Mujtama’a na Madawa ya Kulevya.

Hakika utumiaji wa mihadarati na pombe ni jaribio la kiwango cha muamko ama kuporomoka kwa mujtama’a. Utumiaji wake ni jangaa kuu kwa njia zote na hurejesha nyuma jamii, huvunja mahusiano na maingiliano yote ya kijamii. Hubadilisha miji kuwa pori na wanadamu kudunika kushinda wanyama. Maadili mema kutokana na kujidhibiti mpaka subira, ukweli mpaka uaminifu yote yamepotea kwa sura ya jamii. Ikiweka nidhamu zote za mujtamaa kuanzia ya utawala, kisisasa, mahakama, usalama, uchumi na kadhalika katika hali tata.

Insha’Allah tutaangalia chanzo cha athari za mihadarati na kiwango gani mihadarati na pombe zimefisidi nidhamu yote. Wanadamu wako na mahitaji ya kiviungo na mahitaji ya kihisia, kushibisha yote hulazimisha nidhamu ambayo itakayoongoza, kupanga na kuwekea ratiba njia zote za kushibisha, nidhamu ambayo inawiyana na umbile la mwanadamu na sio ile inagongana nalo. Utu wa binadamu ni akili na nafsiya (kitabiya), kupima matendo na vitu vinavyo msukuma mwanadamu kufikia kutimiza hisia zake kupitia fikra maalum (itikadi).

Hivyo basi kurudi nyuma kwa mwamko ni matunda ya fikra maalum (nayo ni itikadi) inayo muongoza mwanaadamu katika kushibisha mahitaji yake ya kiviungo na kihisia.

Hali ilivyo sasa, kiulimwengu itikadi inayo tawala ni fikra za kidunia (secular) ambayo imetokana na nidhamu inayotabikishwa kama suluhisho la mas’ala jumla ya maisha. Fikra za kidunia (secular) zimekuja kama mazao ya suluhisho la kati na kati baada mapinduzi ya Europa. Mapinduzi yaliopatikana kupitia umwagaji wa damu yaliozaa fikra maalum kuhusu dini, maisha na siasa; kumvua ubwana Muumba wa mwanadamu, maisha na ulimwengu na kumpa mwanadamu cheo hicho.

Ubwana katika itikadi ya kidunia (secular) nikuwa mwanadamu yuko na uweza wa kujitungia sheria na kujiamualia zuri na baya kinyume na mafundisho ya Mola. Hizi ni fafanuzi/taarifa za kimakosa zinazotokamana na fikra za wanadamu ambazo zinatofautiana kiuwezo wa kiakili ambayo ni kinyume na hugongana na asili ya mwanadamu.

Kwa mfano furaha ni nini? furaha kama hisia za mwanadamu hazina ufafanuzi wa wazi, lakini katika itikadi ya kidunia (secular) kutafuta furaha kumewafanya watu kujitosa kwa kila aina ya vitendo kufikia kilele cha raha. Misemo kama “kua tajiri ama kufa ukijaribu (get rich or dying trying)” ama “fanya tu (just to it)” yamekua kama kumbukumbu ya matendo ya kufikia furaha.

Fikra za uhuru zimetengeza jamii isiowajibika na kucha hufanya juhudi ya kutafuta raha ambayo ni yakidanganyifu badili ya kweli. Kuamini kuwa kujiridhisha kimwili na kumiliki vitu ndio funguo za kupata kilele cha furaha; athari zake ni mkazo wa kihisia (stress) wa hali ya juu, huzuni na uchovu na zimekua ni sononeko la kiulimwengu likizalisha kukata tamaa na fikra ya kukwepa kutoka hali halisi iliyo na dhiki kwa kutafuta vishuhuli na afuweni kutokamana na ukweli usio ridhisha kupelekea watu kwa jamii kujitosa kwenye mihadarati na ulevi. Hii ni katika upande wa mzizi wa haya kuwa ni itikadi ya kidunia (secular), lakini kuna sababu nyengine  ikiwemo uraslimali kama mfumo wa uchumi wa itikadi ya kidunia (secular), mfumo uliokusanya utajiri kwa mikono ya wachache, shirika la OXFAM lilitoa ripoti ya watu wanane wenye umiliki wa utajiri wa hali ya juu kushinda zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni (bilioni 3.6) ikizaa hali kukata tamaa ya kiuchumi. Kudhibiti mali kwa mikono ya wachache nikukanusha nadharia ya fikra ya “kuwa wenye mali ama mashirika makubwa yakinufaika basi jamii yote hunufaika (trickledown theory)” kuwa ni fikra isiowezekana na ya kiuongo. Vipimo vya matendo katika itikadi ya kidunia (secular) ni maslahi na faida, na kwakuwa mihadarati kama “bidhaa ya kiuchumi” huleta faida kubwa kupitia ulanguzi wa madawa ya kulevya. Magenge ya wauzaji mihadarati wakishirikiana na wafanyikazi wa serikali nao ni wanausalama, wanasheria na mpaka wakuu watendaji wa nchi kushirikiana na kuunda vikundi vya mashirikiano katika kueneza mihadarati. siajabu imechkua Amerika zaidi ya miaka 100 mpaka leo kupigana vita juu ya walanguzi wa madawa ya kulevya bila ishara yoyote ya kushinda vita hivi bali uongezeko wa uzalishaji na mahitaji yake kufanya ulanguzi wa madawa kuna ndio sekta inayoongoza ya kIuchumi miongoni mwa sekta nne zinazo ongoza ikiwemo mafuta, silaha na sekta ya urembo. Katika uchumi wa kiraslimali, mihadarati na pombe huchukuliwa kama sehemu asili ya nidhamu ya kimaisha. Uchafu wa mihadarati kihakika ni matunda ya uraslimali.

Nidhamu ya kijamii katika itikadi ya kidunia (secular) imefeli pakubwa katika kufafanua majukumu msingi ya mwanamume na mwanamke katika maisha ya ndoa na mjumuiko wa kijamii ambapo kumejenga pengo kubwa katika malezi na majukumu ya kijamii. Badala  yakuwa na kizazi kinachoenda sambamba na vizazi vya nyuma bali tunavyo vizazi vya kuzorota, viumbe vigeni badili yakuwa ni vizazi. Heshima, maadili na kujali imetoka katika malezi. Malezi yakawa ni kulisha, kuvisha, kupeleka watoto shule bila malezi ya wazazi ambayo yako mbali na kulea kizazi cha kuwajibika.

Itikadi ya kidunia (secular) inafafanua jamii kama mkusanyiko wa watu wenye fikra, rai na maslahi tofauti, na unakuza uwingi na ubinafsi kiasi yakuwa makundi na watu wenye maslahi tofauti kuamini wamedhaminiwa kama makundi ya mashoga, vyama vya kisiasa, na dini lakini ikiambatana na msingi wa kidunia (secular) wala sio kugongana.

Fafanuzi hii ya kimakosa imetengeze watu kwa misingi ya kiubinafsi na kimakundi kwenye jamii inayojali mas’ala ya kiubinafsi na kuacha jukumu la jumuia kwa serikali.

Ndio Uislamu unachukua uchafu huu kama mama wa maovu yote kama vile Mtume (saw) alivyosema

“Tembo (vilevi) ni mama (mzizi) wa machafu”.

Ni wajibu wa mujtama’a wa kiislamu jumla kuamrisha mema na kukataza maovu. Allah (sw) asema:

﴾وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٤

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa”

[Al-i’Imran: 104]

Jukumu ni la kijamii na kisiasa pale jamii itakapowahisabu wenye kufanya maovu haya na wakati huo huo kuhisabu uongozi wa serikali kutekeleza jukumu la kuondoa uovu huu kutoka kwa mizizi yake nayo ni uzalishaji. Sheira ya kiislamu imeeka sharia kali kwa wanye kupatikana na hatia kwa Nyanja zote za muovu huu na kuweka adhabu kali kwa wenye kueneza ufisadi, kuzalisha na kusambaza mihadarati na kuweka mpaka adhabu ya viboko themanini kwa walevi wanaoleta machafuko hadharani.

 

Na Ali Omar

Inatoka Jarida la Uqab: 3

https://hizb.or.tz/2017/04/01/uqab-3/

Maoni hayajaruhusiwa.