Hizb ut Tahrir Na Ummah Mwezi Muharamu

1. MUHADHARA WA KUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KIISLAMU

(a) Masoud Msellem Mwakilishi kwa vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania akizungumzia Mwaka mpya wa Kiislam (1440 Hujiria) kwenye Muhadhara uliofanyika  Masjid Ihsani Goroka kwa Ustadh- Kongowe Dar es Salaam, baada ya swala ya Ijumaa.
#UislamNiHadharaMbadala

(b) Sheikh Musa Kileo alipokuwa akiwakumbusha Ummah Msikiti wa Kichangani Dar es Salaam, Umuhimu wa Mwaka mpya na Tukio kubwa la hijrah

(c) Mada ya 1: Mwaka mpya wa kiislam
Mtoa mada: Ustadh Abubakar Matasi
Mwada ya 2: Hijirah: Nukta ya Mageuzi ya kiislam
Mtoa mada: Ustadh Abass Huseini
Mwendeshaji muhadhara: Shafii AbdulMalik Lugazo

  

2. JAULA MITAANI

(a)  Mashabab wa Hizb ut Tahrir eneo la Kigamboni jana Jumapili 09/09 walifanya Jaula eneo la Kibada kuukumbusha Ummah juu ya kalenda ya Kiislamu na tukio la Hijra kwa ujumla.

#UislamNiHadharaMbadala

b) Wanachama wa Hizb ut Tahrir eneo la Tanga wakifanya Jaula maeneo ya Mwakidila Tanga. Waislam walifahamishwa juu ya dhulma za nidhamu ya kibepari ya kiuchumi, na kuonyeshwa kuwa Uislamu tu na pekee ndio mfumo mbadala wakutatua hali hiyo na kuleta tija kwa Umma. Pia waliwakumbusha Waislamu washiriki pamoja katika kubeba jukumu msingi la ulinganizi

#UislamNiHadharaMbadala

(c) Kwa munasaba wa kuingia mwaka mpya wa kiislam 1440 Mashabab wa Hizb ut-Tahrir Zanzibar leo jioni wamefanya Jaula ya kuwatembelea ndugu zao wa kiislam katika mitaa mbali mbali ya Amani mjini  Zanzibar ikiwa ni kuwakumbusha ukubwa wa tukio la Hijra na mabadiliko ya kweli ya Umma wetu ni kupitia Khilafah ambayo itaukomboa Umma mzima wa kiislam kutoka katika minyororo ya kibepari.

  

3. KHUTBA ZA IJUMAA

(a) Khatib: Ustadh Hassan Kishk
Mada: Mwezi Muharam
Masjid: Fat-h National Mwanza

  

(b) Khatib: Sheikh Musa Kileo Mwenyekiti Kamati ya Mawasiliano Hizb ut Tahrir Tanzania

Mada: Madhara ya kuishi chini ya mfumo wa kikafiri na faida ya kuishi chini ya KHILAFAH.
Masjid: Lulu Chamazi

  

(c) Masjid Rahma Buguruni Kwa Madenge Dar es Salaam.
    

(d)  Khatib: Sheikh Yusufu Mohamedi
Mada: Lengo la kuletwa kwa Mitume (Manabii)
Masjid: Nuruh Mikadi Kigamboni

  

(e)  Khatib: Baraka Rashid
Mada: Tukio kubwa la mwezi Muharam (Hijra)
Masjid: Fat-h national Mwanza

  

(f) Khatib: Ustadhi Juma Abdallah
Mada: Mazingatio ya hijra
Masjid: kizinga Mbagala Dar es Salaam

  

(g) Khatib: Ustadh Hassan Kishk
Mada: Mwezi Muharam
Masjid: Fat-h National Mwanza

  

(h) – Masjid Rahma, Kipapo/ Mtondooni -Pemba Zanzibar

– Masjid: Rahma Pile Temeke.

 

 

4. KALIMA NJE ZA MISIKITI

(a)  Mwanaharakati wa Hizb ut Tahrir eneo la Mwanza Ust. Issa Nassib akitoa kalima nje ya Masjid Qadiriya (Libeti) Mwanza juu ya kuukaribisha Mwaka mpya wa Kiislamu 1440 Hijriya.

  

(b) Ustadh Abubakar Matasi na Ustadh Mkiongwe Mbwana wakiukumbusha ummah wa Kiislamu Tukio kubwa la Hijra lililoufanya ummah wa Kiislamu kupata Izzah kutokana na madhila waliyopata kutoka kwa makafiri kutokana na imani yao kwa Allah.
Mwezi huu wa Muharamu ambao ndio mwezi wa mwanzo wa mwaka 1440 Hijiria tuutumie kurejesha tena Izzah na utukufu uliopotea baada ya kuangushwa kwa Dola ya Khilafah
#UislamuNiHadharaMbadala

  

(c) Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania Shafii AbdulMalik Lugazo, akiwakumbusha ummah wa kiislamu      tukio kubwa la Hijra lililoupa ummah wa Kiislamu Izzah toka udhalili na kupata mamlaka ya utawala wa        Dola ya kiislamu.

Enyi Ummah wa Kiislamu!
Utumieni mwezi huu wa Muharamu kurejesha Izzah yetu iliyopotea baada ya kuangushwa kwa Dola ya        kiislamu ya Khilafah tareh 28 Rajabu 1342 hijiria sawa na 3 machi 1924 miladia

  

(d) Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania Ustadh Yahya Idrisa akiwakumbusha ummah wa kiislamu mazingatio kutokana na tukio la hijra, baada ya swala ya Ijumaa Masjid Ngazija, Posta Dar es Salaam.

  

(e) MASHINDANO YA HIJRA CUP

Mashindano ya mpira wa miguu yalioanzishwa na Hizb ut tahrir kwa lengo la kuwakumbusha watu juu ya tukio zima la Hijra na Mwaka mpya wa Kiislam 1440.
Mashindano hayo yalianza rasmi tarehe 22/09/2018 katika viwanja vya shule ya msingi Igoma Nyamagana-Mwanza.

  

 

Mashindano ya hijra cup ambayo yamemalizika tarehe 29 /9/2018 Miladia – 19 Muharamu 1440 Hijiria kwa Mchezo wa fainali kati ya Igoma magharib Mwanza dhidi ya Mandu Fc ambapo timu ya Mandu fc iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuibuka kua mabingwa wa Hijra Cup 1440.
Nasaha fupi ikitolewa na Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania Sheikh Issa Nasibu, iliyo lenga kuukumbusha umma juu ya tukio la Hijra na kuwajulisha lengo la Hijra Cup na kufafanua vyema kuadhimishwa kwa mwaka mpya wa Kiislam ambayo leo ni kitu kilichosahaulika katika historia.

  

5. ZIARA MAALUM ZA MADRASA

Wanaharakati wa Hizb ut-Tahrir eneo la Zanzibar wakiwa katika ziara za kuzitembelea madrasa mbali mbali za kiislam katika mfululizo wa matukio ya kampeni maalum ya kuukaribisha Mwaka mpya wa kiislam 1440 Hijria. Wakiwa Katika madrassa ya Tilaawatul-lquran iliopo Bububu mianzini                               Zanzibar, walipata fursa kubwa ya kuwakumbusha walimu wa madrasa hio juu ya umuhimu wa  kuifundisha vyema Tarekhe (historia) tukufu ya kiislam ikiwemo sira ya Nabii Muhammad (S.A.W) kwa vijana wa kiislam ili kuilewa dini yao na matukio makubwa ya kitarekhe ikiwemo tukio kubwa la hijra  ambao ndio imeasisiwa rasmini kalenda ya kiislam kwa munasaba wa tukio hilo.

  

6. SAUMU YA ASHURAA

Wanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania wakiwafuturisha ndugu zao waislam Masjid Haqqah Buguruni Kwa Madenge Dar es Salaam
#UislamNiHadharaMbadala

  

7. NDANI YA STUDIO

(a)Mashababu wa Hizb ut Tahrir eneo la Zanzibar wakiwa katika studio za Island Tv katika kipindi cha ‘Ujue Uislamu’. Mada ilikuwa: ‘Kuangamizwa Fir-aun’

Kipindi kilirushwa hewani Ijumaa saa 3.00 usiku InshaAllah

 

(b)REDIO AL- NOOR

Mjumbe wa Kamati Mawasiliano Hizb ut Tahrir Tanzania, Mohammed El-Bahry Mjumbe wa Kamati Mawasiliano Hizb ut Tahrir Tanzania, Mohammed El-Bahry alipokuwa mubashara katika studio za Radio Al Noor 93.3 FM (Zanzibar )

8. KUTANGAZA THAQAFAH

(a) A’amali ya kusambaza Thaqafah ya kiislam kupitia uuzaji wa vitabu na CD mbali mbali za mawaidha na makongamano ya kiislam iliyo fanyika katika msikiti wa Amani magengeni Zanzibar

  

(b) Aamali kusambaza Thaqafah ya kiislam kupitia uuzaji wa vitabu na CD iliofanyika leo baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Ngamia Kilimahewa Zanzibar

  

(c) A’amali ya kusambaza thaqafah ya kiislam iliofanywa katika masjid sunna rahaleo mjini Zanzibar

    

 

 

Maoni hayajaruhusiwa.