Tunalaani Mateso kwa Vijana wa Hizb ut-Tahrir Zanzibar

2

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania inalaani kwa nguvu zote kitendo cha kishenzi, kiharamia na cha kikatili kilichotendwa na kikundi cha watu wasiojuulikana wenye silaha za moto kuwanyakua kisha kuwatesa vijana watatu wa Kiislamu wa Hizb ut Tahrir mnamo tarehe 1 Machi kijijini Kiboje, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Zanzibar.

Kundi hilo la maharamia likiwa na silaha za moto (bila ya sare) bila ya kujitambulisha, kwa mabavu liliingia kijijini hapo kiasi cha saa nane mchana, baadhi yao wakiizingira nyumba (waliyokuwemo vijana hao) kwa silaha kana kwamba wako vitani, kisha kuwatia nguvuni vijana Juma Muarabu, Ibrahim Silima na Said Mohammed, kuwafunga pingu, kuwafunika nyuso zao, kuwaingiza garini kwa nguvu na kwenda nao pasipojulikana kwa ajili ya kuwatesa kwa mateso ya kikatili, kiuadui na yasiyoelezeka. Hatimae kuwarejesha na kuwaacha huru siku hiyo hiyo kiasi cha saa nne usiku wakiwaonya vikali waache kujihusisha na harakati ya Hizb ut-Tahrir.

Kitendo hiki cha kishenzi, aibu na kilichosheheni woga kiasi cha maharamia hao kukhofu kwa kuwaziba vijana hao nyuso na maharamia hao kukosa hata ujasiri wa kujitambulisha. Lakini zaidi jambo hili ni dhihirisho la wazi la kiwango cha juu cha uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu pamoja na ukweli kuwa Waislamu ndio wengi zaidi kiidadi miongoni mwa wakaazi wa Visiwa vya Zanzibar.

Pamoja na hayo, uwepo wa makundi kama haya ya kiharamia kwa muda mrefu ndani ya Zanzibar na kutenda uharamia wao mchana kweupe bila ya kukemewa amma kuchukuliwa hatua thabiti na serikali ni jambo linalotia shaka kubwa juu ya uwezekano wa makundi hayo kufanya kazi kwa baraka kamili za Jeshi la Polisi  bila ya kusahau kutumiwa makundi hayo na wanasiasa.

Tunawaomba kwa mikono miwili wote wenye walau tembe ya ubinadamu na hisia ya uadilifu kulaani kwa ukali na kukemea matendo haya ya maharamia ambayo huchochea zaidi kudhoofisha mshikamano wa kijamii.

Tunawakumbusha maharamia, wasaidizi wao na wanaowaunga mkono kwamba matendo yao maovu hayatosamehewa wala kusahauliwa.

وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ

مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ

Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayotenda madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapokodoka macho.  Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu”   (TMQ 14: 42-43)

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Tanzania

Kumb: 03/ 1438 AH

Jumatano 9 Jumada II, 1438 AH

3/3/2017 M

Simu: +255778 870609

2 Comments
  1. sklep online says

    Wow, incredible blog layout! How lengthy have you ever been running a blog for?

    you make blogging glance easy. The total look of your web site is wonderful,
    as smartly as the content! You can see similar here najlepszy sklep

  2. Roshaunda says

    I just like the helpful information you provide on your articles.
    I’ll bookmark your blog and take a look at again here frequently.
    I’m reasonably sure I will be informed a lot of new stuff right
    here! Best of luck for the next!

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.