Kazi ya Mwajiriwa kwa Malipo ya Asilimia Bila ya Malipo Maalumu Yenye Kujulikana

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh…

Siku hizi linatumika sana neno asilimia, mfano, mwezi huu ukiuza kwa dinari 120000 chako ni robo asilimia na kama hukuuza huna kitu, je hali hii inafaa (inajuzu)?

Jibu

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh

Mwajiriwa anaefanya kazi kwa mfanyabiashara katika sehemu ya mauzo, ni lazima malipo yake yawe yanajulikana, na inafaa kuongezwa kwenye hayo malipo asilimia (fulani) ya mauzo, mfano kwa mwezi malipo yake yatakuwa 100, akazidishiwa 10% ya kiasi (cha fedha) za mauzo ambayo ameuza.

Ama malipo yake kuwa ya asilimia ya mauzo tu, yaani akiuza analipwa 10% na ikiwa hakuuza halipwi chochote, mas-ala haya yana kauli kadhaa… Na ambayo naipa nguvu katika mas-ala haya ni kwamba kazi ya mwajiriwa na mtu kama kumuuzia katika sehemu yake ya biashara na kuwa malipo yake ni asilimia ya mauzo anayoyauza, yaani akiuza hulipwa asilimia (fulani) katika mauzo, na akiwa hakuuza halipwi chochote,  yenye nguvu (raajih) kwangu ni kuwa hii haifai kwasababu mwajiriwa ni lazima awe na malipo yenye kujulikana… Na inawezekana kuongezewa asilimia ya mauzo, lakini haifai kuwa malipo ya mwajiriwa kuwa asilimia ya mauzo yake, akiuza alipwe malipo ya asilimia na akiwa hajauza halipwi chochote…

Hayo ni kwa dalili zifuatazo:

Ametoa Ibn Abi Shaiba katika muswanif wake kutoka kwa Abi Huraira na Abi Said wamesema: “Mwenye kumuajiri mwajiriwa basi na amjuze malipo yake”

Na ametoa Baihaqy katika Al-Sunan Al-Swaghir kutoka kwa Abi Huraira amesema: kasema Mtume (SAW): “Mpe mwajiriwa malipo yake kabla halijakauka jasho lake”

Kwahiyo, hakika ya mwajiriwa lazima awe na malipo katika kazi yake, na wala haifai afanye kazi kwa mwengine (muajiri) bila ya malipo. Hii ndio (rai) ninayoipa nguvu (raaji) mimi katika mas-ala haya. Na Allah ndie Mjuzi zaidi na Mwenye hekima zaidi.

Ndugu yenu Attah ibn Khalil Abu Rashtah

18 Jamad al-ula 1435

19-03-2014

Maoni hayajaruhusiwa.