Madawa ya Kulevya Tanzania na maslahi yake kwa Ubepari

0

Vita dhidi ya madawa ya kulevya vinaonekana kupamba moto Tanzania baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoa agizo la kukamatwa baadhi ya watu mashuhuri.

Vita hiyo ikaongezeka msukumo zaidi kwa kauli ya Raisi kutangaza kwamba vita hiyo ni ajenda pana inayopasa kuhusisha taasisi zote, pia na uteuzi wake kwa Kamishna Mkuu wa Tume ya Udhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya (The Drug Control and Enforcement Agency (DCEA).

Kwa qadhia, sisi Hizb ut-Tahrir Tanzania tunatamka yafuatayo:

  1. Vita ya madawa ya kulevya Tanzania na dunia nzima inaendeshwa juu ya msingi wa usanii. Kwa kuwa mfumo wa kibepari unaotawala dunia leo umejengwa juu ya msingi wa maslahi. Ambapo kila kitu hupimwa kwa kipimo hicho.

Zaidi ya hayo, siasa katika nidhamu ya kidemokrasia hufadhiliwa na mabepari ambao huwa ndio wadau wakubwa wa biashara ya madawa ya kulevya. Hivyo, ni wazi kwamba vita hivi vimekosa msukumo wa kidhati, ni kauli mbiu tupu bila ya matendo ya kweli ili kuhadaa raia na kuhamisha hisia na fikra zao kutokana na kushindwa  kwa serikali katika qadhia nyingi. Itakumbukwa kuwa wanasiasa mashuhuri waliotangulia waliwahi kutamka kuwa wana orodha ya wahusika wa madawa ya kulevya, lakini licha ya mamlaka yao makubwa hawakuthubutu kuwataja.

  1. Nidhamu ya kidemokrasia inapigia debe na kuwajenga watu fikra hatari ya ‘uhuru binafsi’ inayohamasisha watu kujitosa katika matumizi wa madawa haya, ikiwa ni sehemu ya kujifaragua kwa uhuru wao. Ni wazi, matumizi ya madawa ya kulevya yana fungamano la moja kwa moja na fikra ya ‘uhuru’ ambayo ni nguzo muhimu ndani ya demokrasia.
  2. Mfumo wa kibepari hususan nidhamu yake ya kiuchumi huwabana raia kiasi cha kuchanganyikiwa kutokana na ugumu wake na natija yake ya kikatili. Hali hiyo huwapelekea baadhi kudhani kuwa kujitosa katika matumizi ya madawa ya kulevya kunaweza kupozapoza mashaka waliyonayo au walau kujipatia faraja japo kwa muda. Kimsingi, ubepari hauna suluhisho la kiroho kumtuliza mwanadamu kipindi cha tabu na mashaka.
  3. Zaidi ya hayo, nidhamu ya kidemokrasia katika kusukuma maslahi ya kiuchumi huwaburuza watu kunyenyekea kibubusa na kuwapenda kupita kiasi watu mashuhuri kama vigezo vyao. Watu ambao baadhi yao ni watumiaji wa mihadharati. Matokeo yake vijana waliolewa kuwapenda watu hao maarufu hutumbukia kati kati ya dimbwi la mihadharati.
  4. Nidhamu ya kidemokrasia na mtazamo wake wa kisekula chini ya sheria za kibinadamu kamwe haiwezi kukabilina na tatizo la mihadharati, kutokana mkanganyiko wake wa kinafiki wa kuhalalisha baadhi ya aina za ulevi na kuharamisha nyengine. Ilhali aina zote za ulevi zinamdhuru mwanadamu. Jee ni vipi utakuwa na ujasiri na uhalali wa kimaadili kuzuiya aina fulani ya mihadharati na kuruhusu aina nyengine?

Uislamu ndio mfumo pekee wenye nguvu katika imani na sheria zinazoweza kuilinda jamii dhidi ya mihadharati, kukabiliana na vita hii kwa ukamilifu wake, kwa kuharamisha aina zote za ulevi.

Muda umeshawadia hususan kwa wasiokuwa Waislamu wajionee na kuthamini uadilifu wa Uislamu, ambapo chini ya utawala wake wa Khilafah hufanya kazi bila ya kusita kulinda heshima ya mwanadamu, mali yake, imani yake nk.

 

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut-Tahrir Tanzania.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.