Bei ya Karafuu ni Hafifu Zanzibar na Baadhi ya Wakulima Wanyang’anywa Eka

9

Karafuu ni miongoni mwa jamii ya mazao ya viungo (spices). Asili ya zao hilo kuingia Zanzibar  ni kutoka visiwa vya Molucca ambayo leo inajuilikana kwa jina la Indonesia mapema mwa  karne ya 20 . Utawala wa Kisultan wa Oman uliokuwa wakala wa utawala wa Muingereza ndio uliofanya juhudi kubwa ya kuotesha miche ya mikarafuu . https://en.wikipedia.org/wiki/History_of_Zanzibar

Kisiwa cha Pemba ndicho hadi hii leo chenye mikarafuu mengi kutokana na mfumo wa hali ya hewa na kijiografia ukilinganisha na Kisiwa cha Unguja. Pemba ina milima mingi na mabonde na inapata 80” ya mvua kila mwaka wakati Unguja ni tambarare na inapata 60” ya mvua kila mwaka . Pemba imekuwa mzalishaji mkubwa wa Karafuu ulimwenguni lakini mabadiliko ya uongozi na utawala ya Zanzibar  ya kufuata mfumo wa majaribio wa siasa ya ujamaa wa Kiafrika yaliwakera wakubwa wa dunia licha ya kwamba Mapinduzi ya Zanzibar  yalifanikishwa na Muingereza na hata huo Muungano ulitengenezwa na Marekani kukidhi maslahi yao ya kisiasa na ya ukoloni.  https://en.wikipedia.org/wiki/Zanzibar_Revolution

Kutokana na historia niliyosimuliwa na Mbunge mstaafu wa CCM, Bwana Ame Mbarouk Ussi, wakulima wa karafuu walinufaika sana huko nyuma kwani waliunda muungano wa wakulima wa karafuu ulioitwa CGA 1956 (Clove Growers Association). Umoja huo ndio uliokuwa ukipatana  bei na Serikali na hata misaada ya kumsaidia mkulima (subsidies). www.biblio.com › Dendera

Baada ya vita vya pili vya dunia , mahitaji ya karafuu duniani yalikuwa makubwa kama  ilivyokuwa kwa bidhaa nyengine kutokana na uharibifu wa vita. Kipindi hicho maarufu kinajuilikana “batileti”(historia ya kusimuliwa)na wakulima walinufaika kupindukia kwa karafuu zao kupata bei kubwa. Ilikuwa ni mwaka wa kuvigeuza visiwa vya Zanzibar hasa Pemba kuwa vya maendeleo makubwa badala yake vikaambulia umasikini uleule waliotokana nao nyuma kutokana na sababu tatu kuu.

Ya kwanza ni mila na desturi ya watu wa visiwa vya Zanzibar  wa kuendekeza matumizi ya kipuuzi ya kushindana kwa  karamu zilizoambatana na ushirikina pamoja na matanuzi mengine(lavish expenses).

Ya pili ni mipango ya wakoloni ya kutowasimamia watawaliwa wapate maendeleo na ustawi wa kutosha ili wabaki wanyonge na mawazo finyu ya kutoshughulika na athari ya wakoloni hao .

Ya tatu wakulima kuchukuwa mikopo yenye riba kubwa ya 70% kutoka kwa wakopeshaji matajiri wa Kihindi . Baada ya kushindwa kulipa madeni yao , mashamba hayo yalifilisiwa. Huu ni mpango mbaya wa serikali ya kikoloni kuweka Amri ( decree ) ya 1912 iliyoruhusu uanzishaji wa maduka ya poni.

Kwa kuhofu ya kutokea machafuko ya kisiasa , Serikali ya Kikoloni ilimwita mtaalamu kutoka Uganda John Kerr kusaidia kutatuwa tatizo la madeni makubwa ya wakulima wa mashamba ya karafuu , na yeye akatoa rai yake ya kuanzishwa jumuiya za muawwana (SACCOS) (“Zanzibar Archives- John Kerr commission report of 1950 for establishing savings and credit societies in Zanzibar”).Hata hivyo jumuiya hizo hazikudumu baada ya kupigwa marufuku na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1965.

Mabadiliko ya kiutawala yameathiri sana uzalishaji wa zao la karafuu . Tokea yatokee mapinduzi ya 1964, mkulima wa karafuu amekuwa kama mtumwa wa mali yake baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika miaka ya 60 na 70 kudhibiti soko la karafuu na bei kupitia shirika lake la ZSTC ambalo halina sera ya kumuinua mkulima kiuchumi isipokuwa lugha ya kisiasa kama inavyosimuliwa na mamlaka ya shirika hilo . Ilikuwa kipindi chote cha miaka takriban 40 mkulima alikuwa akilipwa na ZSTC wastani wa Tsh15 kwa kilo  ($2, )1970’s. springer.com/content/pdf/10.1007/BF02930706 .Na ($2.15)1980’s ,www.reuters.com/article/ozabs-zanzibar-cloves- .

Wakati  bei ya soko la dunia haikuwa na mabadiliko makubwa kama ilivyo sasa .Bei ya US$ ni wastani waTsh 7.17 (1970 na 1980) https://www.indexmundi.com/facts/tanzania/official-exchange-rate .

Ni miaka 6 tu nyuma ndio bei ya mkulima imeongezwa kidogo. ZSTC imetoa taarifa kuwa mwaka 2016  ZSTC  imenunuwa tani 5745 za karafuu kavu na kumlipa mkulima Tshs 14,000 kwa kilo kwa karafuu za daraja  ya juu. www.informationvine.com/zanzibar+cloves.

Katika soko la dunia bei ya karafuu ya Zanzibar kupitia wakala wake Feroz OLIA Shehnaze Trading Pte.Ltd  ni  US $ 21000 kwa tani ambazo ni sawa Tshs 48,300 kwa kilo na ZSTC  inamlipa mkulima kwa wastani wa  Tshs 12,000 na 14,000 kwa kilo. Hii inamaana mkulima angeliuza karafuu zake kwa yo yote kwa bei ya US $ 21 kwa kilo sawa na Tshs 48,300 .Yaani Serikali inapata faida mara 4 ya mkulima. www.alibaba.com/showroom/price-of-cloves.htm

Kuondoa misaada kwa wakulima , kuweka vizuizi  vya udhibiti wa karafuu kwa kutumia vikosi vya ulinzi (KMKM) na hata watu kupoteza maisha au kubaki vilema  kwa kuanguka chini  bila msaada wa kutosha kutoka serikalini  limeathiri uzalishaji wa karafuu na sasa Zanzibar  ni ya tatu ulimwenguni badala ya nafasi ya kwanza iliyokuwa nayo zama za ukoloni. articles.latimes.com › Collections › Economy

Lakini leo hii mkulima amerudi nyuma zaidi kuliko zama za mkoloni mkongwe na utawala wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  umezidisha mbano wa wakulima kutopata manufaa ya kutosha kwa karafuu zao.Hivi sasa Serikali imetamka wazi na imeshachukuwa hatua ya kuwanyang’anya zile eka tatu  inazonadi na kujilabu kila inapofikia kilele cha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari ya kila mwaka. Cha kujiuliza Serikali imesibiwa na nini? Au ni muendelezo ya kuwabana wakulima wasisafarishe magendo ya karafuu nje ya kisiwa cha Zanzibar ? au imeanguka kiuchumi ? Lakini kikubwa na huzuni ya wakulima waliopewa mashamba hayo  miaka nenda miaka rudi , wakiishughulikia na kuigharamia kwa fedha nyingi , tahamaki wananyang’anywa bila ya kufidiwa nguvu na gharama zao . licha ya kuwa mashamba hayo asili ni ya wakulima na serikali ili yapora  kisha kuyagawa kiholela sasa ina yapora tena

Uislamu ni mfumo wenye kukidhi hitajio la kila mtu kwa zama na wakati wote. Katika uislamu mashamba yanayofilisiwa ambayo yanamilikiwa kibinafsi  ni yale yaliyokosa kuimarishwa kwa zaidi ya miaka tatu.Pili katika milki ya mtu binafsi mtu anaruhusiwa kuuza mali yake atakavyo bila kuingiliwa na dola ilimradi mauzaji hayo yatimize vigezo vya sharia kihukmu . Lakini tunaona jinsi watawala katika mfumo wa kidemokrasia wanavyo wanyonya na kuwanyanyasa kupindukia watawaliwa.

Kumbe tatizo si kuwaondoa wakoloni . Tatizo msingi ni mfumo mchafu unao wapa thaqafah chafu watawala kuwa wakandamizaji. Kwa hivyo mtawala yoyote anayetokana na mfumo huo thaqafa yake ni kuwandamiza wanyonge. Shime tufanye juhudi ya kuirudisha khilafah ije itukomboe ummah unaangamia.

Na Suleiman Mbarouk(Ticha Sule)

9 Comments
  1. For the reason that the admin of this site is working no uncertainty very quickly it will be renowned due to its quality contents.

  2. Live TV says

    You have noted very interesting details! ps decent web site.Live TV

  3. live streaming horse racing says

    For the reason that the admin of this site is working no uncertainty very quickly it will be renowned due to its quality contents.-shopping queen online ansehen

  4. hey dudes for girls says

    But wanna say that this really is quite helpful Thanks for taking your time to write this. – hey dudes near me

  5. Definitely what a great blog and instructive posts I definitely will bookmark your site.All the Best! .

  6. here says

    I wish I could experience such beauty in person! read review

  7. Kristofer D says

    I like this weblog very much, Its a really nice position to read and receive info.Blog monry

  8. Rackel says

    If you are going for finest contents like myself, simply visit this
    site all the time since it offers feature contents, thanks

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.