Khilafah ndio mkombozi wa Wanawake- No.2

0

Mwanamke ndani ya Ubepari

Ubepari au urasilimali ndio mfumo unaongoza dunia ya leo takribani nchi zote duniani. Nchi zote zinafuata mfumo huu, fikra na ndihamu zake za kimaisha. Ni mfumo ambao umejengeka katika  nidhamu ambayo huhimiza ulimbikizaji wa mali nyingi chini ya mtu mmoja(urasilimali).

Ubepari kama mfumo ulipitia karne kadhaa toka kuzaliwa kwake mpaka kufikia kwenye hatamu ya uongozi wa kifikra wa kiulimwengu chini ya ulezi wa nchi za kimagharibi .

Kipimo cha ubepari ni faida na hasara. Kwa hiyo mwanadamu ndani ya mfumo huu hufanya matendo yake kwa kipimo cha faida na hasara. Ndani ya mfumo huu jambo laweza kuhalalishwa ilihali ya kuwa linaweza likaongeza mapato. Ndio maana vitu kama ulevi umehalalishwa kuuzwa madukani kwa kuwa kuna faida kubwa ndani yake ya kibiashara . Bila ya kuzingatia madhara yake. Mfumo huu haujali afya wala murua wa wanadamu kwa kuwa pombe  ina faida kubwa. Na haujali afya za wanadamu kwa kuwa hauna kipimo cha ubinadamu. Kipimo cha ubinadamu na dini, ama fikra ya kuwa kuna maisha baada ya kifo na kila kitendo kitalipwa baada ya kifo kwao hakiko. Kipimo kama  hakuna katika mfumo huo na  wala hakuangaliwi ubinadamu wala usawa. Bali kinachoangaliwa ni maslahi tu na ndio maana unaweza ukakuta mali ya umma inamilikishwa mtu binafsi bila ya angalizo lolote.

Mwanamke katika mfumo huu anatumiwa kama mojawapo ya nguzo muhimu ya kuutangaza mfumo huo dhalimu na biashara. Mwanamke ndani ya ubepari hunyimwa haki zake za msingi na hudanganywa  kwa wito kadhaa wa kibepari inaolenga kuendelea kutabikisha mfumo. Miito mingi inayolenga kuendeleza uwepo wa mmfumo huu dhalimu hupewa wanawake waifanyie  kazi hiyo. Kwenye kampeni nyingi za kuupigia debe mfumo huu huwachukua wanawake na kuwaweka mbele katika  kuupigia debe mfumo huo.

Aidha, mwanamke ndani ya mfumo huu amekuwa anatumiwa kama chombo cha starehe na kivutio cha biashara. Kwa hakika mwanamke amekosa thamani katika mfumo wa kibepari.

Ingawa baadhi ya mufakiruuna wa kibepari hulipinga dai hilo. Vipindi vya vyombo vya habari, nyimbo za muziki na aina nyingine ya taarifa huwaamsha umma kuwatumia wanawake  kama chombo cha starehe. Hutumiwa kutimiza haja za wanaume halafu baada ya hapo hutelekezwa. Nyimbo za mziki huwalingania wanaume kutafuta wanawake kuwatumia baada ya hapo kuwatekeleza, cha kushangaza wanamuziki hao wengi wao ndio hupewa tuzo za wanamuziki bora. Na wale wanaojiita wanaharakati wa kutetea haki za wanawake huwashukuru wanamuziki wao kuchochea utumikishwaji wa wanawake kama vyombo vya starehe. Ndani ya ubepari tunashuhudia vilabu vya usiku vya wanawake  wacheza uchi nakila siku zinapoongezeka ndivyo madanguro yanavyoongezeka. Madanguro  hayo huweza kujitambulisha kiwazi ama ya kutumia majina tofauti kama sehemu za ‘massage’. Lakini hiyo ni jina tu ila matendo yanayotendwa humo ndani ni kuwatumikisha wanawake hasa mabinti wadogo katika biashara hizo kwa mujibu wa sheria  chini ya mwamvuli wa demokrasia kupitia uhuru wa kibinafsi wa kutenda anayotaka mwanadamu.

Hao mabepari kwa kuwa kipimo chao ni maslahi basi huruhusu utumikishwaji wa mwanamke kama chombo cha starehe ilimradi tu wapate maslahi. Mapato yanayotokana na kumbi za starehe  ni makubwa sana na yanachangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa kibepari.

Mwanamke ndani ya ubepari anaitwa na kulaghaiwa kwa miito mingi ambayo ni ulaghai. Kama kaulimbiu ya haki za binadamu, haki za wanawake, usawa wa kijinsia n.k. Miito hii imehamasisha mwanamke kuacha kazi yake ya asili ya ulezi wa watoto na familia nzima. Miito hii imempatia na imempelekea mwanamke kukandamizwa kupita mipaka na mwishowe kujikuta anashindwa hata kutimiza majukumu yake ya nyumbani na hatimaye watoto wengi kukosa uangalizi wa mama zao.

Ongezeko la vituo vya kushinda watoto wadogo (day care centre) ni ishara ya kuwa mama wengi hawashindi nyumbani kulea watoto wao. Ingawa kuna harakati nyingi zinazompigania mwanamke, ila usawa bado haujapatikana katika mambo mablimbali ikiwemo masuala ya ajira ambapo utakuta idadi kubwa ya wanawake wanalipwa kiasi kidogo cha malipo ukilinganisha na kazi wanaoifanya. Hali zao kiafya pia huathiriwa na mazingira ya kazi wanayofanyia kazi na mwishowe huwa na afya mbovu. Katika jamii za kibepari mwanamke hutumika kama bidhaa nyingine na huwa na thamani duni zaidi ya kuliko hizo bidhaa nyingine.

Mwanamke mwenye mafanikio ndani ya ubepari hupimwa kuwa na uwezo   kifedha, elimu ya juu, mzuri, mwembamba mrefu na kadhalika. Watu kama Michelle Obama mwenye kazi nzuri na kuwa mama wa watoto 2 na mke wa raisi hufanywa kiigizo/kioo cha jamii. Sambamba na hilo dhana ya mke kumtegemea mume wake ama baba yake basi huonekana ni daraja la chini. Kuwa mama wa nyumbani yaani kuwa mke bila ya kazi basi anahisabiwa kuwa duni  na kufeli. Wanawake huhisi unyonge pindi wanapoulizwa swali. “kazi yako ni ipi?”. Ugumu unaopata huonekana pale wanapojibu “mimi ni mama” au “mimi ni mama wa nyumbani”.

Aidha, katika ubepari mwanamke anatakiwa aoonyeshe maungo yake kwa namna ili watu wampime na kumthaminisha kama bidhaa zingine za kawaida. Ndio maana biashara za madanguro huhalalishwa ndani ya ubepari na hata kwa baadhi ya nchi zinalipiwa hadi  bima. Na urembo wa mwanamke ndani ya ubepari anatakiwa uonekane wazi  na ndio bishara ya uanamitindo, ulimbwende huwalipa wanawake pesa nyingi. Makampuni huwekeza fungu kubwa la fedha kwenye biashara hizo. Biashara hizo  zimevuka mipaka kuwachukua mabinti wenye umri chini ya miaka 18. Vile vile  wamekuwa wanasafirishwa kinyemela kutoka eneo moja kwenda jingine kufanyishwa kazi za ngono kwenye madanguro na mabaa mbalimbali.

Wanawake ndani ya ubepari hutapeliwa kwa wingi kupitia miito ya kitapeli ya kuwainua kiuchumi kama vile kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa( saccoss), ushirika na kadhalika. Ndani ya vyama hivi wanawake hudanganywa kuwa wakijiunga basi watafanikiwa kutatua matatizo yao ya kiuchumi. Huchangishwa michango mbalimbalina hupewa fursa ya kuweza kukopa ila kwa riba. Huelezwa kupitia mikopo hiyo wataweza kununua vitu, kujiendeleza kielimu na kadhalika. Ukiangalia suala hilo kwa kina utagundua kuwa wanawake hujitumbukiza katika matatizo  makubwa ya  kiuchumi  kwani kwa kujiunga na jumuiya kama hizo hujikuta mshahara wao mkubwa huishia kwenye kulipa madeni na sehemu ndogo sana hubakia kwa ajili ya matumizi yao binafsi.

Wanawake ndani ya ubepari hubakwa na kudhalilishwa kijinsia kwa kiwango kikubwa. Katika nchi zilizoendelea kuna idadi ikubwa sana ya kasi za udhalilishaji wa wanawake na matukio ya kubakwa kwa wanawake ni mengi sana. Kasi ya udhalilishaji wa wanawake na matukio ya kubakwa kwa wanawake ni mengi sana. Mfumo huu umewaonyesha wanawake ili wakubalike wavae viguo vifupi na kuonyesha maungo na mapambo yao. Mavazi haya huwavutia wanaume kimapenzi na baadhi yao hushindwa  kuvumilia na kujikuta wanawabaka. Vilevile katika mfumo huu wanawake hawakingwi kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi vingine, na hujikuta wakisongwa na msongo wa mawazo na baadhi yao huugua magonjwa ya akili na mwishowe kuwauwa.

Mauwaji ya  wanawake ni kitu cha kawaida sana kwenye mfumo wa kibepari na mfumo unashindwa kutatua tatizo hilo. Unyanyasaji wa kijinsia umekuwa ni jambo la kawaida sana kwenye mfumo wa kibepari. Wake za watu wengi sana huwa wameshakumbwa na vipigo toka kwa waume zao. Sababu za kupigwa kwao mara nyingi hutokana na ulevi nk. Mfumo wa ubepari hutegemea mapato mengi sana kutoka kwenye biashara za pombe na yatokanayo na ulevi huo. Ulevi ndio chanzo kikubwa cha vurugu za majumbani na ndio kichocheo  kikubwa kwa kuvunjika ndoa kadhaa.

Wanawake ndani ya ubepari hupewa kiini macho cha fursa za upendeleo kwenye masuala ya utawala. Karibia serikali zote za kiulimwengu zina fursa maalumu za upendeleo kwa ajili ya kuwainua wanawake. Vilevile hupewa fungu kubwa la serikali za kibepari ili kuingia kwenye nyanja hizi. Ila fungu hilo mara nyingi huliwa na vikundi fulani vya watu au familia kadhaa. Wanawake pia wanaopata hizo fursa za bure huwa ni wale wenye maslahi binafsi kwa baadhi ya watu waliopo kwenye serikali na huwa wanatoa rushwa za ngono ili kuzipata nafasi hizo. Kwani huwa ni nafasi zenye maslahi makubwa. Wakubwa kwenye serikali huamua kuwapa watu ambao ni wapenzi wao au walau wapambe au ndugu wa damu. Hata kama mwanamke ana taaluma ya hali ya juu inayomwezesha kushika nafasi hiyo ya juu ya utawala basi hapewi mpaka awe na mahusiano ya kimapenzi na mkubwa ndani ya serikali au awe na udugu wa damu na mmojawapo ya watu wakubwa kwenye serikali.

Vilevile hata kwenye ajira za kawaida wanawake hupata kazi kwa kutoa hongo ya hela ama kutoa hongo ya penzi.  Na huweza kufukuzwa kazi kama wakishindwa kutoa ngono pindi wanapokuwa tayari wapo kwenye ajira. Kwani mwanamke anaweza akaajiriwa bila ya rushwa ya aina yoyote lakini pindi anapokuwa yupo kazini huweza kujikuta anadaiwa atoe rushwa ya mapenzi na huwa anapokataa hufukuzwa kazi.

Wanawake ndani ya ubepari wanaathiriwa na lishe mbovu. Tunaona leo toka mfumo wa kibepari  uchukue hatamu za uongozi wa kimfumo. Idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wanakula vyakula ambavyo havina rutuba nyingi za kuweza kuimarisha miili yao kiafya. Na hili linatokana na kuwa ardhi inamilikishwa kwa watu wachache binafsi ambao ndio wenye mitaji mikubwa na kuacha wakulima wadogo wadogo kubaki na maeneo mengine madogo ambayo huwa na rutuba kidogo sana. Suala hili hupelekea bei ya vyakula kuwa juu kwani hao mabepari wakubwa kwa kuwa wamewekeza mitaji mikubwa na hivyo hutaka mizao yao ya vyakula iuzwe kwa bei kubwa ili warejeshe faida haraka haraka. Matokeo yake huonekana katika kipindi cha uzazi ambacho mwanamke huweza kujifungua mtoto mwenye matatizo mengi ambaye kitalamu ni kutokana na lishe mbovu hususan kipindi kile cha ujauzito. Watoto wengi wa naozaliwa nyakati hizi huwa na mapungufu ya kibaiolojia ambayo hutokana na ukosefu wa lishe bora na iliyo katika kiwango cha mizani.

Wanawake ndani ya ubepari hukumbwa na maradhi mbalimbali ambayo kwa namna moja ama nyingine husababishwa na uwepo wa mfumo wa kibepari. Mfano mzuri ni maradhi ya ngozi ambayo yanayowakumba wanawake wengi. Pia maradhi yanayopatikana kupitia matendo ya zinaa kama ukimwi, kaswende nk. Hii ni kutokana na fikra za kiuhuru ambazo amma huwahamasisha wao kujihusisha na zinaaa au kupitia waume zao ambao nao wameathirika na fikra hizo.

Wanawake huathiriwa na miito batili ya urembo/ulimbwende kupitia vyombo vya habari. Asilimia kubwa ya vipodozi vilivyo kwenye soko huwa na uwezo mkubwa wa kudhuru ngozi ya kinamama ila huwa hazipigiwi marufuku kwa kuwa biashara hizo huziingizia serikali mapato yanayotokana na makusanyo ya kodi. Makusanyo yanayotokana na kodi za vipodozi ni ndogo ukilinganisha na gharama ambazo hutumika kugharamia matibabu ya maradhi hayo.

Wanawake ndani ya ubepari huuwawa bila ya hatia, wamekuwa ni wahanga wa mauaji mbalimbali bila hata ya kuwa na hatia. Mauaji ya kimbari, mauwaji ya Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati, vita vya Iraq, Afghanistan, Somalia, Syria, vita vya wenyewe kwa wenyewe na aina nyingine za uvunjifu wa amani zimekuwa  zinawaathiri  sana kwani wamekuwa wanauwawa kwa makundi bila ya kuwa na mtetezi wa kuwatetea. Vita nyingi zimewafanya wanawake ama wafe, kubaki vilema wa maisha kutokana na majeraha yanayotokana na mapigano hayo na zaidi kukosa wa kusimamia maisha yao baada ya kupoteza waume zao na watoto wao. Na vita vyote hivi husababishwa na nchi za kibepari katika  ugomvi wa kunyonya rasilmali na kulinda mfumo wao batil wa kibepari.

Wanawake ndani ya ubepari hupewa malipo kidogo kuliko kazi wanazokuwa wanazifanya.Ingawa kuna sheria kama “equal pay” kwa miaka 30 katika nchi zilizoendelea lakini wanawake bado wanapata malipo kidogo kuliko wanaume. Hili halishangazi kwani wanawake walihamasishwa kufanya kazi kutokana na hitajio  la mpito kiuchumi. Pale walipotakiwa kuchangia kwenye uchumi vilipoibuka  vita vya pili vya dunia  “ sababu kubwa ya kuwainua wanawake ni hitajio la kiuchumi………….. mageuzi ya kiuchumi yalileta hitajio la ajira kwa wanawake, ambayo linahamasisha vita ya sasa…………. Kuwahusisha wanawake kwenye uchumi na mabadiliko ya kijamii  na mabadiliko  ya kijamii yaliyotokana nayo yaliendelea kipindi cha vita na baada na hata kuleta mabadiliko ya kisheria kuwapendelea wanawake. Haya  yalileta mabadiliko ya kijamii na kifamilia”  Pia huelezea ni kwa nini baada ya karne ya kulingania usawa na haki za wanawake, karne ya 20 ilimalizika na Uingereza kuwa na asilimia 4 tu ya mahakimu, 11% wakurugenzi na 2% ya FTSE , wakurugenzi 100 wanawake. Mwanamke anayefanya kazi huku akiwa na watoto huwa anahuzunika  kwa muda mdogo anaoutumia na watoto wake. Huku hujikuta kwenye msuguano kati ya kuwa mke mwema na kazi yake. Katika familia nyingi bado mwanamke mfanyakazi hayajapunguza wajibu wake wa nyumbani.  Mwanasholojia Joseph h Pleck ananukuliwa:    “wasomi wote hukubaliwa hata kwenye tafiti kama wa 4 wenye wake walioajiriwa hufanya kazi zaidi za nyumbani, ongezeko ni dogo na wanawake walioajiriwa bado wanaendelea kufanya kazi nzito za ndani ya familia.”  Siku yake huitumia kufanya jukumu moja kwenda lingine; kutengeneza chai kwa familia yake, kuwaosha wanawe, kwenda kazini, kuwapeleka watoto shuleni. Mara kadhaa wanawake huhisi kushindwa kufanya majukumu yake kwa kiwango cha juu kwa sababu huchoka sana. Lisa Belkin katika kitabu chake cha “life’s work: confessions of an unbalanced mom”  ameandika “ hakuna mmoja yetu mwenye uwezo kutoa 100% yetu kwenye kazi zetu na 100% kwenye familia zetu na 100% ya kujihudumia wenyewe”

Itaendelea………

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.