Miezi Mitukufu ndani ya Mwaka

2

Hili ni swali linaloweza kumpitikia mtu yoyote ndani ya nafsi yake kwa kuzingatia mtazamo mdogo wa macho ya kibinadamu kuwa miezi yote mbona iko sawa sasa ni vipi mengine kuitwa mitukufu ilihali yanaonekana mbona mambo yote kuwa sawa khususani katika kipindi hichi cha mwanzoni mwa mwezi wa Dhul-hijja ambao nao ni miongoni mwa miezi 4 mitukufu aliyoitukuza Allah Taala pale aliposema ndani ya surat Tawba -:

إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ.

Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah Taala ni kumi na mbili (12)katika hukmu ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, (iko miezi) mine(4) mitukufu. Hivyo ndiyo Dini iliyo nyooka. Basi msijidhulumu nafsi zenu (kwa kufanya maasi) ndani ya miezi hiyo, na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita . Na jueni kwamba Allaah Taala Yu pamoja na wacha Mungu.

[At-Tawbah: 36]

Kwa kuangalia makusudio ya  Allah (s.w.t) aliyoyaeleza mwenyewe  katika Kitabu chake kitukufu cha Qur-an ni kwamba idadi ya miezi ni kumi na mbili na iko kihakika katika nidhamu ya ulimwengu wa kimaumbile, kwa kufuata mzunguruko wa dunia kila siku katika njia yake wa kuizunguka jua na mwezi. Wala haitokei siku ikaenda kinyume na nidhamu hio katika maisha yote wanayoishi wanadamu.

Makusudio ya siku alipoumba mbingu na ardhi ni kwamba yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu aliumba ulimwengu wenye utaratibu maalum wa muda wa masaa na vipindi mbali mbali vya kubainisha majira, yaani idadi ya miezi hii, sio kwamba imewekwa na binadamu na ugunduzi wake; isipokuwa ni desturi na nidhamu ya maumbile.

Kimsingi ni kwamba binadamu hupima wakati  na kuupanga kwa anavyoona na kuhisi. Tukiangalia maumbile ambayo yatatuongoza katika kujua wakati, hatupati zaidi ya jua na mwezi. Jua kila siku linakwenda kwa mfumo mmoja kutoka mashariki na kutua magharibi, bila ya kuweko tofauti.

Kupitia hilo jua twajua wakati wa asubuhi mchana na jioni, na wala halihusiki na kujua mwezi si kwa karibu wala mbali. Lakini mwezi ni kinyume na hivyo. Huwa unajitokeza kwa picha maalum kuanzia siku ya kwanza ya kuandama kwake , ambao ndiyo siku ya kwanza ya mwezi. Tunapojua mwezi ndio tunajua mwaka.

Anasema Razi: Desturi ya Waarabu tangu zamani ni kuwa na mwaka wa mwezi na sio wa jua .Hukumu hii walirithi kutoka kwa Ibrahim na Ismail AS . Vile vile Mtume (s.a.w) amebainisha wazi miezi hio minne (4)mitukufu pale aliposema kupitia hadithi aliopokea Abubakar kwa kusema.

عن أبي بَكْرَةَ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنه قَالَ:  ((إن الزَّمَانَ قَدْ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ ذُو الْقَعْدَةِ وَذُو الْحِجَّةِ وَالْمُحَرَّمُ وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشَعْبَانَ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Bakr ra kwamba Nabii Muhammad saaw amesema: “Hakika mgawano wa zama umerudi katika hali yake ya asili siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili; mine(4) miongoni ya hiyo ni mitukufu, mitatu(3) inafuatana pamoja; Dhul-Qa’adah, Dhul-Hijjah na Muharram, mwengine ni Rajab wa (kabila la) Mudhwarr ambao uko baina ya Jumaadaa na Sha’baan”

[Al-Bukhaariy na Muslim]

Imaam Atw-Twabariy amesema: “Katika miezi yote kumi na mbili Allaah swt ameichagua hii minne na Ameifanya kuwa ni mitukufu na kusisitiza kuitakasa, na kwamba dhambi zitakazofanyika humo ni zaidi na hali kadhalika thawabu za ‘amali njema zinakuwa maradufu na zaidi.

Qataadah amesema kuhusu kauli ya Allah swt:

فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ

“Basi msidhulumu humo nafsi zenu humo.”(9:36)

Dhulma itakayotendeka katika miezi mitukufu ni mbaya na kubwa (au khatari) kuliko dhulma itakayotendeka katika miezi mingine. Hakika dhulma daima ni dhambi lakini Allah swt hufanya baadhi ya vitu kuwa ni vizito kuliko vingine vile Apendavyo. Akachagua baadhi ya viumbe vyake na baadhi ya vitu kuwa bora zaidi kuliko vingine. Amechagua Wajumbe kutoka Malaika na kutoka wanaadamu.Na mwanadamu kufanya amali za kheri ndani ya miezi hiyo kwa mujibu wa uislamu zina malipo maradufu pia . Tujitahidi kila mmoja wetu kujikita kufanya amali za kheri ndani ya miezi yote 12 lakini tuzidishe zaidi ndani ya miezi hiyo mitukufu.

Vile vile Amechagua baadhi ya kauli Zake kuwa ni bora kuliko nyingine, Misikiti kuwa bora kuliko sehemu nyingine za ardhi, Ramadhaan na miezi mitukufu kuwa bora kuliko miezi mingine, siku ya Ijumaa kuwa ni bora kuliko siku nyingine, na usiku wa Laylatul-Qadr kuwa ni bora kuliko masiku mengine. Kwa hiyo itakase vile Alivyotakasa Allah, kwani kufanya hivyo ni vitendo vya watu wenye akili na wenye kufahamu” [Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]

Miongoni mwa yaliyokatazwa katika miezi mitukufu ni kama Anavyosema Allah swt :

  يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللَّـهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu kupigana humo. Sema: “Kupigana humo ni dhambi kubwa, lakini kuzuia (watu kufuata) njia ya Allah na kumkufuru Yeye na (kuzuia wasiende) Al-Masjidil-Haraam na kuwatoa watu wake humo ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua.” Na wala hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakutoeni katika Dini yenu wakiweza. Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeporomoka ‘amali zao katika dunia na Aakhirah. Na hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu. 

[Al-Baqarah:  217]

Hivyo ni jukumu kwa umma wa kiislam kuiheshimu miezi hii mitukufu na kuipa heshima yake kama yalivyo matukufu mengine ya uislam ambayo yampasa kila muislam kuyapa heshima inayostahiki kama vile kutokufanya yale yaliokatazwa kama Allah alivyo sisitiza kama vile kutokudhulumiana kwa namna yoyote ile iwe kwa wizi, utapeli au mauaji baina ya waislam.Na ni dhihirisho la wazi kuwa miezi hii mine (4) ina utukufu wa pekee ndani ya idadi ya miezi 12 iliyobakia ukitoa mwezi wa Ramadhani ambao utukufu wake ni zaidi ya miezi yote iliyomo katika mwaka mzima.

SULEIMAN KHAMIS (JAULA)

2 Comments
  1. gygienede says

    success rate of clomid Because there are multiple activities occurring throughout the simulation and students may be focused only on their specific roles, debriefing can be used to review key points about the simulation

  2. slidova says

    where can i buy zithromax Overexpression of Treg related markers and higher activity of Treg cells affect the immune system in female breast cancer patients

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.