Sehemu Kutoka Katika Khutba ya Carly Florina, Mkurugenzi wa Hewlett-Packard (HP)

“Kuliwahi kuwa na ustaarabu ambao ulitikisa dunia.

Ambao uliweza kuunganisha mataifa makubwa katika mabara ambao ramani yake ilianzia bahari moja hadi bahari nyingine, kutokea kaskazini hadi kupita katika majangwa. Ndani ya utawala wake waliishi mamilioni ya watu, kutoka katika rangi tofauti na makabila tofauti.

Moja ya lugha yake ikiwa ndio lugha ya ulimwengu, ilikua ni daraja la wanaardhi. Jeshi lake lilijengwa na wanajeshi wamataifa tofauti tofauti, na ulinzi wa jeshi lake ulidhamini amani kiasi ambacho haikuwahi kutokea kabla yake. Ustaarabu huo ulieenea kutoka Amerika ya kusini hadi China na kila sehemu.

Na thaqafa hii ilisimamiwa zaidi ya kitu chochote, kwa uvumbuzi. Wanamitindo wake wakisanaa katika ujenzi ambayo ilidhibiti kani ya mvutano. Wanahesabu wake ndio waligundua aljebra na algorithms ambavyo vilipelekea upatikanaji wa kompyuta, na mitindo mingi ya kihesabu. Madaktari wake ndio waliochunguza na kugundua tiba mpya za magonjwa. wanaanga wake walitizama angani na kuzipa majina nyota, hivyo kutengeneza njia za safari za angani na gunduzi za angani.

Waandishi wake ndio walitengeneza hadithi. Hadithi za uhamasishaji na maajabu. Wanamashairi wake waliandika mapenzi wakati ambapo wakati waandishi wengine kabla yao walijawa na khofu juu ya mambo hayo.

Wakati mataifa mengine yaliposhindwa kutengeneza ubunifu, thaqafa hii iliwainua na kuwafanya waiishi. Wakati matatizo yalipotishia kusambaratisha ujuzi wao uliotangulia, thaqafa hii ilinyanyua elimu na ujuzi na kurithisha.

Wakati ambao thaqafa ya kimagharibi inajaribu kufuata baadhi, thaqafa ninayozungumzia ilikua ni dunia ya kiislamu kuanzia mwaka 800 hadi 1600, ambayo ilijumuisha dola ya Ottoman Empire (Khilafah uthmania) na sehemu za Baghdad, Damascus na Cairo, na viongozi wenye muamko kama Suleiman The Magnificent.

Ingawa hatujui deni tulionalo katika thaqafa hii lakini mchango wake ni mkubwa katika urithi wetu. Teknolojia ya viwanda isingekuwepo bila michango ya wanahesabu wa kiarabu. Viongozi kama Suleimani walitoa mchango mkubwa katika nadharia nyingi mfano ni ile inayohusu uongozi wa raia.

Na pia tunaweza kujifunza somo kupitia mfano wake : ni utawala ulioegemea katika meritocracy, sio kurithishana. Ni utawala wenye uwezo wa kumiliki idadi ya watu kama wakristo, waislamu na mayahudi.

Utawala huu uliokua na muamko -utawala ulisimamia utamaduni, kujimiliki, utu na ari_uliongoza miaka 800 ya ugunduzi na ubora wa kiwango.

Katika kiza na nyakati ngumu kama hii, nilazima tujibidiishe kujenga jamii na taasisi zenye malengo kama haya. Ni lazima tulenge katika umuhimu wa utawala_tujikite mikataba ya kiutawala.

Na Muhammad Imran

Maoni hayajaruhusiwa.