Ujumbe Maalumu Uliowasilishwa Ubalozi wa Nchi ya Jordan.

Ujumbe maalumu kutoka Hizb ut Tahrir Wilaya ya #Uturuki uliowasilishwa kupitia mkutano wa vyombo vya habari katika ubalozi wa nchi ya Jordan.
Kutokana na #IsmailAlwahwah, kuwekwa kizuizini kwa dhulma na serikali ya #Jordan.
Ismail Alwahwah, mwanachama wa ofisi ya habari ya Hizb ut Tahrir nchini #Australia, ambae alikamatwa wakati akifika katika uwanja wa ndege wa Queen Aliyah mnamo 25 mwezi wa saba alipokua safarini kwenda kuwatembelea ndugu zake wa Jordan. Na bado anashikiliwa hadi hivi sasa. Mikutano ya waandishi wa habari inayofanywa na Hizb ut Tahrir hivi sasa katika nchi zote Australia na Wilayah ya Jordan inatoa mwito wa kumalizika kwa dhulma , na kuachiwa kwa Ismail Alwahwah,
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilaya ya uturuki umewasilishwa kwa lugha zote ikiwa ni kiarabu, Kituruki na kiingereza katika ubalozi wa Jordan uliopo Ankara.
Mkutano huo ulilenga na ulisisitiza mambo yafuatayo:
“Masiku 10 yamepita tangu kukamatwa, hakuna mashtaka yaliothibitishwa na mbaya zaidi amenyimwa uwakilishi wala usaidizi wowote wa kisheria ikiwa ni pamoja na kutopewa hata wakili wa utetezi.
Ustadh Ismail anasumbuliwa baadhi ya maradhi, chronic and life-threatening, hivyo utawala wa Jordan utawajibika kwa chochote kitakachotokea kuhusiana na afya ya Abu Anas.
Na ni bora tukumbushe kwamba utawala wa Jordan unahistoria mbaya ya utesaji na unyanysaji.
Wanaharakati wengi wa kisiasa wapo jela tena bila kuzingatia utawala wa sheria na haki, ambavyo vyote hivi vinatufanya tuwe na khofu zaidi kuhusu hali ya Ustadh Ismail na usalama wake …”
“Tunatoa mwito kwa vyombo vya dola vya utawala wa Jordan kwamba vikwazo hivi vilivyowewa katika njia Allah havitaweza kuizuia Hizb ut Tahrir na wanachama wake katika kuwaita watu na kufanya kazi na ummah na hilo litaendelea hadi kufikia ahadi ya nguvu kutoka kwa Allah na ushindi uliozungumzwa na Mtume wake ﷺ wa kuisimamisha khilafah rashida kupitia njia ya Utume imefikiwa…”

Ismail Alwahwah ni mmoja kati ya wanachama wa Hizb ut Tahrir, alishikiliwa na utawala wa jordan mnamo 1990. Na bado yupo jela kwa kipindi kirefu na alihukumiwa kifo. Lakini aliachiwa baada ya kugundulika kuwa mashtaka anayotuhumiwa hayakua na ushahidi wowote. Bado anaendelea kubeba ulinganizi (Da’wah) nchini Australia, na amefanikiwa kulisambaza jina la Hizb ut Tahrir na fikra zake katika kipindi kifupi na amefanikiwa kupata rai amma katika mambo tofauti kuhusu waislamu katika nchi ya Australia.

Tunamomba Allah (swt) kufanikisha uachiwaji wa ndugu yetu Ismail Alwahwah kutoka katika makucha ya madhwalimu na kumpa ponyo ya afya yake na usalama wake kwa kipindi hichi kigumu anachopitia.

Ofisi ya habari ya Hizb ut Tahrir
wilaya ya uturuki
Jumanne, 17th Dhul Hijjah 1439 AH – 28/08/2018 CE

Imetafsiriwa kutoka page ya Alkhilafah
https://web.facebook.com/646683775466624/posts/1426182290850098/?_rdc=1&_rdr

Maoni hayajaruhusiwa.