni manufaa yanayotokana na huo mkopo, inajumuishwa (hiyo ziada) katika yale aliyoyapokea Alharith bin Abii Usama kutokana na hadithi ya Ali (RA) kwa lafdhi “Hakika ya Mtume (SAAW) amekataza mkopo wenye kuvuta manufaa”. Na katika riwaya nyengine Kila mkopo unaovuta manufaa basi hiyo ni riba”

Pia hapasemwi kuwa aina nzuri nayo ni riba, hapasemwi hivyo kwasababu Mjumbe (SAAW) amejuzisha na akaihesabu kuwa ni katika ulipaji mzuri kama ilivyo katika hadithi ya Abii Rafi’i iliyotajwa hapo juu.

Nataraji haya kuwa yametosheleza Inshallah. 

Ndugu yenu Ata ibn Khalil Abu Rashta

05, Shaban 1439H

21, April 2018

Maoni hayajaruhusiwa.