Mikopo ya Masomo

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Kuna baadhi ya vijana hawana uwezo wa kulipa gharama za masomo ya chuo kikuu, na serikali inawakopesha, mwanzoni mikopo hii haikuwa na riba , kisha ikatangazwa kuwa itakuwa na riba asilimia sita 6% kwa madai ya kuporomoka thamani ya shilingi ya Tanzania ukilinganisha na dola ya Marekani, ni sawa wale waliopewa mkopo kabla au baada ya tangazo kutolewa watalipa pamoja na riba , ni kwa namna gani tuamiliane nao na wafanye nini wale waliochukuwa mkopo kabla ya tangazo?

Jibu:

Hakika wewe umetaja kwenye swali lako hali mbili:

1 – Hali ya kwanza: Watu waliochukuwa mkopo toka serikalini kwa masomo ya chuo kikuu kwa sharti kwamba walipe deni pasina ziada, yaani hawakuchukuwa mkopo wa riba…… Lakini serikali baada ya hapo imetoa agizo la kulazimisha kutoa asilimia 6%  sita ziada ya mkopo ambao wamechukuwa kwa hoja ya kuporomoka thamani ya shilingi mbele ya dola ya Marekani….. Katika hali kama hii serikali ndio itapata madhambi kwa sababu ndio iliowalazimisha wanafunzi wa chuo kikuu walipe zaidi ya vile walivyochukuwa. na wala hiyo sio riba kwa upande wa wanafunzi, bali ni katika jumla ya kama kodi zinazowekwa serikali kwa raia, na kwasababu hiyo hawana madhambi wanafunzi ikiwa wataamua kutekeleza agizo hili la serikali, pamoja na ziada ambayo imewekwa na serikali, na serikali ndio itapata madhambi katika jambo hilo, kwa sababu inachukuwa mali za watu pasina haki.

2 – Hali ya pili: Watu ambao wamechukuwa mikopo toka serikalini kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu na hali ya kuwa wanajua kuwa watalipa na ziada ya asilimia 6% kwa kuwa serikali imeweka sharti hilo kwa hoja ya kuporomoka  thamani ya shilingi mbele ya dola…. Katika hali hii unakuwa huu ni mkopo wa riba na watapata madhambi wote wawili mkopeshaji ambaye ni serikali na mkopaji ambaye ni mwanafunzi…

Ama namna ya kuamiliana na watu wa hizi hali mbili wakiwa ni Mashababu, wale waliochukuwa mkopo kwa mujibu wa hali ya mwanzo, hao hawana madhambi na wala hakuna hatua zozote za kiidara zitakazochukukuliwa dhidi yao…. ama wale waliochukuwa mkopo kwa mujibu wa hali ya pili, hakika itakuwa wamechukuwa mkopo wa riba na wanapata madhambi, katika hali hii pindi zikitufika habari kuwa mmoja wa Mashababu (Walimu) kuwa kachukuwa mkopo wa riba, basi tutachukuwa katika haki yake hatua za kiidara zenye kufaa, na tutamtaka aepukane na mkopo huu kwa haraka  sana iwezekanavyo.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashta

Maoni hayajaruhusiwa.