Kumbukumbu Yangu Kwa Yona Fares Maro

1

Yonas Fares Maro https://www.facebook.com/profile.php?id=100012677088799

Amefariki dunia na kuzikwa Jumatatu tarehe 15 Januari 2018 kijijini kwao Mowo, Moshi. Yonas Fares Maro atakumbukwa sana kwa kuwa ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa kundi /group maarufu la facebook linalojulikana kwa jina la Ulinzi na Usalama. https://www.facebook.com/groups/ulinzinausalama/about/ .

Kupitia kundi hilo tuliweza kujifunza mambo kadhaa kupitia makala mbalimbali zikiwemo pia tahadhari za kiusalama. Mbali na hilo, pia Yonas  kwa kuwa alikuwa mweledi wa masuala ya fani ya IT mara nyengine alikuwa mwandishi wa masuala ya teknohama na masuala ya kijamii ndani ya gazeti la Mwananchi.

Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, Yona Fares aliamua kujitoa uhai wake baada ya kukata tamaa na mgogoro wa muda mrefu ndani ya ndoa yake, huku akiacha ujumbe nyuma yake unaosomeka:

“Nimekuwa kwenye matatizo ya ndoa kwa miaka 4, kila wiki nikipambana na mke mlevi na mzinzi.
“Tukio la jana usiku na leo asubuhi limenisononesha na kunitia simanzi kubwa. Nimekata tamaa ya kila kitu na kila jambo nangoja mapenzi ya Mungu tu. Nalazimika kutumia dawa za usingizi lakini wapi. Sasa nipumzike ………..”

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=436003433485472&id=141069916312160

Nilijuana rasmi na Yona Fares Maro ndani ya mwezi Juni, 2015, baada ya Yona kuitumia makala yangu moja kwa jina lake kisha makala ile kuchapishwa kwa jina lake ndani ya gazeti la Mwananchi. Makala ilibeba anuani : ‘Mtazamo thabiti juu ya sakata la ulevi wilayani Rombo’

Makala ile niliandika kutokana na sakata la kukithiri kwa ulevi wilayani Rombo, kiasi cha kupelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa mahusiano ya ndoa katika jamii wilayani humo. Kwa kumbukumbu ya Yona Fares Maro naiweka tena makala hiyo: https://www.facebook.com/permalink.php?story_fbid=405355259878160&id=100012110684395

Halikuwa jambo jema kutumia makala ya mtu mwengine kwa jina lako, lakini nilithamini tabia njema aliyokuwa nayo Yonas Fares Maro ya kuwa na hamu ya kusoma na kujifunza kutoka kwa wengine. Na kitendo cha kupachika jina lake kwenye makala yangu ambayo ilipatikana ndani  ya mitandao ya jamii ni dalili ya hilo. Kwa kuwa asingekuwa msomaji na mfuatiliaji kamwe asingeiyona makala ile.

Baada ya ndugu yangu mmoja kunipatia nakala ya lile gazeti la Mwananchi nakuona kwa macho yangu ile makala yangu ikiwa na jina la Yona Fares Maro, nilimpigia simu na kumueleza malalamiko yangu juu ya suala lile, Yonas hakuonesha upinzani, hivyo nikamtaka tuonane ana kwa ana, na akakubali.

Kwa mara ya mwanzo nilimkaribisha Yonas Fares Maro nyumbani kwangu, tukaongelea kuhusu ile makala yangu na namna alivyoitumia kwa jina lake, Yonas akanieleza kuwa alifanya vile kwa dhamira njema ya kuusambaza ujumbe ule ufike kwa hadhira kubwa zaidi.

Nikamtanabahisha Yonas Fares Maro kwamba nia njema, ni vyema iambatane na kitendo chema. Hata hivyo, Yonas Fares Maro aliomba radhi kwa unyenyekevu nami nikamsamehe, tukakhitimisha na kufunga mjadala wa lile, na tukaanza kuzungumzia masuala mengine, kubadilishana mawazo hususan juu ya tasnia ya habari na uandishi kwa ujumla.

Tukio hilo baina ya mimi na Yona likawa mwanzo mwema wa kufungua milango wazi, ukaribu na mawasiliano baina yetu. Ikawa mara kadhaa hubadilishana nae mawazo kupitia inbox ya fb kuhusiana na qadhia mbalimbali.

Kwa masikitiko makubwa Yonas Fares Maro ametutoka baada ya kuelemewa na mgogoro wa ndoa, ilhali makala yangu ambayo aliisoma na kuipenda ingemtosha kumpa suluhisho mwanana kutokana na mashaka na mgogoro wa ndoa uliomsibu kiasi cha kumpelekea kukata tamaa. Kwa kuwa makala ile iligusia kwa kina juu ya mambo mawili makubwa, yaani janga la ulevi na masuala ya mahusiano ya kifamilia. Mambo yaliokuwa changamoto nzito zilizozingira ndoa yake.

Yonas Fares Maro umetutoka daima tutakukumbuka.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

24/01/2018

1 Comment
  1. gygienede says

    We work with many out- of- town patients doing embryo adoption cycles at the National Embryo Donation Center here in Knoxville or with any of the other local clinics tamoxifen gynecomastia before and after

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.